Kwa Nini Huitwi Kwenye Usaili?
Jifunze kusahihisha makosa madogo yanayoigharimu CV yako na kukufanya ukose “Shortlist” kila mara.
Umewahi kutuma maombi ya kazi zaidi ya 50 na hukuwahi kuitwa hata kwenye usaili mmoja? Tatizo sio uwezo wako au vyeti vyako; mara nyingi tatizo ni JINSI unavyowasilisha maombi hayo. Mifumo ya kisasa (kama Ajira Portal na ATS) inachuja maombi kwa sekunde chache.
Makosa 5 Yanayoua Maombi Yako na Tiba Zake
Usitumie CV ileile uliyotuma Bank kuomba kazi Hospitali. Kila tangazo la kazi lina mahitaji tofauti. Mfumo wa kuchuja (ATS) unatafuta maneno maalum (Keywords) yaliyopo kwenye tangazo.
Fanya Hivi: Soma tangazo, chukua maneno muhimu (mfano: “Project Management”, “Data Analysis”), na hakikisha yanatokea kwenye CV yako.
Kama tangazo linasema “Tuma PDF pekee”, ukipandisha Word Document, mfumo unakukataa papo hapo. Pia, usitumie majina ya ajabu kwenye faili kama “CV_Yangu_Mpya_Final_version2.pdf”.
Fanya Hivi: Ipe faili jina rasmi: “Jina_Lako_Nafasi_Unayoomba.pdf” (Mfano: Juma_Juma_Accountant.pdf).
Kwenye Ajira Portal, wengi hujaza elimu na kuacha sehemu ya “Experience” au “Referees” tupu wakidhani wataona kwenye CV. Mfumo huchuja wasifu kabla ya kufungua CV.
Fanya Hivi: Jaza kila kipengele cha wasifu wako kwa 100% hata kama taarifa hizo zipo kwenye CV.
Waajiri wanajua ukicopy barua mtandaoni. Barua inayoanza na “I hereby apply for the job…” haina mvuto.
Fanya Hivi: Anza kwa kuonesha utatuzi wa matatizo. Mfano: “Naomba nafasi hii ili kutumia uzoefu wangu wa miaka 3 kupunguza gharama za uendeshaji…”
Ushauri wa Kitaalamu (Pro Tips)
Hakikisha namba zako za simu na email zinafanya kazi. Watu wengi wanakosa kazi kwa sababu hawapatikani hewani.
Weka picha (Passport size) inayoeleweka kwenye akaunti yako ya Ajira Portal. Epuka picha za “Selfie”.
Kwenye sehemu ya “Referees” (Wadhamini), weka watu ambao unawasiliana nao na wanafahamu utendaji wako, sio tu majina makubwa yasiyokujua.
Unataka CV Yako Iwe “Shortlist Magnet”?
Usihangaike kuandika CV au Barua za maombi kwa kubahatisha. Sisi DeVine Vision Tech tuna utaalamu wa kuandaa CV za kisasa (ATS Friendly) na kuboresha akaunti zako za maombi ya kazi.
Huduma zetu:
- Kuandika na Kuboresha CV.
- Kuandika Cover Letter zenye mvuto.
- Kufanya Marekebisho ya Akaunti ya Ajira Portal.
Tunapatikana Kisesa, Mwanza.
