Tenzi za Rohoni 75 – Waimba, Sikizeni
Tenzi za Rohoni 75 – Waimba, Sikizeni Tenzi Na. 75 Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 75, “Waimba, Sikizeni”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza. Maneno ya Wimbo Waimba, sikizeni, Malaika Mbinguni; Wimbo wa tamu sana Wa pendo zake Bwana, “Duniani salama, Kwa wakosa rehema.” Sisi sote na twimbe Nao wale wajumbe; Waimba, sikizeni, Malaika mbinguni. Ndiye Bwana wa Mbingu, Tangu milele Mungu, Amezaliwa mwili, Mwana wa mwanamwali; Ametoka enzini Kuja ulimwenguni Mwokozi atufie, Ili tusipotee. Waimba, sikizeni, Malaika Mbinguni. Mtukufu wa amani Ametoka Mbinguni, Jua la haki, ndiye Atumulikiaye; Amejivua enzi, Alivyo na mapenzi, Ataka kutuponya, Kutuzalisha upya, Waimba sikizeni, Malaika Mbinguni. Njoo upesi, Bwana, Twakutamani sana; Kaa nasi, mwokozi Vita hatuviwezi; Vunja kichwa cha nyoka, Sura zako andika, Tufanane na wewe, Kwetu sifa upewe, Waimba, sikizeni, Malaika Mbinguni. ← Tenzi 74 | Tenzi Zote | Tenzi 76 → Tazama Tenzi za Rohoni 1–164 Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android