Ordinary Diploma in Pharmaceutical Sciences
(Stashahada ya Sayansi ya Dawa)
Taaluma muhimu inayohusu utengenezaji, utunzaji, na utoaji sahihi wa dawa kwa ajili ya kuokoa maisha.
Pharmaceutical Sciences (Famasi) ni moja ya kozi nyeti na zinazoheshimika sana katika sekta ya afya. Wahitimu wa kozi hii (Pharmaceutical Technicians) ndio wataalamu wanaohakikisha wagonjwa wanapata dawa sahihi, kwa kipimo sahihi, na kwa matumizi salama.
1. Sifa za Kujiunga (Admission Requirements)
Kwa mujibu wa mwongozo wa sasa wa NACTVET, ili kujiunga na kozi hii, mwombaji lazima awe na sifa zifuatazo:
- Awe na Cheti cha Kidato cha Nne (CSEE).
- Awe na ufaulu wa Alama “D” Nne (4) au zaidi katika masomo yasiyo ya dini.
- Kati ya hizo “D” nne, LAZIMA kuwe na ufaulu katika masomo haya mawili ya sayansi:
- Chemistry (Kemia) – Lazima uwe na D au zaidi.
- Biology (Biolojia) – Lazima uwe na D au zaidi.
Ufaulu (Pass) katika masomo ya Basic Mathematics na English Language ni sifa ya ziada itakayokupa kipaumbele wakati wa kuchaguliwa (Selection), hasa katika vyuo vya Serikali vyenye ushindani mkubwa.
2. Utajifunza Nini? (Core Modules)
Katika kipindi cha miaka mitatu (NTA Level 4-6), utajifunza mambo ya msingi na ya kitaalamu kuhusu dawa:
Pharmaceutics (Utengenezaji Dawa)
Kujifunza jinsi ya kuchanganya kemikali kutengeneza dawa za maji, vidonge, krimu, na marashi (Compounding).
Pharmacology (Matumizi ya Dawa)
Kuelewa jinsi dawa inavyofanya kazi mwilini, madhara yake (Side effects), na mwingiliano wa dawa (Drug interactions).
Pharmacy Practice
Sheria za dawa, maadili ya kazi, na jinsi ya kuhudumia wagonjwa dirishani (Dispensing) kwa kutoa maelekezo sahihi.
Inventory Management
Jinsi ya kuagiza dawa, kuzihifadhi stoo ili zisiharibike, na kudhibiti muda wa kuisha matumizi (Expiry dates).
3. Fursa za Ajira na Kujiajiri
Soko la ajira kwa wataalamu wa Famasi ni kubwa na linazidi kukua:
4. Muda wa Masomo
Kozi hii inachukua Miaka Mitatu (3) kukamilika:
- Mwaka wa 1 (NTA Level 4): Basic Technician Certificate in Pharmaceutical Sciences.
- Mwaka wa 2 (NTA Level 5): Technician Certificate in Pharmaceutical Sciences.
- Mwaka wa 3 (NTA Level 6): Ordinary Diploma in Pharmaceutical Sciences.
Unataka Kusoma Famasi?
Uchaguzi wa chuo ni muhimu sana. Kuna vyuo vingi vya afya, lakini sio vyote vina vifaa bora vya maabara ya famasi.
Sisi DeVine Vision Tech tunakusaidia kuchagua vyuo bora na kufanya maombi (Admission) kwa usahihi.
Fika ofisini kwetu: Kisesa, Mwanza.
