Skip to main content

Tenzi za Rohoni

Tenzi za Rohoni

Tenzi za Rohoni 65 – Safari

Tenzi za Rohoni 65 – Safari Tenzi Na. 65 Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 65, “Safari”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza. Maneno ya Wimbo Katika safari yetu Kwenda Mbinguni Tusiishe siku zetu Usingizini. Ng’oani! Tujifungeni, Twende zetu juu! Kristo ndiye kiongozi; Tusihofu tu. Atwekwe badala yetu, Mwenyewe Bwana; Yesu kiongozi wetu Atapokea. Kisimani, maji tele, Maji mazima! Maji hayo, Ya milele Yana neema. Njiani miiba mingi, Yatuumiza; Hofu na hatari nyingi, Sana zakaza. Kweli, njia ya Mbinguni Ni ya mashaka; Tuwe na Yesu njiani, Mara hufika. ← Tenzi 64 | Tenzi Zote | Tenzi 66 → Tazama Tenzi za Rohoni 1–164 Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

Tenzi za Rohoni

Tenzi za Rohoni 64 – Ujaribiwapo, Sifanye Dhambi

Tenzi za Rohoni 64 – Ujaribiwapo, Sifanye Dhambi Tenzi Na. 64 Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 64, “Ujaribiwapo, Sifanye Dhambi”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza. Maneno ya Wimbo Ujaribiwapo, sifanye dhambi, Bali uzishinde, kwa Yesu kutii. Fuliza kiume ushinde tamaa; Yesu ni Mwokozi, hukuokoa. Umwombapo yu papo Akuongeze nguvu, Atakusaidia; Yesu atakufaa. Wepushe waovu, matusi dharau; Heshima la Mungu, kamwe sisahau; Fanya uhodari, uwe mpole, Atakuokoa hata milele. Avumiliaye hupewa taji; Tujaposumbuka tu washindaji, Na mwokozi wetu hutuwezesha Tusiwe kushindwa kama twakesha. ← Tenzi 63 | Tenzi Zote | Tenzi 65 → Tazama Tenzi za Rohoni 1–164 Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

Tenzi za Rohoni

Tenzi za Rohoni 63 – Ndugu wa kirohoni

Tenzi za Rohoni 63 – Ndugu wa kirohoni Tenzi Na. 63 Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 63, “Ndugu wa kirohoni”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza. Maneno ya Wimbo Ndugu wa kirohoni Mliokombolewa, Tafakarini sana Yatupasayo. Wapenzi wake Yesu Tuliokombolewa Tujitoe kabisa Wengi waponywe. Siku itatimia Tutakapoulizwa Wale wa nyumba zetu Na majirani Tujitoeni, ndugu, Tukahubiri Injili. Atutumie Roho kuponya wengi. Wasiokombolewa Ni wengi vijijini, Wataokolewaje Tukiogopa? Bwana alijitoa Akapotewa mengi, Ili atuokoe, Tusiwe waoga. Aliyetununua, Kwa kuimwaga damu, Angalieni sana Msimwepuke. ← Tenzi 62 | Tenzi Zote | Tenzi 64 → Tazama Tenzi za Rohoni 1–164 Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

Tenzi za Rohoni

Tenzi za Rohoni 62 – Bwana Wa Mabwana

Tenzi za Rohoni 62 – Bwana Wa Mabwana Tenzi Na. 62 Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 62, “Bwana Wa Mabwana”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza. Maneno ya Wimbo Bwana wa mabwana, Mwenye nguvu sana Twakusihi: Neno la milele Na liende mbele, Waongoke tele Kwa Mwokozi. Tunaowaona Wanavyopatana, Kulipinga, Hawataliweza Neno, kulitweza: Huwaje! Kucheza: Na upanga? Heri wajitunze Ili wapatane, Na Mwokozi; Watafute sana, Wapate kuona, Yesu kuwa Bwana, Mkombozi. Mungu awaita Wasije kukuta Pigo lake; Hakuona vyema Wakose uzima, Awape rehema, Waokoke. Mwenye utukufu Tunamshukuru Yeye pweke! Nasifiwe sana, Baba, naye Mwana, Na wa tatu tena Roho yake. ← Tenzi 61 | Tenzi Zote | Tenzi 63 → Tazama Tenzi za Rohoni 1–164 Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

Tenzi za Rohoni

Tenzi za Rohoni 61 – Tumesikia Mbiu

Tenzi za Rohoni 61 – Tumesikia Mbiu Tenzi Na. 61 Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 61, “Tumesikia Mbiu”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza. Maneno ya Wimbo Tumesikia mbiu: Yesu lo! aponya, Utangazeni kote, Yesu, lo! aponya. Tiini amri hiyo; Nchini na baharini, Enezeni mbiu hii; Yesu , lo! aponya. Imbeni na vitani; Yesu, lo! aponya; Kwa nguvu ya kombozi, Yesu, lo! aponya. Imbeni wenye shida, Unapoumwa moyo. Na karibuni imba; Yesu, lo! aponya. Mawimbini uenee; Yesu, lo! Aponya; Wenye dhambi jueni; Yesu, lo! Aponya. Visiwa na viimbe, Vilindi itikeni, Na nchi shangilieni; Yesu, lo! Aponya. Upepo utangaze; Yesu, lo! Aponya; Mataifa yashangaaa; Yesu lo! Aponya. Milimani, bondeni, Sauti isikike Ya wimbo wa ushindi; Yesu, lo! Aponya. ← Tenzi 60 | Tenzi Zote | Tenzi 62 → Tazama Tenzi za Rohoni 1–164 Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

