Ratiba ya Lishe: Siri ya Kukua kwa Kuku na Kupunguza Gharama
Je, unajua kuwa 80% ya gharama zako shambani zinaenda kwenye chakula? Ukikosea hapa, umepoteza faida yote. Jifunze sayansi ya ulishaji inayookoa mfuko wako.
Kwanini Chakula Ndicho Kinaamua Utajiri Wako?
Wafugaji wengi hufikiri kuwa kuku akila sana ndiyo anakua. Huo ni uongo wa kishamba! Kuku hapanwi kama puto; anajengwa kisayansi. Chakula ndicho kinaamua kama utapata mayai mengi, nyama nzito, au utabaki na kuku goigoi wanaokula mtaji wako kila siku.
Mwongozo wa Hatua kwa Hatua wa Lishe
Siku ya 1-14: Hatua ya Starter
Hapa ndipo unajenga msingi (Foundation). Kuku anahitaji protini nyingi (20% – 22%) kwa ajili ya kutengeneza viungo vya ndani na kinga.
- Msisitizo: Hakikisha chakula ni laini (crumbles) na kina vitamini za kutosha.
- Maji: Maji yawe safi na ya kutosha masaa 24. Kuku asiyekunywa maji, hali chakula!
Wiki ya 3-8: Hatua ya Grower
Hapa tunajenga fremu (Mifupa na Ukubwa wa Mwili). Lengo ni kuku akue kimo bila kuwa na mafuta mengi yatakayoziba njia ya yai au kuharibu ladha ya nyama.
- Mbinu: Punguza protini kidogo (16% – 18%) lakini ongeza nishati (Energy).
- Siri: Usiwape kuku mafuta; wape uwezo wa kutengeneza misuli.
Wiki ya 8 Kwenda Juu: Finisher/Layers
Huu ndiyo wakati wa mavuno. Kwa kuku wa nyama, tunahitaji uzito (Weight). Kwa kuku wa mayai, tunahitaji madini ya kalsiamu (Calcium) kwa ajili ya maganda imara ya mayai.
- Broilers: Chakula chenye nishati nyingi ili kuongeza minofu haraka.
- Layers: Ongeza kalsiamu ili kuzuia kuku wasiishie kutaga mayai laini (“vichele”).
Makosa 3 Hatari: Kuepuka Hasara Shambani
1. Kubadilisha Chakula Ghafla
Kuku akishtushwa na mabadiliko ya ghafla ya chakula, tumbo linavurugika na anacha kukua kwa wiki nzima.
2. Chakula Chenye Fangasi
Unyevu husababisha sumu kuvu (Aflatoxins) inayoua kuku kimyakimya na kudhoofisha kinga yao.
3. Kutotumia Vipimo
Kulisha kwa “kukadiria” kwa mkono ni adui wa faida. Tumia mizani au vipimo maalum vya ujazo.
Mbinu za Kisasa za Ulishaji Kuku
Umechoka kununua chakula cha gharama madukani? Kitabu hiki kinakupa Fomula za Siri za kuchanganya chakula nyumbani ukitumia malighafi za bei rahisi na kuokoa hadi 30% ya gharama!
Bei ya Kawaida: TZS 15,000
Fomula za Starter, Grower & Layers.
Mbinu za kupunguza vifo kwa lishe.
Anza Kuokoa Pesa Sasa!
Usisubiri hadi mtaji wako uishe kwenye magunia ya chakula. Pata nakala yako ya kidijitali (PDF) sasa hivi na ubadilishe ufugaji wako kuwa biashara yenye faida kubwa.
Ofa hii ni kwa watu 50 wa kwanza wa leo tu! Namba ya msaada: 0620 339 260.
