eRITA: Cheti cha Kuzaliwa Mtandaoni
Mwongozo Kamili wa Jinsi ya Kupata au Kuhakiki Cheti cha Kuzaliwa (Verification) 2026.
Katika ulimwengu wa sasa wa kidijitali, huduma nyingi za serikali nchini Tanzania zimehamia mtandaoni ili kurahisisha upatikanaji. Kama vile ambavyo tumekuwa tukikuelekeza kuhusu NIDA Online hapa DeVine Vision Tech, Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) nao wana mfumo uitwao eRITA.
Mfumo huu unakuwezesha kuomba cheti kipya cha kuzaliwa au kuhakiki cheti cha zamani (Verification) kwa ajili ya mikopo ya elimu ya juu (HESLB), ajira, au matumizi mengine bila kulazimika kupanga foleni ndefu ofisini.
Mahitaji Kabla ya Kuanza
Kabla hujaingia kwenye mfumo, hakikisha una vitu hivi ili usikwame katikati:
- Kifaa: Kompyuta au Simu janja (Smartphone) yenye internet.
- Nakala Laini (Scanned/Picha): Kadi ya Kliniki ya mtoto au Barua ya Serikali ya Mtaa.
- Vithibitisho vya Wazazi: Kitambulisho cha NIDA, Mpiga Kura, au Pasi ya Kusafiria.
- Cheti cha Zamani: (Kama unafanya uhakiki/verification).
- Mawasiliano: Barua pepe (Email) na Namba ya Simu inayofanya kazi.
Hatua kwa Hatua: Jinsi ya Kutumia eRITA
1 Kufungua Akaunti (Sign Up)
Kama ilivyo mifumo mingine, lazima ujisajili kwanza.
- Tembelea tovuti rasmi: erita.rita.go.tz
- Bofya “Tengeneza Akaunti” (Create Account).
- Jaza taarifa zako (Jina, Simu, Email, Mkoa, Wilaya).
- Thibitisha akaunti kupitia link utakayotumiwa kwenye Email.
2 Kuanzisha Maombi
Baada ya kuingia (Login) kwenye akaunti yako:
- Chagua “New Registration” kuomba cheti kipya.
- Chagua “Verification” kuhakiki cheti cha zamani (Muhimu kwa HESLB).
- Bofya “Start Application”.
3 Kujaza Taarifa (Data Entry)
Hapa ndipo umakini unahitajika zaidi. Jaza taarifa za:
- Mtoto/Mwombaji: Tarehe ya kuzaliwa, Mahali, Jinsia.
- Wazazi: Majina kamili kama yalivyo kwenye vitambulisho vyao.
*Zingatia: Hakikisha majina hayana makosa ya herufi. Makosa hapa yatasababisha cheti kukataliwa.
4 Kupakia Viambatanisho
Pakia picha au PDF za Kadi ya Kliniki na Vitambulisho vya wazazi.
- Hakikisha picha ziko wazi (zinasomeka).
- Usipakie faili kubwa sana (zaidi ya 2MB mara nyingi hukataa).
5 Malipo (Control Number)
Mfumo utatoa Control Number. Fanya malipo kupitia:
- Mitandao ya Simu (M-Pesa, Tigo Pesa, Airtel Money).
- Benki (NMB au CRDB).
Tunza ujumbe wako wa malipo kama ushahidi.
6 Kusubiri na Kupakua
Maombi yataenda RITA kuhakikiwa. Ingia mara kwa mara kuangalia.
- Ikisoma “Approved”, pakua (Download) cheti chako na ukiprinti.
- Mfumo kuwa chini: Jaribu tena usiku au asubuhi mapema.
- Kusahau Password: Tumia sehemu ya “Forgot Password” kurudisha nuni yako kwa email.
- Viambatanisho Kukataliwa: Picha zako hazionekani vizuri, rudia kupakia picha safi.
Je, Umekwama au Unahitaji Msaada?
Tunafahamu kuwa si kila mtu ana uzoefu na mifumo hii, na wakati mwingine inachosha au mtandao unasumbua.
Kama unahitaji msaada wa:
- • Kufungua akaunti
- • Kuscan nyaraka
- • Kujaza fomu kwa usahihi
Fika ofisini kwetu DeVine Vision Tech iliyopo Kisesa, Mwanza.
