Skip to main content

Tenzi za Rohoni

Tenzi za Rohoni

Tenzi za Rohoni 45 – Mtazame Huyo! Aliyeangikwa juu

Tenzi za Rohoni 45 – Mtazame Huyo! Aliyeangikwa juu Tenzi Na. 45 Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 45, “Mtazame Huyo! Aliyeangikwa juu”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza. Maneno ya Wimbo Mtazame Huyo! Aliyeangikwa juu Hivi sasa upate ishi. Mwenye – dhambi dhaifu, mtazame tu Wala usifanye tashwishi. Tazama! Tazama! Tazama uishi! Mtazame huyo aliyeangikwa juu Hivi sasa upate ishi. Kama mwana kondoo hakuondoa dhambi, Na makosa yako maovu! Kama deni zetu zote hakulipa Mbona imemwagika damu? Si kutubu na sala ikomboayo, Ila damu ndiyo salama; Na aliyeimwaga aweza, sasa, Dhambi zako kukufutia. Usiwe na shaka, Mungu amesema, Hakuna alilolisaza; Hapo alipokuja alitimiza Kazi zote alizoanza. Basi twae uzima, kwa kufurahi Upokee kwa Bwana, sasa; Ujijue hakika kwake kuishi Yesu aishiye kabisa. ← Tenzi 44 | Tenzi Zote | Tenzi 46 → Tazama Tenzi za Rohoni 1–164 Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

Tenzi za Rohoni

Tenzi za Rohoni 44 – Kukawa Na Giza Dunia Yote

Tenzi za Rohoni 44 – Kukawa Na Giza Dunia Yote Tenzi Na. 44 Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 44, “Kukawa Na Giza Dunia Yote”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza. Maneno ya Wimbo Kukawa na giza dunia yote, Ni Mwanga wa ulimwengu, Ikaisha ulipokuja yote, Ni mwanga wa ulimwengu. Jua, Yesu hana mwenziwe! Nalipofuka kama wewe: Nakuombea umwone nawe, Ni mwanga wa ulimwengu. Hatuna giza tudumuo mwake, Ni mwanga wa ulimwengu; Tumwandamiapo nyayoni mwake Ni mwanga wa ulimwengu. Enyi wa gizani wenye kutanga! Ni mwanga wa ulimwengu, Kaulekeeni, mpate lenga; Ni mwanga wa ulimwengu. Tutamwona Mwokozi juu ya mbingu Ni mwanga wa ulimwengu: Ni nuru za mbingu kondoo wa Mungu Ni mwanga wa ulimwengu. ← Tenzi 43 | Tenzi Zote | Tenzi 45 → Tazama Tenzi za Rohoni 1–164 Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

Tenzi za Rohoni

Tenzi za Rohoni 43 – Yesu Akwita

Tenzi za Rohoni 43 – Yesu Akwita Tenzi Na. 43 Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 43, “Yesu Akwita”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza. Maneno ya Wimbo Yesu akwita, chanena Chuo: Uje leo, uje leo; Kwani kusita? Akwita, Njoo; Unatanga upeo. Hwita leo, hwita leo. Yesu akwita kwa upole akwita leo. Waliochoka, wapumzike, Hwita leo, hwita leo: Wenye mizigo, wakamtweke, wapate mapumuo. Anakungoja, uliye yote, Uje leo, uje leo; Uliyekosa usijifiche: Woshwe, uvikwe nguo. Yesu asihi wakawiao, Waje leo, waje leo. Watafurahi waaminio; Usije kwani? Njoo. ← Tenzi 42 | Tenzi Zote | Tenzi 44 → Tazama Tenzi za Rohoni 1–164 Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

Tenzi za Rohoni

Tenzi za Rohoni 42 – Kivulini Mwa Yesu

Tenzi za Rohoni 42 – Kivulini Mwa Yesu Tenzi Na. 42 Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 42, “Kivulini Mwa Yesu”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza. Maneno ya Wimbo Kivulini mwa Yesu kuna Kituo: Kituo mbali na hamu, kituo kilicho tamu. Kivulini mwa Yesu kuna kituo; kivulini mwa Yesu kuna kituo; Raha tu, mle; amani tupu, Furaha tele; kivulini mwa Yesu Raha tu, mle; amani tupu, Furaha tele; kivulini mwa Yesu. Kivulini mwa Yesu nina amani Iliyopita fahamu, tena itakayodumu. Kivulini mwa Yesu, nina furaha; Furaha yenye fahari, ya kueneza habari. ← Tenzi 41 | Tenzi Zote | Tenzi 43 → Tazama Tenzi za Rohoni 1–164 Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

Tenzi za Rohoni

Tenzi za Rohoni 41 – Yesu Aliniita

Tenzi za Rohoni 41 – Yesu Aliniita Tenzi Na. 41 Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 41, “Yesu Aliniita”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza. Maneno ya Wimbo Yesu aliniita, “njoo, Raha iko kwangu, Kichwa chako ukilaze Kifuani mwangu.” Nilikwenda kwake mara, Sana nilichoka; Nikapata kwake raha, Na furaha tena. Yesu aliniita, “njoo, Kwangu kuna maji, Maji ya uzima, bure, Unywe uwe hai, “ Nilikwenda kwake mara Na maji nikanywa: Naishi kwake, na kiu Kamwe sina tena. Yesu aliniita, “njoo, Dunia ni giza, Ukinitazama nuru Takung’arizia.” Nilikwenda kwake mara Yeye jua langu, Ni kila wakati mwanga Safarini mwangu. ← Tenzi 40 | Tenzi Zote | Tenzi 42 → Tazama Tenzi za Rohoni 1–164 Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

