Skip to main content

Tenzi za Rohoni

Tenzi za Rohoni

Tenzi za Rohoni 145 – Ndoa Yetu Nzima

Tenzi za Rohoni 145 – Ndoa Yetu Nzima Tenzi Na. 145 Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 145, “Ndoa Yetu Nzima”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza. Maneno ya Wimbo KIITIKIO: /: Ndoa yetu, Bwana, ndiwe baraka! :/ 1. Ndoa yetu nzima simika, Yesu! Usiku na mchana uwepo kwetu. Leo tuna raha, wewe watupa. 2. Atoka kijana, ataka mchumba. Siku zinapita za kupimana. Leo twapatana pamoja kukaa. 3. Vyote hapa chini vinakaa muda, vyote vinaoza, tena vyachakaa. Pendo la dunia nalo huchakaa. 4. Kaa kwetu, Bwana, Kutukagua, pendo letu sisi lisichakae; hivi na tukae na baraka tu. 5. Kana arusini ulialikwa. Walivyoishiwa, ukaongeza, nasi shida zetu utazishinda. ← Tenzi 144 | Tenzi Zote | Tenzi 146 → Tazama Tenzi za Rohoni 1–164 Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

Tenzi za Rohoni

Tenzi za Rohoni 144 – Mbele Ninaendelea

Tenzi za Rohoni 144 – Mbele Ninaendelea Tenzi Na. 144 Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 144, “Mbele Ninaendelea”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza. Maneno ya Wimbo KIITIKIO: Ee Bwana, uniinue, kwa imani nisimame. Nipande milima yote, Ee Bwana, unipandishe. 1. Mbele ninaendelea, ninazidi kutembea. Maombi uyasikie, Ee Bwana, unipandishe. 2. Sina tamani nikae mahali pa shaka, kamwe; hapo wengi wanakaa. Kuendelea naomba. 3. Nisikae duniani, asumbuapo Shetani. Natazamia mbinguni, nitafika na imani. 4. Nataka nipandishwe juu, zaidi yale mawingu. Nitaomba nifikishwe, Ee Bwana, unipandishe. ← Tenzi 143 | Tenzi Zote | Tenzi 145 → Tazama Tenzi za Rohoni 1–164 Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

Tenzi za Rohoni

Tenzi za Rohoni 143 – Nchi Nzuri Yametameta

Tenzi za Rohoni 143 – Nchi Nzuri Yametameta Tenzi Na. 143 Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 143, “Nchi Nzuri Yametameta”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza. Maneno ya Wimbo KIITIKIO: /: Si mbali, karibu, tutaimba na sisi huko! :/ 1. Nchi nzuri yametameta, huonekana kule mbali; naye Yesu hutuongoza, tukafike na sisi huko. 2. Kule tutawaona wengi wapendwao na Yesu Bwana. Tutashirikiana nao, itakuwa furaha kubwa. 3. Tutamwona na Bwana wetu, Yesu Kristo Mwokozi wetu. Tutashangilia daima; tuna hamu ya kwenda kwetu. ← Tenzi 142 | Tenzi Zote | Tenzi 144 → Tazama Tenzi za Rohoni 1–164 Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

Tenzi za Rohoni

Tenzi za Rohoni 142 – Babangu Kule Mbinguni

Tenzi za Rohoni 142 – Babangu Kule Mbinguni Tenzi Na. 142 Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 142, “Babangu Kule Mbinguni”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza. Maneno ya Wimbo 1. Babangu kule mbinguni, aliye juu pa malaika, /: aangalia njia zangu na kunilinda maisha. :/ 2. Hata unywele kichwani hauanguki ovyo tu, /: na siri zote za moyoni zajulikana kwa Baba. :/ 3. Zamani nisipojua, amekwisha kuandika /: mkononi mwake jina langu; ndio upendo wake mkuu. :/ 4. Ee Baba yangu, u mwema, nami nataka kufanya /: kama malaika wafanyavyo mbinguni kwako milele! :/ ← Tenzi 141 | Tenzi Zote | Tenzi 143 → Tazama Tenzi za Rohoni 1–164 Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

Tenzi za Rohoni

Tenzi za Rohoni 141 – Pana Jito, Lina Maji Mazuri

Tenzi za Rohoni 141 – Pana Jito, Lina Maji Mazuri Tenzi Na. 141 Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 141, “Pana Jito, Lina Maji Mazuri”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza. Maneno ya Wimbo KIITIKIO: Ninakuita nawe njoo! Utafute jito hilo! Maji yake yapoza moyo; nawe yateke unywe. 1. Pana jito, lina maji mazuri, yaenda ulimwenguni. Lametameta nalo linang’aa. Walijua jito hilo? 2. Wanywao maji haya wafurahi, waimba kwa shangwe kubwa. Makosa na shida yanaondoshwa, wote waoshwa na Bwana. 3. Jito hilo latoa maji mengi matamu yapendezayo; yaponya wagonjwa, yatia nguvu; uchafu watakasika. 4. Maji ya jito hilo ni uzima unaotoka kwa Yesu. Damu yake yenye kiasi kikuu imemwagwa tusafike. ← Tenzi 140 | Tenzi Zote | Tenzi 142 → Tazama Tenzi za Rohoni 1–164 Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

