Skip to main content

Tenzi za Rohoni 142 – Babangu Kule Mbinguni

Tenzi za Rohoni 142 – Babangu Kule Mbinguni

Tenzi Na. 142

Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 142, “Babangu Kule Mbinguni”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza.


Maneno ya Wimbo

1. Babangu kule mbinguni,
aliye juu pa malaika,
/: aangalia njia zangu
na kunilinda maisha. :/

2. Hata unywele kichwani
hauanguki ovyo tu,
/: na siri zote za moyoni
zajulikana kwa Baba. :/

3. Zamani nisipojua,
amekwisha kuandika
/: mkononi mwake jina langu;
ndio upendo wake mkuu. :/

4. Ee Baba yangu, u mwema,
nami nataka kufanya
/: kama malaika wafanyavyo
mbinguni kwako milele! :/


Tazama Tenzi za Rohoni 1–164


Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

Scroll to Top