Tenzi za Rohoni

Tenzi za Rohoni 40 – Nasikia Kwitwa

Tenzi za Rohoni 40 – Nasikia Kwitwa Tenzi Na. 40 Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 40, “Nasikia Kwitwa”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza. Maneno ya Wimbo Nasikia kwitwa Na sauti yako Nikasafiwe kwa damu Ya kwangikwa kwako. Nimesogea Mtini pako, Unisafi kwa damu ya kwangikwa kwako. Ni mnuonge kweli, Umenipa nguvu, Ulivyonisafi taka, Ni utimilivu. Yesu hunijuvya; Mapenzi, imani; Tumai, amani, radhi, Hapa na Mbinguni. Huipa imara, Kazi yake, ndani: Huongezeka neema, Ashindwe Shetani. Huishuhudia, Myoyo ya imani Ya kuzipata ahadi, Wakimuamini. Napata wokovu, Wema na neema; kwako Bwana nina nguvu Na haki daima. ← Tenzi 39 | Tenzi Zote | Tenzi 41 → Tazama Tenzi za Rohoni 1–164 Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

Tenzi za Rohoni

Tenzi za Rohoni 39 – Mwenye Dhambi Huna Raha

Tenzi za Rohoni 39 – Mwenye Dhambi Huna Raha Tenzi Na. 39 Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 39, “Mwenye Dhambi Huna Raha”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza. Maneno ya Wimbo Mwenye dhambi huna raha, Sikiza nakusihi, Utapata msamaha Kwake Yesu Mwokozi! Njoo hima, njoo hima, Naye atafurahi. Yesu anakwita sana Naye yuko Mbinguni; Hofu ya kifo hapana Kwake ukiamini. Njoo hima, njoo hima, Utapata amani. Hatakwita siku zote; Ni ya sasa nafasi. Lete na uchafu wote, Kukawa haipasi. Njoo hima, njoo hima, Ni wokovu halisi. Uzima uko kwa Bwana Twae uzima hasa Bure unapatikana, Wokovu twae sasa! Njoo hima, njoo hima, Twae utakatifu. ← Tenzi 38 | Tenzi Zote | Tenzi 40 → Tazama Tenzi za Rohoni 1–164 Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

Tenzi za Rohoni

Tenzi za Rohoni 38 – Twende Kwa Yesu

Tenzi za Rohoni 38 – Twende Kwa Yesu Tenzi Na. 38 Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 38, “Twende Kwa Yesu”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza. Maneno ya Wimbo Twende kwa Yesu mimi nawe, Njia atwonya tuijue Imo Chuoni; na Mwenyewe, Hapa asema, Njoo! Na furaha tutaiona, Mioyo ikitakata sana, Kwako, Mwokozi, kuonana, Na milele kukaa. “Wana na waje”, atwambia, Furahini mkisikia, Ndiye mfalme wetu pia, Na tumtii, Njoo. Wangojeani? Leo yupo; Sikiza sana asemapo; Huruma zake zikiwapo, Ewe kijana, Njoo. ← Tenzi 37 | Tenzi Zote | Tenzi 39 → Tazama Tenzi za Rohoni 1–164 Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

Tenzi za Rohoni

Tenzi za Rohoni 37 – Waitwa, Mwovu, na Bwana

Tenzi za Rohoni 37 – Waitwa, Mwovu, na Bwana Tenzi Na. 37 Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 37, “Waitwa, Mwovu, na Bwana”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza. Maneno ya Wimbo Waitwa, mwovu, na Bwana Umwendee hima sana, Usafiwe dhambi zako, Humwoni ni mwema kwako? Unaitwa! Itika tu! Umwendee Bwana Yesu! Sifiche makosa yako, Uungame dhambi zako! Kristo tu umuamini, Ndiyo njia ua Mbinguni. Alilipa damu yake Ili kukukweza kwake; Alikufa yeye Bwana, Mimi nawe tuwe wema. Ukifanywa kuwa mwema Mwishoni utasimama, Utaingia rahani Na wapenzi wa zamani. Ni mwanga tu, nchi ile; Uovu hauko kule, Kwamba wataka ufike Sharti huku uosheke. ← Tenzi 36 | Tenzi Zote | Tenzi 38 → Tazama Tenzi za Rohoni 1–164 Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

Tenzi za Rohoni

Tenzi za Rohoni 36 – Anisikiaye, Aliye Yote

Tenzi za Rohoni 36 – Anisikiaye, Aliye Yote Tenzi Na. 36 Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 36, “Anisikiaye, Aliye Yote”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza. Maneno ya Wimbo Anisikiaye, aliye yote; Sasa litangae, wajue wote, Duniani kote neno wapate, Atakaye na aje! Ni “Atakaye”, ni “atakaye”, Pwani hata bara, na litangae; Ni Baba Mpenzi alinganaye Atakaye na aje. Anijiliaye, Yesu asema, Asikawe, aje hima mapema; Ndimi njia, kweli, ndimi uzima; Atakaye na aje! Atakaye aje, ndivyo ahadi; Atakaye hiyo, haitarudi! Atakaye lake, ni la abadi! Atakaye na aje. ← Tenzi 35 | Tenzi Zote | Tenzi 37 → Tazama Tenzi za Rohoni 1–164 Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

banner
Scroll to Top