Tenzi za Rohoni 150 – Haya, Ee Moyo Wangu
Tenzi Na. 150
Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 150, “Haya, Ee Moyo Wangu”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza.
Maneno ya Wimbo
1. Haya, ee moyo wangu,
imba kwa furaha.
Umwimbie Muumbaji
mbingu na dunia.
Atukuzwaye pote,
umsifu na wewe
kwa nguvu zako zote,
umri wako wote.
2. Mungu wake Yakobo
ndiye Mungu wetu.
Ukimchagua yeye,
una fungu jema;
unacho kitu chema;
umepata mali,
moyo utakung’aa
shida zitakwisha.
3. Ni mwenye nguvu nyingi,
hana amshindaye.
Kwa hekima aumba,
vyote ni ajabu:
Misitu na mabonde,
milima, mashamba,
vilivyo baharini,
wanyama porini.
4. Ana mizungu mingi,
kuponya wanawe.
Anawapa riziki,
hata siku za njaa.
Wenye chakula haba
wanenepa miili;
hata waliofungwa
anawafungua.
5. Mashangilio yote
hayamtoshi yeye.
Ni mwema peke yake,
nami ni vumbi tu!
Ananihurumia
kwa kuwa ni wake;
kwa hiyo nalikuza
jina lake pote.