Tenzi za Rohoni

Tenzi za Rohoni 60 – Waponyeni Watu

Tenzi za Rohoni 60 – Waponyeni Watu Tenzi Na. 60 Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 60, “Waponyeni Watu”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza. Maneno ya Wimbo Waponyeni watu wamo kifoni, Watoeni walio shimoni; Na aangukaye mumzuie; Ya Bwana Yesu wahubirini. Walio kifoni waokoeni, Mwokozi yuko, wahubirini. Wajapokawia anangojea, Awasubiri waje tobani; Msiwadharau, muwaonyeni; Huwasamehe; wakiamini. Myoyoni mwa ndani, yule shetani Ameyaseta mawazo yao; Lakini kwa Bwana huwa mazima, Tukiwavuta kwa pole hao. Kawaokoeni, wale njiani, Mutimize mapenzi ya Bwana; Na kwa nguvu zake warudi kwake, Kwa subira waonyeni sana. ← Tenzi 59 | Tenzi Zote | Tenzi 61 → Tazama Tenzi za Rohoni 1–164 Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

Tenzi za Rohoni

Tenzi za Rohoni 59 – Peleleza Ndani Yangu

Tenzi za Rohoni 59 – Peleleza Ndani Yangu Tenzi Na. 59 Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 59, “Peleleza Ndani Yangu”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza. Maneno ya Wimbo Peleleza ndani yangu, Iwe safi nia, Kwangu kama kwako Mungu, Idhihiri pia. Peleleza moyo wangu Uunifunulie, Yaliyomo ndani yangu Nami niyajue. Kwanza washe zako tambi, Kumefunga giza; Nijue ambavyo dhambi Ni la kuchukiza. Peleleza na mawazo Ni mbegu za mambo, Asili ya machukizo, Maumbuo – umbo. Zidi kuyapeleleza Katikati yangu Hata wishe nifundisha Udhaifu wangu. Hapo nikikwinamia Mbele zako, Mungu, Hakika nitakujua U mpenzi wangu. ← Tenzi 58 | Tenzi Zote | Tenzi 60 → Tazama Tenzi za Rohoni 1–164 Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

Tenzi za Rohoni

Tenzi za Rohoni 58 – Mwamba Wenye Imara

Tenzi za Rohoni 58 – Mwamba Wenye Imara Tenzi Na. 58 Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 58, “Mwamba Wenye Imara”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza. Maneno ya Wimbo Mwamba wenye imara Kwako nitajificha! Maji hayo na damu Yaliyotoka humu, Hunisafi na dhambi, Hunifanya mshindi. Kwa kazi zote pia , Sitimizi sharia. Nijapofanya bidii, Nikilia nakudhii, Hayaishi makosa; Ndiwe wa kuokoa. Sina cha mkononi, Naja Msalabani; Nili tupu, nivike; Ni mnyonge, nishike; Nili mchafu naja, Nioshe nisijafa. Nikungojapo chini, Nakwenda kaburini; Nipaapo Mbinguni, Na kukwona enzini: Roho yangu na iwe Rahani mwako wewe. ← Tenzi 57 | Tenzi Zote | Tenzi 59 → Tazama Tenzi za Rohoni 1–164 Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

Tenzi za Rohoni

Tenzi za Rohoni 57 – Naendea Msalaba

Tenzi za Rohoni 57 – Naendea Msalaba Tenzi Na. 57 Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 57, “Naendea Msalaba”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza. Maneno ya Wimbo Naendea Msalaba, Ni mnyonge na mpofu, Yapitayo naacha, Nipone Msalabani. Nakutumaini tu, Ewe Mwana wa Mungu; Nainamia kwako; Niponye, mponya wangu. Nakulilia sana: Nalemewa na dhambi; Pole Yesu asema; “Nitazifuta zote”. Natoa vyote kwako, Nafasi nazo nguvu, Roho yangu na mwili, Viwe vyako milele. Kwa damu yake sasa, Nimegeuka roho, Nikaziacha tama Nimfuate Yesu tu. Yesu yuaja tena! Nimepevuka kwake, Kila chembe kamili; Msifuni yeye mponya! ← Tenzi 56 | Tenzi Zote | Tenzi 58 → Tazama Tenzi za Rohoni 1–164 Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

Tenzi za Rohoni

Tenzi za Rohoni 56 – Ni siku kuu siku ile

Tenzi za Rohoni 56 – Ni siku kuu siku ile Tenzi Na. 56 Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 56, “Ni siku kuu siku ile”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza. Maneno ya Wimbo Ni siku kuu siku ile Ya kumkiri Mwokozi! Moyo umejaa tele, Kunyamaza hauwezi. Siku kuu! Siku kuu! Ya kuoshwa dambi zangu kuu! Hukesha na kuomba tu, Ananiongoza miguu. Siku kuu! siku kuu! Ya kuoshwa dhambi zangu kuu. Tumekwisha kupatana Mimi wake, yeye wangu, Na sasa nitamwandama, Nikiri neno la Mungu. Moyo tulia kwa Bwana Kiini cha raha yako, Huna njia mbili tena; Yesu ndiye njia yako. Nadhiri yangu ya mbele Nitaiweka daima, Hata ije siku ile, Ya kwonana kwa salama ← Tenzi 55 | Tenzi Zote | Tenzi 57 → Tazama Tenzi za Rohoni 1–164 Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

banner
Scroll to Top