Pakua Windows 11 Pro ISO 64-bit – Mwongozo wa Installation
Pakua Windows 11 Pro ISO 64-bit na ufuate hatua za kutengeneza bootable USB kwa Rufus na ku-install Windows kwa usalama.
Ukurasa huu unakupa faili ya Windows 11 Pro ISO pamoja na mwongozo rahisi wa kuandaa bootable USB na kuanza installation. Kabla ya ku-install, hakikisha umehifadhi mafaili yako muhimu.
Toleo: Windows 11 Pro
Jina la faili: Win.11.Pro.26100.2605.iso
Ukubwa: takribani 5.0 GB
Tahadhari: Windows 11 inahitaji hardware inayokidhi masharti yake, ikiwemo UEFI, Secure Boot na TPM 2.0 kwenye mifumo inayotumika rasmi.
Kabla ya Ku-install Windows
- Fanya backup ya Documents, Desktop, Pictures na mafaili mengine muhimu.
- Andaa flash disk ya angalau 8 GB. Data iliyopo kwenye flash inaweza kufutwa.
- Pakua Rufus na uitumie kuandika ISO kwenye USB.
- Kwa computer nyingi za kisasa tumia GPT na UEFI. Kwa baadhi ya computer za zamani unaweza kuhitaji MBR na Legacy BIOS.
- Hakikisha unajua edition ya Windows inayolingana na product key au digital license yako.
Jinsi ya Kutengeneza Bootable USB
- Pakua ISO kutoka kwenye button ya juu.
- Pakua na fungua Rufus.
- Weka flash disk, kisha kwenye Device chagua flash sahihi.
- Kwenye Boot selection, chagua Disk or ISO image, kisha bonyeza SELECT.
- Chagua ISO ya Windows 11 Pro.
- Chagua GPT/UEFI kwa computer nyingi za kisasa au MBR/Legacy kwa computer ya zamani inapohitajika.
- Bonyeza START na subiri mpaka Rufus ionyeshe READY.
Jinsi ya Ku-install
- Weka bootable USB kwenye computer.
- Washa computer na fungua Boot Menu kwa F12, F9, F11, Esc au key inayotumiwa na brand yako.
- Chagua USB drive.
- Chagua lugha na keyboard, kisha bonyeza Install now.
- Weka genuine product key ukiwa nayo, au tumia digital license inayolingana na edition yako.
- Kwa clean install, chagua Custom: Install Windows only.
- Chagua partition kwa uangalifu. Kufuta au ku-format partition kunaweza kufuta data.
- Baada ya installation, connect internet, fanya Windows Update na install drivers.
Activation: Tumia genuine product key au digital license. Post hii haitoi activators za kubypass Windows licensing.
Pakua Rufus
Rufus 4.15 official Standard x64: