TAUSI Taxpayer Portal Tanzania 2026 – Mwongozo Kamili wa Huduma, Faida na Jinsi Inavyofanya Kazi

TAUSI Taxpayer Portal Tanzania 2025 – Mwongozo Kamili wa Huduma, Faida na Jinsi Inavyofanya Kazi

TAUSI Taxpayer Portal Tanzania 2025

Mwongozo Kamili wa Huduma, Faida na Jinsi ya Kutumia Mfumo wa Kidijitali wa Halmashauri

TAUSI Taxpayer Portal ni mfumo rasmi wa kidijitali unaorahisisha upatikanaji wa huduma za kikodi na kiutawala zinazotolewa na Mamlaka za Serikali za Mitaa (LGA) nchini Tanzania. Mfumo huu unasimamiwa chini ya Prime Minister’s Office – Regional Administration and Local Government (TAMISEMI).

TAUSI imekusudiwa kumwezesha mlipakodi (Taxpayer) kupata huduma kwa kujihudumia (self-service) bila usumbufu wa kufika ofisini mara kwa mara. Unaweza kuomba leseni, kulipa kodi, kusajili biashara na kupata huduma nyingine za Halmashauri kwa urahisi kutoka nyumbani au ofisini.

TAUSI Taxpayer Portal ni Nini?

TAUSI ni jukwaa la mtandaoni linalounganisha wananchi, wafanyabiashara na taasisi na Halmashauri zao ili kuomba, kusajili, kusasisha na kulipia huduma mbalimbali kama leseni, vibali, kodi na tozo. Mfumo huu unapunguza urasimu, unaongeza uwazi na kuharakisha utoaji wa huduma za serikali za mitaa.

Ukurasa wa Login wa TAUSI Portal

Ukurasa wa kuingia na kujisajili kwenye TAUSI Taxpayer Portal

Huduma Zinazopatikana Kwenye TAUSI Taxpayer Portal

TAUSI inatoa huduma nyingi za serikali za mitaa zinazoweza kupatikana mtandaoni. Hizi ni baadhi ya huduma kuu:

1. Business License

  • Omba leseni ya biashara
  • Fanya upya (renew) leseni
  • Sitisha (terminate) leseni

2. Liquor License

  • Omba leseni ya pombe
  • Fanya upya leseni
  • Sitisha leseni

3. Hotel Levy

  • Sajili hoteli
  • Wasilisha mauzo (turnover)
  • Lipa tozo za hoteli

4. Building Permit

  • Omba kibali cha ujenzi
  • Pata cheti cha umiliki
  • Pata occupancy certificate

5. Fisheries & Vessel Permits

  • Sajili chombo cha uvuvi
  • Omba leseni za uvuvi
  • Leseni za bidhaa za samaki

6. Service Levy

  • Sajili biashara daraja A
  • Wasilisha mauzo
  • Lipa service levy

7. House Rent

  • Omba kupangisha nyumba
  • Fanya upya nyumba za kupangisha
  • Lipa kodi ya pango

8. e-Auction

  • Jisajili kwenye mfumo
  • Shiriki minada ya serikali
  • Fuata zabuni zilizopo

9. Land Sales

  • Sajili kwa huduma
  • Nunua viwanja
  • Lipa bili za ardhi

10. Parking Services

  • Sajili huduma za maegesho
  • Lipa ada za parking
  • Pata vibali vya maegesho

11. Solid Waste Management

  • Sajili kwa huduma za taka
  • Lipa ada ya usafiri taka
  • Maeneo yaliyowezeshwa

12. Billboard Permits

  • Sajili mabango
  • Omba vibali vya matangazo
  • Lipa ada za billboard

13. Property Tax

  • Sajili mali yako
  • Omba kodi ya majengo
  • Lipa kodi ya mali

Kumbuka: Huduma nyingine zinaweza kuonekana kama “Service Not Activated” kulingana na Halmashauri husika. Kila Halmashauri ina uwezo wa kuwezesha huduma zinazolingana na mahitaji ya eneo lao.

Dashboard ya TAUSI Portal

Dashboard na orodha ya huduma kwenye TAUSI Taxpayer Portal

Jinsi TAUSI Taxpayer Portal Inavyofanya Kazi

Kufanya kazi na TAUSI ni rahisi na salama. Fuata hatua hizi kwa utaratibu:

Hatua za Kutumia TAUSI Portal:

  1. Hatua ya 1: Tengeneza Akaunti
    Tembelea tovuti ya TAUSI: https://tausi.tamisemi.go.tz/ na sajili akaunti kwa kutumia Namba ya Utambulisho wa Taifa (NIN). Hakikisha taarifa zako zote ni sahihi.
  2. Hatua ya 2: Sasisha Taarifa za Kodi
    Kwa Mtu Binafsi: Sasisha TIN binafsi kwenye profaili yako.
    Kwa Taasisi/Biashara: Wasilisha barua ya utambulisho kwa Halmashauri husika ili akaunti yako iongezwe TIN na NIN kulingana na maelezo ya barua.
  3. Hatua ya 3: Omba Huduma
    Chagua huduma unayotaka (leseni, kibali, kodi n.k.) kutoka kwenye orodha ya huduma zilizopo. Jaza fomu za mtandaoni kwa makini na pakia nyaraka zinazohitajika kama nakala za vitambulisho, hati za biashara, n.k.
  4. Hatua ya 4: Fanya Malipo
    Lipa ada au tozo kupitia njia za malipo zilizoainishwa ndani ya mfumo. Unaweza kutumia simu ya mkononi, benki au njia nyingine za malipo ya mtandaoni.
  5. Hatua ya 5: Fuatilia Maombi Yako
    Fuata hatua ya maombi yako moja kwa moja kwenye akaunti yako. Utapokea taarifa za maendeleo kupitia barua pepe na ujumbe mfupi. Pokea majibu na idhini kutoka Halmashauri husika.
Maombi ya Leseni ya Biashara kwenye TAUSI

Mfano wa fomu ya maombi ya leseni ya biashara kwenye TAUSI Portal

Video ya Mwongozo wa Kutumia TAUSI Portal

Tazama video hii ya kujifunza jinsi ya kupata leseni ya biashara na kutumia TAUSI Taxpayer Portal hatua kwa hatua:

Faida za Kutumia TAUSI Taxpayer Portal

  • Huduma 24/7 Bila Kusafiri: Pata huduma muda wowote usiku au mchana bila kwenda ofisini.
  • Uwazi na Ufuatiliaji wa Maombi: Fuata maendeleo ya maombi yako kwa uwazi mkubwa.
  • Kupunguza Muda na Gharama: Okoa muda wa kusafiri na gharama za usafiri kwenda Halmashauri.
  • Kumbukumbu Salama: Hifadhi salama ya malipo, leseni na hati zote za kidijitali.
  • Urahisi wa Malipo: Lipa moja kwa moja kupitia simu au benki.
  • Mazingira Bora: Kupunguza matumizi ya karatasi na kusafiri.

Anza Kutumia TAUSI Leo

Jisajili sasa kwenye TAUSI Taxpayer Portal na upate huduma za Halmashauri kwa urahisi na haraka.

Bofya Hapa Kuanza na TAUSI Portal

Maswali Yanayoulizwa Mara kwa Mara (FAQs)

Je, TAUSI ni bure?

Ndiyo, kujisajili na kutumia portal ni bure. Unalipa tu ada za huduma zinazohitajika kama leseni au kodi.

Je, ninaweza kutumia TAUSI bila TIN?

Kwa huduma za binafsi unaweza, lakini kwa biashara au taasisi TIN inahitajika.

Je, huduma zote zinapatikana katika Halmashauri yangu?

Inategemea Halmashauri. Baadhi ya huduma huwezeshwa hatua kwa hatua.

Pata Msaada wa TAUSI Portal, TIN, BRELA na Huduma Nyingine

Unahitaji msaada wa kujisajili au kutumia TAUSI, kupata TIN au BRELA? Tunakusaidia hatua zote haraka.

Pia tunatoa notes za masomo, past papers, maswali ya mitihani na huduma za kitaalumu.

Tuma ujumbe WhatsApp bila malipo ili tukuweze kukusaidia mara moja.

© 2025 Devine Vision Tech | Msaada wa Biashara na Elimu kwa Watanzania

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Scroll to Top