Skip to main content

Tenzi za Rohoni

Tenzi za Rohoni

Tenzi za Rohoni 155 – Hapana Rafiki Kama Yesu

Tenzi za Rohoni 155 – Hapana Rafiki Kama Yesu Tenzi Na. 155 Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 155, “Hapana Rafiki Kama Yesu”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza. Maneno ya Wimbo KIITIKIO: Yesu ajua shida zetu, aweza kutuongoza. Hapana rafiki kama Yesu, yu pekee, yu pekee. 1. Hapana rafiki kama Yesu, yu pekee, yu pekee. Hapana mpozi kama Yesu, yu pekee, yu pekee. 2. Yeye anaye sifa, ni Yesu, yu pekee, yu pekee. Ndiye aliye mnyenyekevu, yu pekee, yu pekee. 3. Yesu pamoja nasi daima, yu pekee, yu pekee. Kwa usiku aleta salama, yu pekee, yu pekee. 4. Kulinda Yesu yu mwaminifu, yu pekee, yu pekee. Atawakubali wahalifu, yu pekee, yu pekee. 5. Alipelekwa awe Mwokozi, yu pekee, yu pekee. Anatutayarishia enzi, yu pekee, yu pekee. ← Tenzi 154 | Tenzi Zote | Tenzi 156 → Tazama Tenzi za Rohoni 1–164 Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

Tenzi za Rohoni

Tenzi za Rohoni 154 – Bariki Yote Yawe Mema

Tenzi za Rohoni 154 – Bariki Yote Yawe Mema Tenzi Na. 154 Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 154, “Bariki Yote Yawe Mema”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza. Maneno ya Wimbo KIITIKIO: Kaa kwetu, Bwana, bariki. Uamini, wee ee ndugu, kweli yake Kristo. Jaa utukufu wa Bwana siku zako zote. 1. Bariki yote yawe mema, yote yawe mbaraka. Watu wa nchi za dunia, uwajaze utukufu. 2. Nyumba za wote zibariki kwa jina lako takata. Ujaze utukufu wako nchi zote za dunia. 3. Nyosha mkono ubariki waliojiunga nawe: Wakupokee maishani, watunzwe nawe milele. 4. Bwana, yatunze mambo yote yaliyo mazuri kwako. Uwape wote wakuombao, wafanikishe maisha. ← Tenzi 153 | Tenzi Zote | Tenzi 155 → Tazama Tenzi za Rohoni 1–164 Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

Tenzi za Rohoni

Tenzi za Rohoni 153 – Nimepita Ulimwengu

Tenzi za Rohoni 153 – Nimepita Ulimwengu Tenzi Na. 153 Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 153, “Nimepita Ulimwengu”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza. Maneno ya Wimbo 1. Nimepita ulimwengu. Ulimwengu ni mzuri, lakini natamani ulimwengu mwingine. 2. Nimeona watu wengi, hutafuta daima; maisha yao yote ndiyo taabu na shida. 3. Imebaki hali njema ya furaha ya roho: Hubirini pote pote taabu itatulia. 4. Msalabani pa Golgotha, jerahani mwa Yesu ni mahali penye raha kwao wote kabisa. ← Tenzi 152 | Tenzi Zote | Tenzi 154 → Tazama Tenzi za Rohoni 1–164 Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

Tenzi za Rohoni

Tenzi za Rohoni 152 – Uliyesulibishwa

Tenzi za Rohoni 152 – Uliyesulibishwa Tenzi Na. 152 Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 152, “Uliyesulibishwa”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza. Maneno ya Wimbo 1. Uliyesulibishwa, Mtakatifu Bwanangu, uwe ngao shidani, uniombee mimi. Uliyesulibishwa, Mtakatifu Bwanangu! 2. Wongofu sina hata, niondolee makosa. Mwovu akinishtaki, nasumbuka rohoni. Wongofu sina hata, niondolee makosa. 3. Wewe tu nipokee, nakukimbilia wee. Hata nifanye bidii, nikatoe machozi: Wewe tu nipokee, nakukimbilia wee. 4. Uwe ngao shidani, niombee na mimi! Hapa nikiumizwa, saa ya mwisho ikija: Uwe ngao shidani, niombee na mimi! ← Tenzi 151 | Tenzi Zote | Tenzi 153 → Tazama Tenzi za Rohoni 1–164 Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

Tenzi za Rohoni

Tenzi za Rohoni 151 – Usiku Mtakatifu

Tenzi za Rohoni 151 – Usiku Mtakatifu Tenzi Na. 151 Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 151, “Usiku Mtakatifu”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza. Maneno ya Wimbo 1. Usiku mtakatifu! Wengine walala, wakeshao ni Yosefu tu na Maria waliomlinda Yesu, mwana mzuri, Yesu, mwana mzuri. 2. Usiku mtakatifu! Wachunga wapewa habari nzuri na malaika, zienezwe popote sasa: Yesu Mponya kaja, Yesu Mponya kaja. 3. Usiku mtakatifu! Siku ya furaha imetuangaza Kimungu. Tumeupewa ukombozi: Kristo amefika, Kristo amefika. ← Tenzi 150 | Tenzi Zote | Tenzi 152 → Tazama Tenzi za Rohoni 1–164 Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

