Skip to main content

Jinsi ya Kudownload na Ku-Install Windows 11 | Official Microsoft Guide

Jinsi ya Kudownload na Ku-Install Windows 11 | Direct Link

Mwongozo wa Kudownload & Ku-Install Windows 11

Pakua mfumo wa uendeshaji (OS) wa kisasa zaidi kwenye kompyuta yako bila usumbufu kupitia link ya moja kwa moja.

Windows 11 Interface

Windows 11 ni mfumo wa kisasa kutoka Microsoft. Devine Vision Tech imeweka kiungo cha Windows 11 Pro ISO kupitia Google Drive kwenye kituo chake cha downloads. Kwa toleo la sasa la Windows 11 lililothibitishwa na Microsoft, tumia pia kiungo rasmi cha Microsoft hapo chini. Hakikisha unatumia leseni halali na unathibitisha faili kabla ya ku-install.

Pakua Windows 11 Pro ISO – Devine Vision Tech

Faili: Win.11.Pro.26100.2605.iso (takribani 5 GB). Kiungo hiki kinaelekeza kwenye faili ya Google Drive iliyoorodheshwa na Devine Vision Tech. Google Drive inaweza kuomba uthibitisho kwa faili kubwa.

Pakua Windows 11 Pro – Devine Vision Tech

Fungua ukurasa wa Windows 11 Pro wa Devine Vision Tech


Pakua Windows 11 ISO Rasmi kutoka Microsoft

Kwa ISO rasmi na toleo la sasa, chagua edition na language kwenye ukurasa wa Microsoft.

Download kutoka Microsoft

Mahitaji Kabla ya Ku-Install

  • Flash Drive (USB): Yenye ukubwa wa angalau 8GB (Iwe haina vitu muhimu kwani itafutwa/format).
  • Programu ya Rufus: Hii itatumika kutengeneza “Bootable USB”. Unaweza kuidownload hapa: Index of /downloads.
  • Kompyuta inayokidhi vigezo: Kompyuta iwe na angalau 4GB RAM na uwezo wa kusupport TPM 2.0 na Secure Boot (Ingawa kupitia Rufus unaweza kuruka hivi vigezo).

Hatua za Ku-Install Kwenye Kompyuta

1

Tengeneza Bootable Flash (Kutumia Rufus)

Chomeka Flash yako kwenye kompyuta. Fungua programu ya Rufus, chagua Flash yako, kisha kwenye “Boot selection” bofya ‘SELECT’ na uchague lile faili la Windows 11 ISO ulilodownload hapo juu. Bofya START kuanza mchakato na subiri hadi imalize.

2

Washa Kompyuta Kupitia Flash (Boot from USB)

Chomeka hiyo Flash kwenye kompyuta unayotaka kuweka Windows. Washa kompyuta kisha bonyeza kitufe cha Boot Menu mfululizo (Mara nyingi ni F12, F9, F10, Esc au F2 kulingana na aina ya kompyuta yako kama HP, Dell au Lenovo). Kidirisha kikija, chagua Flash yako (USB Storage Device) na ubonyeze Enter.

3

Anza Mchakato wa Ku-Install

Windows ikishafunguka, chagua lugha yako (English) kisha bonyeza Next, na kisha Install Now. Weka tiki kwenye “I accept the license terms” na ubonyeze Next.

4

Futa Windows ya Zamani (Format C: Drive)

Chagua “Custom: Install Windows only (advanced)”. Utaona orodha ya Partitions za Hard Disk yako. Chagua ile yenye Windows ya zamani (Kawaida ni Drive 0 Partition 2 au inaitwa C:), bofya Format kufuta, kisha ukiwa umeichagua bofya Next. (Onyo: Hakikisha umetoa vitu vyako muhimu kwenye Desktop na Documents kabla ya kufanya hivi!).

5

Subiri Imalize (Kukamilisha Setup)

Sasa kompyuta itaanza kunakili mafile kuingia kwenye Hard Disk. Itajizima na kujiwasha mara kadhaa. Ikimaliza, itakuuliza mambo madogo madogo kama Jina lako na Wi-Fi (Unaweza kuruka sehemu ya Internet ukaweka baadaye). Ukishamaliza, utaona muonekano mpya na mzuri wa Desktop ya Windows 11!

Umekwama au Unahitaji Msaada?

Ku-install Windows kunaweza kuwa kugumu kwa mara ya kwanza na ukikosea unaweza kufuta vitu vyako muhimu. Sisi DeVine Vision Tech tuko tayari kukusaidia au kukufanyia huduma hii kwa gharama nafuu.

© 2026 DeVine Vision Tech | Suluhisho Lako la Mifumo ya Kompyuta.

Scroll to Top
Changia Notes / Document