Tenzi za Rohoni

Tenzi za Rohoni 140 – Mahali Ni Pazuri

Tenzi za Rohoni 140 – Mahali Ni Pazuri Tenzi Na. 140 Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 140, “Mahali Ni Pazuri”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza. Maneno ya Wimbo 1. Mahali ni pazuri ndugu wanapokaa, /: wakipatana vema na wakipendana. :/ 2. Kama umande mzuri unyweshavyo shamba, /: hivyo na Mungu wetu, abariki ndugu. :/ 3. Upendano hujenga boma zuri kwao, /: wakae na amani walioookoka. :/ 4. Na ulimwengu wote wavutwa nuruni, /: halafu kundi moja na Mchunga mmoja tu. :/ ← Tenzi 139 | Tenzi Zote | Tenzi 141 → Tazama Tenzi za Rohoni 1–164 Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

Tenzi za Rohoni

Tenzi za Rohoni 139 – Nuru Ya Rohoni

Tenzi za Rohoni 139 – Nuru Ya Rohoni Tenzi Na. 139 Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 139, “Nuru Ya Rohoni”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza. Maneno ya Wimbo 1. Nuru ya rohoni ni Bwana Yesu. Nakuomba sana niangazishe; ukanitazame kwa huruma tu, /: Ukanitulize mimi maskini. :/ 2. Futa dhambi zangu kwa damu yako. Hasira ya Mungu iniondoke. Machubuko yako, hata mateso, /: Niyawaze vema rohoni mwangu. :/ 3. Nakutumaini peke yako tu, niwe mtumwa wako pote nilipo, utanikubali, sina mashaka! /: Nitakushukuru pasipo mwisho. :/ ← Tenzi 138 | Tenzi Zote | Tenzi 140 → Tazama Tenzi za Rohoni 1–164 Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

Tenzi za Rohoni

Tenzi za Rohoni 138 – Tukutendeleza ( Luganda )

Tenzi za Rohoni 138 – Tukutendeleza ( Luganda ) Tenzi Na. 138 Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 138, “Tukutendeleza ( Luganda )”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza. Maneno ya Wimbo Yesu, Mulokozi wange: Lero nze wuwo wenka; Omusaigwo gunazi’za Yesu Mwana gwendiga. Tukutendereza, Yesu, Yesu Mwana gwendiga; Omusaigwo gunazi’za; Nkwebaza, Mulokozi. Eda nafuba bufubi Okufuna, emirembe; Lero maliride dala Okweyabiza Yesu. Nababuliranga bantu Obulokozi bwona, Obutali bwa kitundu Obulamba obwobuwa Nategezanga ebya Yesu Nobuvumunesitya; Eyanziya mu busibe Nokuwonya eyamponya. Nebaza eyanunula nze; Eyamponya wa kisa! Yesu ankuma Ansanyusaera, Bulijo yebazibwe. ← Tenzi 137 | Tenzi Zote | Tenzi 139 → Tazama Tenzi za Rohoni 1–164 Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

Tenzi za Rohoni

Tenzi za Rohoni 137 – Yesu Mponya

Tenzi za Rohoni 137 – Yesu Mponya Tenzi Na. 137 Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 137, “Yesu Mponya”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza. Maneno ya Wimbo Yesu ndiye mganga wetu Aponya wagonjwa wote; Mganga wetu ni Yesu, Aponyaye hasira. Tumsifu huyo Yesu Tumsifu milele, Kwani Mponya mtakata Mwokozi wa wanyonge Mganga wetu ni Yesu Huondoa matusi; Mganga wetu ni Yesu, Mwenye kuponya choyo. Mganga wetu ni Yesu Huponya wivu wetu; Yesu ndiye aponyae Kelele za nyumbani. Mganga wetu ni Yesu Mponya wa tamaa mbaya; Mganga wetu ni Yesu Uasherati hufuta Mganga wetu ni Yesu Aponya kiu cha pombe, Mganga wetu ni Yesu Kila dhambi uponya ← Tenzi 136 | Tenzi Zote | Tenzi 138 → Tazama Tenzi za Rohoni 1–164 Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

Tenzi za Rohoni

Tenzi za Rohoni 136 – Msifuni, Yesu Ndie Mkombozi

Tenzi za Rohoni 136 – Msifuni, Yesu Ndie Mkombozi Tenzi Na. 136 Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 136, “Msifuni, Yesu Ndie Mkombozi”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza. Maneno ya Wimbo Msifuni ,Yesu ndiye mkombozi; Imbeni ya pendo zake kuu, Sujuduni,malaika mlioko, Jina lake liwe na sifa kuu. Kama vile mchunga uchungavyo Vivyo sisi kutwa atachunga. Msifuni mlio wakw watoto Msifuni aliye mchunga. Msifuni,Yesu ndiye mkombozi; Akateswa tupate ongoka; Ndiye Mwamba,Dhamana ya kuokoka; Sujuduni kwake muangikwa, Yesu aliyeudhiwa na hamu Kwa pendo za baba yake Mungu. Aliyefyolewa na kusulubiwa. Msifuni ndilo letu fungu. Msifuni,Yesu ndiye Mkombozi; Shindukeni,enyi malango juu; Bwana Yesu tangu milele Mwokozi, Mvikeni taji, ni yake tu. Atakuja kuitawala nchi, Yesu,Mwombezi wetu wa Mungu. Msifuni, ni mfalme wa salama; Ndiye kweli mwana wake Mungu. Msifuni, ni mfalme wa salama; Ndiye kweli mwana wake Mungu. ← Tenzi 135 | Tenzi Zote | Tenzi 137 → Tazama Tenzi za Rohoni 1–164 Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

banner
Scroll to Top