Tenzi za Rohoni

Tenzi za Rohoni 150 – Haya, Ee Moyo Wangu

Tenzi za Rohoni 150 – Haya, Ee Moyo Wangu Tenzi Na. 150 Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 150, “Haya, Ee Moyo Wangu”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza. Maneno ya Wimbo 1. Haya, ee moyo wangu, imba kwa furaha. Umwimbie Muumbaji mbingu na dunia. Atukuzwaye pote, umsifu na wewe kwa nguvu zako zote, umri wako wote. 2. Mungu wake Yakobo ndiye Mungu wetu. Ukimchagua yeye, una fungu jema; unacho kitu chema; umepata mali, moyo utakung’aa shida zitakwisha. 3. Ni mwenye nguvu nyingi, hana amshindaye. Kwa hekima aumba, vyote ni ajabu: Misitu na mabonde, milima, mashamba, vilivyo baharini, wanyama porini. 4. Ana mizungu mingi, kuponya wanawe. Anawapa riziki, hata siku za njaa. Wenye chakula haba wanenepa miili; hata waliofungwa anawafungua. 5. Mashangilio yote hayamtoshi yeye. Ni mwema peke yake, nami ni vumbi tu! Ananihurumia kwa kuwa ni wake; kwa hiyo nalikuza jina lake pote. ← Tenzi 149 | Tenzi Zote | Tenzi 151 → Tazama Tenzi za Rohoni 1–164 Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

Tenzi za Rohoni

Tenzi za Rohoni 149 – Haya, Umati Wa Yesu

Tenzi za Rohoni 149 – Haya, Umati Wa Yesu Tenzi Na. 149 Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 149, “Haya, Umati Wa Yesu”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza. Maneno ya Wimbo 1. Haya, umati wa Yesu ulioungwa naye! Haya, enendeni hima katika vita kubwa! Shetani tayari kupigana na sisi! 2. Tumfuate Yesu Kristo, tumwamini yeye tu. Mwovu akituvizia, sisi hatuogopi. Majeshi ya mbingu ni pamoja na sisi! 3. Tukikesha na kuomba Yesu anavyotaka, tukishika Neno lake na tukimtegemea kwa nguvu hizi tu, tutaweza kushinda! 4. Sasa haya, wenzi wangu, tumfuate Yesu tu! Siku za maisha yetu, tuwe katika yeye. Tuache dunia kuingia mbinguni! 5. Pale Mungu atawapa taji walioshinda, wapate urithi wao nyumbani mwa milele. Hayani! Tuimbe, tumsifu Bwana wetu! ← Tenzi 148 | Tenzi Zote | Tenzi 150 → Tazama Tenzi za Rohoni 1–164 Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

Tenzi za Rohoni

Tenzi za Rohoni 148 – Ondokeni! Tunaitwa

Tenzi za Rohoni 148 – Ondokeni! Tunaitwa Tenzi Na. 148 Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 148, “Ondokeni! Tunaitwa”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza. Maneno ya Wimbo 1. Ondokeni! tunaitwa na walinzi wa juu mnarani. Yerusalemu, amka wee! Ni usiku wa manane, yuaja Bwana wa arusi, wanawali wako wapi? Amkeni upesi! Kaziwasheni taa. Haleluya! Fuateni arusini kwenda kumpokea Bwana! 2. Sayuni anasikia moyo waruka kwa furaha, yu macho, anaondoka. Mponya wake anashuka mbinguni mwenye utukufu, aleta mwanga wa kweli; taji yake yaja na Mwana wa Mungu. Hosiana! Twafuata kwenye shangwe tukale karamu yake. 3. Waimbiwa nyimbo nzuri kwa misemo ya watu wote na ya malaika mbinguni. Tukifika mjini kwako kwenye milango ya malulu, tutakuimbia nasi. Furaha kama hii haijasikiwa duniani. Nasi sasa tunaimba, tunakusifu, Ee Bwana. ← Tenzi 147 | Tenzi Zote | Tenzi 149 → Tazama Tenzi za Rohoni 1–164 Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

Tenzi za Rohoni

Tenzi za Rohoni 147 – Tegemea Mpaka Kufa

Tenzi za Rohoni 147 – Tegemea Mpaka Kufa Tenzi Na. 147 Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 147, “Tegemea Mpaka Kufa”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza. Maneno ya Wimbo KIITIKIO: Njoo upesi! Njoo upesi! Fika kwa Bwana Yesu. 1. Tegemea mpaka kufa, utapata wokovu. Bwana Yesu ni Mwokozi, yeye anakupenda. Uje kwake, ‘sikawie, yeye akuokoa. 2. Acha mambo ya dunia yakuhangaishayo. Iko mali ya uzima, unaitiwa hiyo. Mali hiyo ni uzima, utapewa na Bwana. 3. Wakatae, waepuke wanaokudanganya. Ni wajinga, wakuponza, wakupoteza wewe; ila wewe ukatae kuondoka kwa Yesu. 4. Ukijua jambo hilo, usipolifuata, kosa hilo kubwa sana, wapasiwa hukumu. Vumilia, jizuie, utapata uzima. 5. Bwana Yesu amekwisha kukutengenezea kitu chema kwake Mungu, ndiko unakokwenda. Kile kitu upendacho, kule utakipewa. ← Tenzi 146 | Tenzi Zote | Tenzi 148 → Tazama Tenzi za Rohoni 1–164 Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

Tenzi za Rohoni

Tenzi za Rohoni 146 – Neno La Mungu Takata

Tenzi za Rohoni 146 – Neno La Mungu Takata Tenzi Na. 146 Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 146, “Neno La Mungu Takata”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza. Maneno ya Wimbo KIITIKIO: /: Twakushika siku zote maishani na kufani. :/ 1. Neno la Mungu takata lililotoka mbinguni, ambalo moto na panga haziwezi kulishinda. 2. Waliotutangulia, waliokutegemea, wamekufia mashujaa; nasi tulio watoto, 3. Neno la Mungu takata, tukushuhudie nasi kwa neno tamu na tendo kunako wenzi au adui. ← Tenzi 145 | Tenzi Zote | Tenzi 147 → Tazama Tenzi za Rohoni 1–164 Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

banner
Scroll to Top