Ordinary Diploma in Accountancy
(Stashahada ya Uhasibu)
Jenga mustakabali wako katika ulimwengu wa fedha. Kozi yenye heshima, mapato mazuri, na fursa zisizo na kikomo za kujiajiri.
Uhasibu ndio uti wa mgongo wa kila biashara. Hakuna kampuni, shirika la umma, hospitali, shule, wala NGO inayoweza kujiendesha bila mhasibu. Kozi hii inakuandaa kuwa mtaalamu wa fedha anayeaminika, mwenye uwezo wa kusimamia rasilimali, na kutoa ushauri wa kibiashara.
1. Sifa za Kujiunga (Admission Requirements)
Ili uwe mhasibu bora, lazima uwe na msingi mzuri wa mahesabu. Kwa mujibu wa NACTVET, sifa za kujiunga ni:
- Lazima uwe na Cheti cha Kidato cha Nne (CSEE).
- Uwe na ufaulu wa Alama “D” Nne (4) au zaidi katika masomo yasiyo ya dini.
- SHARTI KUU: Moja ya hizo “D” lazima iwe ya somo la Basic Mathematics.
*Kama huna D ya Hesabu, huwezi kusoma Diploma ya Uhasibu moja kwa moja.
- Awe na Basic Technician Certificate (NTA Level 4) katika Accountancy (Uhasibu).
- Hii ni njia mbadala kwa wale waliokosa sifa za moja kwa moja kidato cha nne, wakaanza na cheti (Certificate) na sasa wanapanda ngazi.
2. Kwanini Uchague Kozi Hii? (Faida Zake)
Uhasibu siyo tu kuhesabu pesa; ni taaluma yenye faida nyingi:
Kila biashara mpya inayofunguliwa inahitaji mhasibu. Tofauti na fani nyingine ambazo zinaweza kupitwa na wakati, fedha lazima zisimamiwe daima.
Diploma ya Uhasibu inakupa msingi imara wa kufanya mitihani ya Bodi ya Wahasibu (NBAA). Ukifaulu na kupata CPA (T), unakuwa mmoja wa wataalamu wanaolipwa vizuri zaidi nchini.
Utajifunza kutumia programu za kisasa za uhasibu kama QuickBooks, Tally, na Excel. Hii inakufanya uwe na thamani kubwa sokoni kuliko mtu anayejua nadharia tu.
3. Fursa za Kujiajiri (Self-Employment)
Hutaki kuajiriwa? Uhasibu unakupa nyenzo za kusimama mwenyewe mapema sana:
Wafanyabiashara wengi wadogo na wa kati wanahangaika na makadirio ya kodi za TRA. Unaweza kufungua ofisi ya kuwasaidia kukokotoa kodi, kujaza fomu za marejesho (Returns), na kutunza kumbukumbu zao kwa malipo.
Unaweza kuhudumia kampuni 5 hadi 10 kwa wakati mmoja kama “Mhasibu wa Nje” (Outsourced Accountant). Unawaandalia vitabu vya hesabu, ripoti za mwezi, na kuwashauri jinsi ya kukuza mtaji.
4. Fursa za Ajira (Career Opportunities)
Ukihitimu, unaweza kufanya kazi katika sekta mbalimbali:
Mabenki na Taasisi za Fedha
Kama Loan Officer, Teller, au Back-office Accountant katika mabenki kama CRDB, NMB, na taasisi za mikopo (Microfinance).
Serikali na Halmashauri
Kufanya kazi kama Mhasibu Msaidizi katika Halmashauri za Wilaya, Hospitali za Serikali, na Mashirika ya Umma (Parastatals).
Mashirika ya Kimataifa (NGOs)
Kusimamia fedha za miradi ya wahisani (Donor Funded Projects). Hapa kunahitajika umakini na uadilifu mkubwa.
Sekta Binafsi
Kwenye viwanda, mahoteli, mashule, na kampuni za usafirishaji kusimamia mapato na matumizi.
Ujuzi Utakaopata
Financial Reporting Auditing Taxation (VAT/PAYE) Cost Accounting Computerized Accounting Budgeting Business LawUko Tayari Kuwa Mhasibu?
Kuchagua chuo sahihi ni hatua ya kwanza ya mafanikio. Tunakusaidia kuchagua vyuo vyenye mitaala bora na kukusaidia kufanya maombi (Admission) bila makosa.
Fika ofisini kwetu: Kisesa, Mwanza.
