Tenzi za Rohoni 147 – Tegemea Mpaka Kufa
Tenzi Na. 147
Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 147, “Tegemea Mpaka Kufa”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza.
Maneno ya Wimbo
KIITIKIO:
Njoo upesi! Njoo upesi!
Fika kwa Bwana Yesu.
1. Tegemea mpaka kufa,
utapata wokovu.
Bwana Yesu ni Mwokozi,
yeye anakupenda.
Uje kwake, ‘sikawie,
yeye akuokoa.
2. Acha mambo ya dunia
yakuhangaishayo.
Iko mali ya uzima,
unaitiwa hiyo.
Mali hiyo ni uzima,
utapewa na Bwana.
3. Wakatae, waepuke
wanaokudanganya.
Ni wajinga, wakuponza,
wakupoteza wewe;
ila wewe ukatae
kuondoka kwa Yesu.
4. Ukijua jambo hilo,
usipolifuata,
kosa hilo kubwa sana,
wapasiwa hukumu.
Vumilia, jizuie,
utapata uzima.
5. Bwana Yesu amekwisha
kukutengenezea
kitu chema kwake Mungu,
ndiko unakokwenda.
Kile kitu upendacho,
kule utakipewa.