Tenzi za Rohoni 144 – Mbele Ninaendelea
Tenzi Na. 144
Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 144, “Mbele Ninaendelea”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza.
Maneno ya Wimbo
KIITIKIO:
Ee Bwana, uniinue,
kwa imani nisimame.
Nipande milima yote,
Ee Bwana, unipandishe.
1. Mbele ninaendelea,
ninazidi kutembea.
Maombi uyasikie,
Ee Bwana, unipandishe.
2. Sina tamani nikae
mahali pa shaka, kamwe;
hapo wengi wanakaa.
Kuendelea naomba.
3. Nisikae duniani,
asumbuapo Shetani.
Natazamia mbinguni,
nitafika na imani.
4. Nataka nipandishwe juu,
zaidi yale mawingu.
Nitaomba nifikishwe,
Ee Bwana, unipandishe.