Mwongozo wa Kudownload & Ku-Install Windows 11
Pakua mfumo wa uendeshaji (OS) wa kisasa zaidi kwenye kompyuta yako bila usumbufu kupitia link ya moja kwa moja.
Windows 11 ni toleo jipya na la kisasa kutoka Microsoft linalokuja na muonekano mzuri sana, usalama ulioboreshwa, na uwezo wa kuendesha programu (Apps) za Android. Wakati mwingine kupakua kutoka kwenye tovuti ya Microsoft inaweza kuwa usumbufu kutokana na masharti mengi. Hapa tumekuwekea Direct Link ya kupakua faili la ISO kwa urahisi kabisa.
Pakua Faili la Windows 11 (ISO Image)
Faili hili lina ukubwa wa takriban 5GB+. Hakikisha una bando la kutosha na mtandao wenye kasi (Wi-Fi inashauriwa).
Download Windows 11 ISOMahitaji Kabla ya Ku-Install
- Flash Drive (USB): Yenye ukubwa wa angalau 8GB (Iwe haina vitu muhimu kwani itafutwa/format).
- Programu ya Rufus: Hii itatumika kutengeneza “Bootable USB”. Unaweza kuidownload hapa: Index of /downloads.
- Kompyuta inayokidhi vigezo: Kompyuta iwe na angalau 4GB RAM na uwezo wa kusupport TPM 2.0 na Secure Boot (Ingawa kupitia Rufus unaweza kuruka hivi vigezo).
Hatua za Ku-Install Kwenye Kompyuta
Tengeneza Bootable Flash (Kutumia Rufus)
Chomeka Flash yako kwenye kompyuta. Fungua programu ya Rufus, chagua Flash yako, kisha kwenye “Boot selection” bofya ‘SELECT’ na uchague lile faili la Windows 11 ISO ulilodownload hapo juu. Bofya START kuanza mchakato na subiri hadi imalize.
Washa Kompyuta Kupitia Flash (Boot from USB)
Chomeka hiyo Flash kwenye kompyuta unayotaka kuweka Windows. Washa kompyuta kisha bonyeza kitufe cha Boot Menu mfululizo (Mara nyingi ni F12, F9, F10, Esc au F2 kulingana na aina ya kompyuta yako kama HP, Dell au Lenovo). Kidirisha kikija, chagua Flash yako (USB Storage Device) na ubonyeze Enter.
Anza Mchakato wa Ku-Install
Windows ikishafunguka, chagua lugha yako (English) kisha bonyeza Next, na kisha Install Now. Weka tiki kwenye “I accept the license terms” na ubonyeze Next.
Futa Windows ya Zamani (Format C: Drive)
Chagua “Custom: Install Windows only (advanced)”. Utaona orodha ya Partitions za Hard Disk yako. Chagua ile yenye Windows ya zamani (Kawaida ni Drive 0 Partition 2 au inaitwa C:), bofya Format kufuta, kisha ukiwa umeichagua bofya Next. (Onyo: Hakikisha umetoa vitu vyako muhimu kwenye Desktop na Documents kabla ya kufanya hivi!).
Subiri Imalize (Kukamilisha Setup)
Sasa kompyuta itaanza kunakili mafile kuingia kwenye Hard Disk. Itajizima na kujiwasha mara kadhaa. Ikimaliza, itakuuliza mambo madogo madogo kama Jina lako na Wi-Fi (Unaweza kuruka sehemu ya Internet ukaweka baadaye). Ukishamaliza, utaona muonekano mpya na mzuri wa Desktop ya Windows 11!
Umekwama au Unahitaji Msaada?
Ku-install Windows kunaweza kuwa kugumu kwa mara ya kwanza na ukikosea unaweza kufuta vitu vyako muhimu. Sisi DeVine Vision Tech tuko tayari kukusaidia au kukufanyia huduma hii kwa gharama nafuu.
