Vyakula Mbadala vya Kuku
Njia 15 za Kupunguza Gharama za Ufugaji Bila Kushusha Ubora.
Gharama ya chakula cha kuku inachukua takribani 70% ya gharama zote za ufugaji. Ikiwa unategemea chakula cha dukani pekee, faida yako inaweza kuwa ndogo sana. Hapa kuna orodha ya vyakula mbadala 15 unavyoweza kutumia kuchanganya chakula chako mwenyewe na kuokoa pesa.
Vyanzo vya Nishati (Wanga)
Hiki ni chakula kikuu mbadala. Ni rahisi kupata na bei nafuu kuliko mahindi yenyewe. Hakikisha hazina ukungu.
Zina mafuta na protini kidogo. Changanya na pumba za mahindi ili kuku wasikinai. Pia husaidia mmeng’enyo.
Mihogo iliyokaushwa na kusagwa ni chanzo kizuri cha nguvu. Angalizo: Usipe mihogo mibichi, ina sumu ya sianidi.
Machicha ya mbege au duka la pombe. Yafaa kwa kuku wakubwa (Growers/Layers). Usipe vifaranga wadogo.
Vyanzo vya Protini (Kujenga Mwili)
Chanzo kikuu cha protini ya mimea. Mashudu nyeusi yana mafuta zaidi kuliko nyeupe. Muhimu sana kwa kukuza kuku.
Dagaa wa ziwa au bahari. Ina protini bora na Calcium. Muhimu sana kwa kuku wa mayai na vifaranga.
Hupatikana machinjioni. Lazima ichemshe na kukaushwa vizuri kuua wadudu. Ina protini nyingi sana (80%+).
Mabuu ya Inzi Weusi (Black Soldier Fly). Unaweza kuwafuga mwenyewe kwa kutumia mabaki ya jikoni. Chakula cha bure kabisa!
Mmea wa majini unaokua haraka sana. Unaweza kuvunwa kila siku. Hupunguza gharama ya chakula kwa hadi 30%.
Wadudu hawa ni watamu sana kwa kuku. Unaweza kuwatega kwa kutumia chungu na makaratasi/mahindi mabichi.
Majani haya yana protini nyingi. Yakaushe kivulini na usage. Changanya kwa kiasi kidogo (usizidi 5%).
Madini na Vitamini
Mifupa iliyochomwa na kusagwa. Muhimu sana kwa kujenga mifupa imara na ganda gumu la yai.
Chanzo rahisi kabisa cha Calcium. Inapatikana kwa bei nafuu sana madukani. Usitumie chokaa ya kujengea nyumba!
Usitupe maganda! Yachemshe kuua wadudu, yakaushe na uyasage. Ni Calcium safi ya bure kurudisha kwa kuku.
Mchicha, kabichi, na masalia ya matunda. Hupa kuku vitamini na kupunguza stress. Onyo: Usipe vyakula vilivyooza.
Tahadhari Muhimu
Unapotumia vyakula mbadala, ni lazima uhakikishe Mchanganyiko (Formula) uko sawa. Usipe kuku pumba tupu watadumaa. Lazima uchanganye Wanga, Protini, na Madini kwa uwiano sahihi kulingana na umri wa kuku.
Unahitaji Formula ya Kuchanganya Chakula?
Tunaweza kukutumia fomula (vipimo) vya jinsi ya kuchanganya vyakula hivi 15 ili upate chakula bora kabisa (Starter, Grower, Finisher) kwa gharama nafuu.
