Tenzi za Rohoni 132 – Sauti Sikilizeni
Tenzi Na. 132
Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 132, “Sauti Sikilizeni”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza.
Maneno ya Wimbo
Sauti sikilizeni
Za waimbao juu,
“Aleluya, Aleluya,
Aleluya, mkuu!”
Wako makundi-makundi
Kama nyota wang’ara,
Kwa makuti ya mitende,
Na meupe wamevaa.
Wazazi na manabii
Wafanyaji wa njia;
Mashahidi, waandishi,
Nao wafalme pia!
Mabikira kina-mama,
Wajane wa kusali,
Waimba wakikutana
“Msifunu Imanweli”.
Watu toka huzunini
Wameosha na nguo,
Ni kwa damu yake Yesu;
Maonjo, mbali nao!
Walitekwa, walikatwa
Hata kwa misumeno,
Kwao kifo na shetani
Walishindiwa mno.
Mungu mumo mwake Mungu,
Nuru mumu mwa nuru,
Kwa kufungamana mwako
Tutaishi mahuru;
Tujalize, Imanweli,
Kujaa kwako wewe
Mungu Baba, Mungu Mwana,
Mungu Roho, tunawe.