Skip to main content

Tenzi za Rohoni

Tenzi za Rohoni

Tenzi za Rohoni 115 – Kilima kando Ya Mji

Tenzi za Rohoni 115 – Kilima kando Ya Mji Tenzi Na. 115 Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 115, “Kilima kando Ya Mji”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza. Maneno ya Wimbo Kilima kando ya mji Alikufa Bwana; Kuokoa wakosaji Akateswa sana. Kabisa hayasemeki, Mateso dhaifu Alikufa mwenye Haki Tupate wokovu. Alimwaga damu yake Ili tuwe wema, Tufae kukaa kwake Mbinguni daima. Hatuna mwenye imani Aliye na haki, Wa kutosha yetu deni, Rafiki Yesu tu. Alijua peke yake Kufungu Mbingu Ufunguo damu yake Kondoo wa Mungu. Aliyetupenda hivyo Nasi tumpende, Tukamtumai vivyo Na kazi tutende. ← Tenzi 114 | Tenzi Zote | Tenzi 116 → Tazama Tenzi za Rohoni 1–164 Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

Tenzi za Rohoni

Tenzi za Rohoni 114 – Bwana Mungu, Nashangaa Kabisa

Tenzi za Rohoni 114 – Bwana Mungu, Nashangaa Kabisa Tenzi Na. 114 Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 114, “Bwana Mungu, Nashangaa Kabisa”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza. Maneno ya Wimbo Bwana Mungu, nashangaa kabisa Nikitazama kama vilivyo Nyota, ngurumo, vitu vingi vyote viumbwavyo kwa uwezo wako. Roho yangu na ikuimbie Jinsi Wewe ulivyo Mkuu, Roho yangu na ikuimbie Jinsi Wewe ulivyo Mkuu. Nikitembea pote duniani, Ndege huimba, nawasikia, Milima hupendeza macho sana, Upepo nao nafurahia. Nikikumbuka kama Wewe Mungu Ulivyompeleka Mwanao, Afe azichukue dhambi zetu, Kuyatambua ni vigumu mno. Yesu Mwokozi utakaporudi Kunichukua kwenda Mbinguni, Nitashukuru na kwimba milele, Wote wajue jinsi ulivyo. ← Tenzi 113 | Tenzi Zote | Tenzi 115 → Tazama Tenzi za Rohoni 1–164 Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

Tenzi za Rohoni

Tenzi za Rohoni 113 – Ni Mfalme Wa Mapenzi

Tenzi za Rohoni 113 – Ni Mfalme Wa Mapenzi Tenzi Na. 113 Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 113, “Ni Mfalme Wa Mapenzi”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza. Maneno ya Wimbo Ni Mfalme wa mapenzi Ndiye anichungaye, Sipungukiwi, hawezi. Kunipoteza yeye. Kando ya mji mazima Yeye huniongoza Katika malisho mema Daima hunilaza. Mara nyingi hupotea Kwa ukaidi wangu, Naye huniandamia, Hunirudisha kwangu. Uvulini mwa mauti, Siachi hatari kamwe, Wewe Bwana huniachi, Mwokozi wangu wewe. Waniandikia meza Neema kwako tele. Kwa wewe, yote naweza. Na msalaba mbele. Kamwe hautapungua Uule wema wako; Mwisho, atanichukua, Juu, niimbe kwako. ← Tenzi 112 | Tenzi Zote | Tenzi 114 → Tazama Tenzi za Rohoni 1–164 Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

Tenzi za Rohoni

Tenzi za Rohoni 112 – Nilikupa Wewe, Maisha Yangu

Tenzi za Rohoni 112 – Nilikupa Wewe, Maisha Yangu Tenzi Na. 112 Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 112, “Nilikupa Wewe, Maisha Yangu”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza. Maneno ya Wimbo Nilikupa wewe Damu ya moyoni, Ili wokolewe, Winuke ufuni: Nimekunyimani? Umenipa nini? Nilikupa miaka Yangu duniani Upate inuka, Kuishi Mbinguni: Nimekunyimani? Umenipa nini: Niliacha nuru Za Baba, Mbinguni, Kwingia taabu Za ulimwenguni: Nimekunyimani? Umenipa nini? Niliteswa sana, Mateso kifoni, Usije yaona Hayo ya motoni: Nimekunyimani? Umenipa nini? Nimekuletea Huku duniani Upendo na afya Zatoka Mbinguni: Nimekunyimani? Umenipa nini? Nipe siku zako, Udumu mwangani; Na taabu yako, Wingie rahani Nafsi, pendo, mali, Twae Imanweli. ← Tenzi 111 | Tenzi Zote | Tenzi 113 → Tazama Tenzi za Rohoni 1–164 Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

Tenzi za Rohoni

Tenzi za Rohoni 111 – Neno,Lako Bwana

Tenzi za Rohoni 111 – Neno,Lako Bwana Tenzi Na. 111 Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 111, “Neno,Lako Bwana”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza. Maneno ya Wimbo Neno lako, Bwana, Ni imara sana; Lilo latwongoza, Lilo latufunza. Adui wabaya Wakikaribia, Neno lake Bwana Ni ulinzi sana. Siku za dhoruba Soma ukiomba; Neno lake Bwana Msaada sana. Ukiliamini, Hwenda na amani; Una na furaha Neno ni siraha. Ni furaha kweli, Na wingi wa mali, Neno lake Bwana Kwa wasiokana Neno la rehema, Tukali wazima; Faraja I papo, Tufarikanapo. ← Tenzi 110 | Tenzi Zote | Tenzi 112 → Tazama Tenzi za Rohoni 1–164 Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

