Tenzi za Rohoni 135 – Mapenzi Ya Milele
Tenzi za Rohoni 135 – Mapenzi Ya Milele Tenzi Na. 135 Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 135, “Mapenzi Ya Milele”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza. Maneno ya Wimbo Mapenzi ya milele Ndiyo yanipendezayo; Yalinipenda mbele, Sina fahamu nayo; Sasa amani yake Tele rohoni mwangu, Ni mimi kwa kuwa wake, Na yeye kuwa wangu, Ni mimi kuwa wake, Na yeye kuwa wangu Mbingu zinang’ara juu, Na nchi nayo vivyo; Macho ya dunia tu Hayajaona hivyo; Nyuni huimba sana, Maua yana rangi, Ni kumjua Bwana Na pendo zake nyingi, Ni kumjua Bwana Na pendo zake nyingi, Mambo mengi maovu Nayo yenye kutisha, Sasa hayana nguvu, Si yenye kututisha; Ni mkononi mwake, Nalindwa salamani Ninajua ni wake, Ni wake mapenzini. Ninajua ni wake, Ni wake mapenzini. Wake hata milele, Si kutengana tena; Hunipa raha tele Moyoni mwangu, Bwana; Hiyo nchi na Mbingu Zitatoweka zile, Ni wake, Yeye wangu, Milele na milele. Ni wake, Yeye wangu, Milele na milele. ← Tenzi 134 | Tenzi Zote | Tenzi 136 → Tazama Tenzi za Rohoni 1–164 Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android