Mwongozo wa Ajira Portal Tanzania
Hakikisha Ombi Lako Linakubalika kwa Kuzingatia Vigezo Hivi Muhimu.
Mfumo wa Ajira Portal (portal.ajira.go.tz) unaosimamiwa na Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma (PSRS), ni daraja kuu la kuingia katika ajira za serikali Tanzania. Hata hivyo, maelfu ya waombaji hukataliwa kila mwaka kwa makosa madogo yanayoweza kuepukika.
1. Usahihi wa Taarifa za NIDA
Mfumo wa Ajira Portal sasa hivi umeunganishwa moja kwa moja na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA). Hakikisha majina yako yanayosomeka kwenye NIDA yanafanana herufi kwa herufi na yale yaliyopo kwenye vyeti vyako vya kitaaluma.
2. Kupandisha Vyeti (Uploads)
Hapa ndipo waombaji wengi hukosea. Zingatia yafuatayo:
3. Kukamilisha Wasifu (Profile Completion)
Kabla ya kubonyeza kitufe cha “Apply”, hakikisha wasifu wako (Profile) umekamilika kwa 100%. Hii ni pamoja na:
- Taarifa binafsi na anuani.
- Elimu (kuanzia msingi hadi kiwango cha juu).
- Uzoefu wa kazi (Work experience).
- Wadhamini (Referees) wasiopungua watatu.
4. Barua ya Maombi (Application Letter)
Andika barua ya maombi kwa kila nafasi unayoomba. Usitumie barua moja ya jumla kwa kazi tofauti. Hakikisha:
- Inaelekelewa kwa Katibu wa Sekretarieti ya Ajira.
- Inataja “Ref. No” ya tangazo la kazi.
- Imetiwa saini (Signed).
5. Muda wa Kutuma Maombi
Epuka kutuma maombi siku ya mwisho (Deadline). Mara nyingi mfumo unakuwa na msongamano mkubwa na unashindwa kufanya kazi vizuri (System Overload). Tuma maombi yako angalau siku tatu kabla ya tarehe ya mwisho.