Tenzi za Rohoni

Tenzi za Rohoni 110 – Mapya Ni Mapenzi Hayo

Tenzi za Rohoni 110 – Mapya Ni Mapenzi Hayo Tenzi Na. 110 Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 110, “Mapya Ni Mapenzi Hayo”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza. Maneno ya Wimbo Mapya ni mapenzi hayo, Asubuhi tunayo, Saa za giza hulindwa Kwa uzima kuamshwa. Kila siku, Mapya pia Rehema, wema, na afya, Wokofu, na msamaha, Mawazo mema, furaha. Tukijitahidi leo Na mwendo utupasao, Mungu atatueleza Yatakayompendeza. Mambo yetu ya dunia Mungu atayang’aria, Matata atageuza Yawe kwetu ya Baraka. Yaliyo madogo, haya Mungu tukimfanyia, Yatosha: tutafaidi Huvuta kwake zaidi. Ewe Bwana, siku zote, Tusaidie kwa yote: Mwendo wetu wote vivyo, Uwe kama tuombavyo. ← Tenzi 109 | Tenzi Zote | Tenzi 111 → Tazama Tenzi za Rohoni 1–164 Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

Tenzi za Rohoni

Tenzi za Rohoni 109 – Nitaimba Na Yesu

Tenzi za Rohoni 109 – Nitaimba Na Yesu Tenzi Na. 109 Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 109, “Nitaimba Na Yesu”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza. Maneno ya Wimbo Nitaimba ya Yesu, Kwa rehema zake, Baraka nyingi sana Nimepata kwake; Nitaimba ya Yesu, Sadaka ya Mungu, Alimwaga damu Ukombozi wangu. Nitaimba ya Yesu Hapa siku zote, Nitakapokumbuka Vyema vyake vyote; Nitaimba ya Yesu Hata mashakani, Yeye atanilinda Mwake ubavuni. Nitaimba ya Yesu Niwapo Njiani; Takaza Mwendo, hata Nifike Mbinguni; Nikiisha ingia Mlangoni mle, Yesu nitamwimbia Mbinguni milele. ← Tenzi 108 | Tenzi Zote | Tenzi 110 → Tazama Tenzi za Rohoni 1–164 Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

Tenzi za Rohoni

Tenzi za Rohoni 108 – Twenenda Sayuni

Tenzi za Rohoni 108 – Twenenda Sayuni Tenzi Na. 108 Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 108, “Twenenda Sayuni”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza. Maneno ya Wimbo Mpendao Bwana Ije raha yenu! Imbeni nyimbo za raha Wa ibada yenu. Twenenda Sayuni, Mji mzuri Sayuni; Twenenda juu Sayuni Ni maskani ya Mungu. Wasiimbe wao wasioamini, Watoto wa Mungu ndio waimbao chini. Twaona rohoni Baraka za Mungu, Tusijafika Mbinguni Kwenye utukufu. Tutakapo mwona Masumbuko basi, Huwa maji ya uzima, Anasa halisi. Tupaaze sauti, Na fute machozi, Twenenda kwa Imanweli Naye ni Mwokozi. ← Tenzi 107 | Tenzi Zote | Tenzi 109 → Tazama Tenzi za Rohoni 1–164 Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

Tenzi za Rohoni

Tenzi za Rohoni 107 – Ewe,Baba Wa Mbinguni

Tenzi za Rohoni 107 – Ewe,Baba Wa Mbinguni Tenzi Na. 107 Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 107, “Ewe,Baba Wa Mbinguni”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza. Maneno ya Wimbo Ewe, Baba wa Mbinguni, Usikie twombalo Hapa chini duniani, Na uwe radhi nalo Ee Mungu, bariki Ndugu hawa wawili! Ee Mungu, bariki Ndugu hawa wawili! Watu hawa mbele zako, Na mbele ya kanisa; Watimize Neno lako Wanakutana sasa. Kama Yesu na Kanisa, Ni mmoja, na hivyo, Watu hawawape sasa Wawe mmoja vivyo Walinde, Bwana, daima, Wabariki nyumbani Uwape nyingi salama Humu ulimwenguni. Wabariki, ewe Bwana, Watu hawa wawili, Wape upaji wa wana, Wafurahishwe kweli. Siku za duniani Zitakapopungua, Wape kurithi Mbinguni Mema ya kwendelea. ← Tenzi 106 | Tenzi Zote | Tenzi 108 → Tazama Tenzi za Rohoni 1–164 Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

Tenzi za Rohoni

Tenzi za Rohoni 106 – Mungu Awe Nanyi Daima

Tenzi za Rohoni 106 – Mungu Awe Nanyi Daima Tenzi Na. 106 Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 106, “Mungu Awe Nanyi Daima”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza. Maneno ya Wimbo Mungu awe nanyi daima, Hata twonane ya pili, Awachunge kwa fadhili, Mungu awe nanyi daima. Hata twonane huko juu, Hata twonane kwake kwema; Hata twonane huko juu, Mungu awe nanyi daima. Mungu awe nanyi daima; Ziwafunike mbawaze, Awalishe, awakuze; Mungu awe nanyi daima. Mungu awe nanyi daima; Kila wakati wa shani Awalinde hifadhini; Mungu awe nanyi daima. Mungu awe nanyi daima; Awabarikie sana, Awapasulie kina; Mungu awe nanyi daima. ← Tenzi 105 | Tenzi Zote | Tenzi 107 → Tazama Tenzi za Rohoni 1–164 Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

banner
Scroll to Top