Uhakiki wa Cheti cha Kuzaliwa (Verification)
Badilisha cheti chako cha zamani kiwe cha kidijitali kwa ajili ya Mikopo ya Elimu ya Juu, Pasipoti na Ajira.
Je, unamiliki cheti cha kuzaliwa cha zamani (kilichoandikwa kwa mkono) na unataka kukitumia kwa ajili ya maombi ya Bodi ya Mikopo (HESLB), Pasipoti, au NIDA?
Lazima ufanye Uhakiki (Verification) kupitia mfumo wa eRITA ili taarifa zako ziingizwe kwenye kanzidata ya taifa na utambuliwe kidijitali.
Kimeandikwa kwa mkono, hakipo mtandaoni, hakiwezi kusomwa na mifumo ya HESLB au Uhamiaji moja kwa moja.
Kimechapishwa kwa kompyuta, kinaonekana mtandaoni (Online Verified), kinakubalika popote duniani.
Mahitaji ya Kubadilisha/Kuhakiki
- Cheti cha Zamani: Nakala halisi (Original) au Copy yake.
- Vitambulisho vya Wazazi: NIDA, Mpiga Kura au Pasipoti (Mmoja au wote wawili).
- Vyeti vya Shule: Cheti cha kumaliza shule ya Msingi au Sekondari (Kama unacho, kinasaidia kuhakiki majina).
- Picha ya Pasipoti: Softcopy ya picha yako ya hivi karibuni (Passport size).
Hatua za Kufanya Mtandaoni
Fuata hatua hizi ili kuhakiki cheti chako:
Msaada na Ushauri
Je, Mtandao Unasumbua au Huna Uhakika?
Kukosea kujaza fomu za RITA kunaweza kukugharimu muda na pesa. Sisi DeVine Vision Tech tunakusaidia mchakato mzima kwa usahihi na haraka.
Tunakusaidia:
- Kufungua akaunti na kujaza fomu za uhakiki.
- Kubadili picha na nyaraka ziwe na ukubwa sahihi.
- Kufuatilia hadi upate uhakiki wako.
Ofisi zetu zipo: Kisesa, Mwanza, Tanzania.
