Usajili wa Cheti cha Kifo (eRITA)
Pata Cheti cha Kifo cha ndugu au jamaa kwa haraka kupitia mfumo wa eRITA bila usumbufu.
Cheti cha Kifo ni nyaraka muhimu ya kisheria inayothibitisha kutokea kwa kifo cha mtu. Hii ni nyaraka ya msingi katika kushughulikia masuala ya mirathi, mafao ya hifadhi ya jamii, bima, na kufunga akaunti za benki za marehemu.
Sasa unaweza kuomba cheti hiki mtandaoni kupitia mfumo wa eRITA.
Vitu Vinavyohitajika (Requirements)
Kabla ya kuanza mchakato mtandaoni, hakikisha una nakala laini (Scanned Copies) za nyaraka zifuatazo. Picha zinapaswa kuwa wazi na zisisomeke vibaya.
- Kibali cha Mazishi (Burial Permit): Hiki hutolewa na Serikali ya Mtaa au Hospitali.
- Taarifa ya Kifo (Notification of Death): Fomu kutoka Hospitali (kama alifia hospitali) au Barua ya Serikali ya Mtaa/Polisi (kama alifia nyumbani au kwa ajali).
- Kitambulisho cha Mwombaji: NIDA, Pasi ya Kusafiria, au Leseni ya Udereva ya mtu anayeomba cheti (lazima awe ndugu wa karibu).
- Taarifa za Marehemu: Jina kamili, Tarehe ya kuzaliwa, Tarehe ya kifo, na Mahali pa kifo.
- Namba ya Simu: Inayofanya kazi kwa ajili ya kupokea ujumbe wa malipo.
Hatua za Kuomba Cheti cha Kifo Mtandaoni
Fuata hatua hizi kwa umakini:
Msaada na Ushauri
Umekwama au Una Haraka?
Mchakato wa kupata nyaraka za vifo unaweza kuwa mgumu na unahitaji umakini mkubwa ili kuepuka makosa yanayoweza kuchelewesha mirathi.
Sisi DeVine Vision Tech tunakusaidia:
- Kufungua akaunti ya eRITA na kujaza fomu kwa usahihi.
- Kuscan na kupakia nyaraka kwa viwango vinavyokubalika.
- Kufuatilia maombi yako mpaka upate cheti.
Ofisi zetu zipo: Kisesa, Mwanza, Tanzania.
