Tenzi za Rohoni 153 – Nimepita Ulimwengu
Tenzi Na. 153
Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 153, “Nimepita Ulimwengu”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza.
Maneno ya Wimbo
1. Nimepita ulimwengu.
Ulimwengu ni mzuri,
lakini natamani
ulimwengu mwingine.
2. Nimeona watu wengi,
hutafuta daima;
maisha yao yote
ndiyo taabu na shida.
3. Imebaki hali njema
ya furaha ya roho:
Hubirini pote pote
taabu itatulia.
4. Msalabani pa Golgotha,
jerahani mwa Yesu
ni mahali penye raha
kwao wote kabisa.