Tenzi za Rohoni 141 – Pana Jito, Lina Maji Mazuri
Tenzi Na. 141
Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 141, “Pana Jito, Lina Maji Mazuri”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza.
Maneno ya Wimbo
KIITIKIO:
Ninakuita nawe njoo!
Utafute jito hilo!
Maji yake yapoza moyo;
nawe yateke unywe.
1. Pana jito, lina maji mazuri,
yaenda ulimwenguni.
Lametameta nalo linang’aa.
Walijua jito hilo?
2. Wanywao maji haya wafurahi,
waimba kwa shangwe kubwa.
Makosa na shida yanaondoshwa,
wote waoshwa na Bwana.
3. Jito hilo latoa maji mengi
matamu yapendezayo;
yaponya wagonjwa, yatia nguvu;
uchafu watakasika.
4. Maji ya jito hilo ni uzima
unaotoka kwa Yesu.
Damu yake yenye kiasi kikuu
imemwagwa tusafike.