Skip to main content

Pakua Rufus 4.15 – Tengeneza Windows Bootable USB

Pakua Rufus 4.15 – Tengeneza Windows Bootable USB

Pakua Rufus 4.15 official na ujifunze kutengeneza bootable USB kwa Windows 11, Windows 10 na Windows 7.

Rufus ni programu ndogo ya Windows inayotumika kuandika ISO kwenye USB ili USB iweze ku-boot. Toleo hili ni Rufus 4.15 Standard x64 kutoka official Rufus GitHub release.

Toleo: Rufus 4.15 Standard x64

Jina la faili: rufus-4.15.exe

Ukubwa: takribani 1.9 MB

Pakua Rufus 4.15 Direct

Tahadhari: Rufus hu-format USB wakati wa kutengeneza bootable media. Hamisha mafaili yote muhimu kutoka kwenye flash kabla ya kubonyeza START.

Rufus Inafanya Kazi Gani?

Rufus hutengeneza USB inayoweza ku-boot kutoka kwenye ISO. Unaweza kuitumia kuandaa installation media ya Windows 11, Windows 10, Windows 7 na mifumo mingine inayotumia bootable ISO.

Jinsi ya Kutumia Rufus

  1. Pakua Rufus kupitia button ya juu.
  2. Weka flash disk ya angalau 8 GB.
  3. Fungua Rufus na uchague flash sahihi kwenye Device.
  4. Kwenye Boot selection chagua Disk or ISO image.
  5. Bonyeza SELECT na uchague Windows ISO.
  6. Kwa computer nyingi za kisasa, tumia GPT na UEFI. Kwa baadhi ya computer za zamani tumia MBR na Legacy BIOS.
  7. Bonyeza START. Rufus itafuta yaliyomo kwenye USB na kuandika installation files.
  8. Subiri mpaka status iwe READY ndipo uondoe USB.

Pakua Windows ISO

Scroll to Top