Skip to main content

Tenzi za Rohoni

Tenzi za Rohoni

Tenzi za Rohoni 125 – Ati Twonane Mtoni?

Tenzi za Rohoni 125 – Ati Twonane Mtoni? Tenzi Na. 125 Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 125, “Ati Twonane Mtoni?”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza. Maneno ya Wimbo Ati twonane mtoni? Maji mazuri ya Mbingu; Yanatokea mwangani, Penye kiti cha Mungu. Naam, twonane mtoni! Watakatifu, kwenu ni mtoni! Tutakutanika mtoni Penye kiti cha Mungu. Tukitembea mtoni Na Yesu mchunga wetu Daima tu ibadani Usoni pake kwetu. Kwang’ara sana mtoni Cha Mwokozi ni kioo, Milele hatuachani, Tumsifu kwa nyimbo. Si mbali sana mtoni, Karibu tutawasili, Mara huwa furahani Na amani ya kweli. ← Tenzi 124 | Tenzi Zote | Tenzi 126 → Tazama Tenzi za Rohoni 1–164 Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

Tenzi za Rohoni

Tenzi za Rohoni 124 – Mungu Ulisema

Tenzi za Rohoni 124 – Mungu Ulisema Tenzi Na. 124 Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 124, “Mungu Ulisema”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza. Maneno ya Wimbo Mungu ulisema, Giza ilikoma; Twakushukuru! Twakusihi sote, Duniani mote Na kwa watu wote, Iwe nuru. Yesu ulikuja, Ulituletea Nuru kuu; Macho kwa vipofu, Maisha kwa wafu; Twakushukuru. Roho kiongozi, Roho wa mapenzi Tia nuru; Mwovu hata sasa Watu huwatosa, Tunakwomba hasa, Iwe nuru. Mungu wa utatu Mwanga wao watu, Tuwe huru; Twende kote-kote Wafundishwe wote, Duniani mote, Iwe nuru. ← Tenzi 123 | Tenzi Zote | Tenzi 125 → Tazama Tenzi za Rohoni 1–164 Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

Tenzi za Rohoni

Tenzi za Rohoni 123 – Nimeketi Mimi Nili Kipofu

Tenzi za Rohoni 123 – Nimeketi Mimi Nili Kipofu Tenzi Na. 123 Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 123, “Nimeketi Mimi Nili Kipofu”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza. Maneno ya Wimbo Nimeketi mimi nili kipofu Gizani nangojea macho; Ewe Bwana Yesu mwenye wokovu, Ondoa dhambi zangu nzito. Huruma hakuna aonaye, Gizani nagojea macho, Sasa nitakase nikusihiye, Yesu, na dhambi zangu nzito. Tangu siku nyingi nimepofuka Natamani uso nikwone; Ewe Bwana Yesu, mwenye baraka Sema neno, basi, nipone. Nimeketi mimi nili na giza, Nami ya kutumai sina; Ili nasikia kunong’oneza, “Kwake Yesu kuna kupona.” ← Tenzi 122 | Tenzi Zote | Tenzi 124 → Tazama Tenzi za Rohoni 1–164 Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

Tenzi za Rohoni

Tenzi za Rohoni 122 – Bwana Yesu

Tenzi za Rohoni 122 – Bwana Yesu Tenzi Na. 122 Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 122, “Bwana Yesu”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza. Maneno ya Wimbo Bwana Yesu, Bwana Yesu, Mbona unaumia? Unateseka sana, Kwa ajili ya kuomba, Waomba na jasho jingi likageuka damu. Kumbe! Ni dhambi zangu zinazokuumiza. Bwana wangu, Mungu wangu, Mimi leo, naja kwako Ili niziungame. Bwana Yesu, Bwana Yesu, Mbona unaumia, na mizigo mizito? Umejitwalia wewe, msalaba mabegani Kwa ajili ya watu. Bwana Yesu, Bwana Yesu, Mbona unatukanwa, wawambwa kama mwizi, Bila kosa ukalia, Baba yangu, wasamehe, Chukua roho yangu. Bwana Yesu, Bwana Yesu, Muda ulipofika, nchi ikawa giza, Mbinguni pakatulia, Angani pakawa kimya, Watu wakaogopa. Bwana Yesu, Bwana Yesu, Jinsi ulivyoumwa, ukamwomba Baba, Leo umeshinda kifo, sasa wapaa Mbinguni, Naimba, Haleluya. ← Tenzi 121 | Tenzi Zote | Tenzi 123 → Tazama Tenzi za Rohoni 1–164 Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

Tenzi za Rohoni

Tenzi za Rohoni 121 – Liko Lango Moja Wazi

Tenzi za Rohoni 121 – Liko Lango Moja Wazi Tenzi Na. 121 Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 121, “Liko Lango Moja Wazi”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza. Maneno ya Wimbo Liko lango moja wazi, Ni lango la mbinguni; Na wote waingiao Watapata nafasi. Lango ndiye Yesu Bwana Wote waingie kwake, Lango! Lango La Mbinguni ni wazi. Yesu ndiye lango hili, Hata sasa ni wazi, Kwa wakubwa na wadogo, Tajiri na maskini. Hili ni lango la raha, Ni lango la rehema; Kila mtu apitaye Hana majonzi tena. Tukipita lango hili Tutatua mizigo, Tuliochukua kwanza, Tutavikwa uzima. Hima ndugu tuingie Lango halijafungwa, Likifungwa mara moja Halitafunguliwa. ← Tenzi 120 | Tenzi Zote | Tenzi 122 → Tazama Tenzi za Rohoni 1–164 Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

Tenzi za Rohoni

Tenzi za Rohoni 120 – Enyi Wanadamu

Tenzi za Rohoni 120 – Enyi Wanadamu Tenzi Na. 120 Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 120, “Enyi Wanadamu”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza. Maneno ya Wimbo Enyi wanadamu mbona Sana mwatanga-tanga, Kama kondoo wanyonge, Wasio na mchunga? Yuko mchunga mmoja Mwenye mapenzi mema; Haya kutaneni kwake, Atawachunga vyema. Mungu tunamwona kuwa Mwenye uwezo wote; Na nguvu zake zapita Mawazo yetu yote: Ni Baba,mapenzi yake Ni makubwa hakika; Hatuwezi kuyajua, Na hayana mpaka. Rehema za Mungu nazo Zina upana sana; Kama huo wa bahari, Mwisho wake hapana; Haki yake ina mema, Kwa hayo twashukuru, Kwetu uko msamaha, Furaha na uhuru. Mapenzi yake mapana, Sisi hatuna cheo Cha kutosha, nao moyo Una wema upeo; Ukombozi mwingi mno Katika damu yake; Sote twapata furaha, Kwa maumivu yake. Yesu mkaribieni Njoni msife myoyo; Njoni kwake kwa imani, Mema yake ni hayo; Heri tuwe kama wana Tushike neno lake, Daima atujaza Tele furaha yake. ← Tenzi 119 | Tenzi Zote | Tenzi 121 → Tazama Tenzi za Rohoni 1–164 Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

Tenzi za Rohoni

Tenzi za Rohoni 119 – Si Damu Ya Nyama

Tenzi za Rohoni 119 – Si Damu Ya Nyama Tenzi Na. 119 Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 119, “Si Damu Ya Nyama”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza. Maneno ya Wimbo Si damu ya nyama Iliyomwagika Iwezayo kuondoa Dhambi za wakosa. Yeye Bwana Yesu Sadaka ya Mungu, Mwenye damu ya thamani, Ni mwokozi kweli. Kwa imani yangu, Namshika yeye, Naziweka dhambi zangu Juu ya kichwa chake. Mzigo wa dhambi Sichukui tena, Ameuchukua yeye, Juu ya msalaba. Bwana Yesu ndiye, Mwokozi wa kweli Tumsifu siku zote, Twapata uhuru. ← Tenzi 118 | Tenzi Zote | Tenzi 120 → Tazama Tenzi za Rohoni 1–164 Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

Tenzi za Rohoni

Tenzi za Rohoni 118 – Ni Ujumbe Wa Bwana

Tenzi za Rohoni 118 – Ni Ujumbe Wa Bwana Tenzi Na. 118 Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 118, “Ni Ujumbe Wa Bwana”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza. Maneno ya Wimbo Ni ujumbe wa Bwana, Aleluya! wa maisha ya daima, Amenena mwenyewe, Aleluya! Utaishi ukitazama. Tazama, ishi sasa! Kumtazama Yesu, Amenena mwenyewe, Aleluya! Utaishi ukitazama. Ni ujumbe wa wema, Aleluya! Nawe shika, rafiki yangu! Ni habari ya raha Aleluya! Mwenye kuinena ni Mungu. Uzima wa daima,Aleluya ! Kwake Yesu utauona. ukimtazama tu, Aleluya! Wokovu u pweke kwa Bwana. ← Tenzi 117 | Tenzi Zote | Tenzi 119 → Tazama Tenzi za Rohoni 1–164 Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

Tenzi za Rohoni

Tenzi za Rohoni 117 – Tufani Inapovuma

Tenzi za Rohoni 117 – Tufani Inapovuma Tenzi Na. 117 Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 117, “Tufani Inapovuma”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza. Maneno ya Wimbo Tufani inapovuma Sana moyoni mwangu, Huona pa kujificha Mkononi mwa Mungu. Hunificha, hunificha Adui hatanipata, Hunificha, hunificha, Mkononi mwake. Pengine kuna taabu Yanisongeza kwake; Naijua si hasira, Ni ya mapenzi yake. Adui wakiniudhi Nami nikisumbuka, Mungu atavigeuza Vyote viwe baraka. Niishipo duniani Ni tufani daima, Anilindapo rohoni Nitakaa salama. ← Tenzi 116 | Tenzi Zote | Tenzi 118 → Tazama Tenzi za Rohoni 1–164 Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

Tenzi za Rohoni

Tenzi za Rohoni 116 – Bwana U Sehemu Yangu

Tenzi za Rohoni 116 – Bwana U Sehemu Yangu Tenzi Na. 116 Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 116, “Bwana U Sehemu Yangu”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza. Maneno ya Wimbo Bwana u sehemu yangu, rafiki yangu wewe; Katika safari yangu, tatembea na wewe; Pamoja na wewe, pamoja na wewe, katika safari yangu, tatembea na wewe. Mali hapa sikutaka, ili niheshimiwe, na yanikute mashaka, sawa sawa na wewe. Pamoja na wewe, pamoja na wewe, heri nikute mashaka sawasawa na wewe. Niongoze safarini, mbele unichukue, mlangoni kwa mbinguni, niingie na wewe. Pamoja na wewe, pamoja na wewe, mlangoni kwa mbinguni, niingie na wewe. ← Tenzi 115 | Tenzi Zote | Tenzi 117 → Tazama Tenzi za Rohoni 1–164 Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

banner
Scroll to Top