Siri za Kufuzu Ajira Portal: Kutoka Maombi Hadi Interview
Ongezeko kubwa la wahitimu limesababisha soko la ajira kuwa gumu. Fahamu hatua sahihi za kufuata, uandishi wa CV inayoaminika, na mambo 10 ya kuzingatia wakati wa kuomba kazi serikalini.
Tumia mfumo wa kielektroniki wa Recruitment Portal kuomba ajira za kudumu serikalini.
UTANGULIZI: Hali ya Soko la Ajira Tanzania
Serikali ya Tanzania imekuwa ikitangaza nafasi za ajira kwenye vitengo mbalimbali baada ya vipindi vya uhakiki. Ongezeko la wahitimu kuanzia ngazi ya cheti hadi shahada limesababisha ushindani kuwa mkubwa sana. Wahitimu wengi hawafuzu si kwa sababu hawana sifa, bali kwa kukosa ujuzi wa kutumia mfumo wa Recruitment Portal kwa usahihi.
Mambo 10 ya Kuzingatia Wakati wa Kufanya Maombi ya Kazi
Vyeti Halisi Pekee
Muombaji anapaswa kuwa na vyeti vinavyohitajika. Result Slips, Transcripts na Affidavits hazikubaliki kwenye mfumo huu kama mbadala wa cheti halisi.
Baruapepe (Email) Binafsi
Lazima uwe na email yako mwenyewe. Hakikisha umehifadhi neno la siri (password) sehemu salama kwani mawasiliano yote yatapita huko.
Nakala za Vyeti
Andaa nakala (copy) za vyeti vyote: Shahada, kidato cha nne (CSEE), kidato cha sita (ACSEE), na cheti cha kuzaliwa.
Picha (Passport Size)
Piga picha ya hivi karibuni (Passport size) na uihifadhi katika mfumo wa ‘soft copy’ kwenye flash au simu.
Uhakiki wa Mwanasheria
Peleka nakala za vyeti kwa wakili au mahakamani kwa ajili ya Certified True Copy (kugongwa muhuri wa uhalali).
Scanning kwa PDF
Scan vyeti vilivyogongwa muhuri na uvihifadhi katika mfumo wa PDF. Kila faili lipe jina linaloeleweka (mfano: “Form Four Certificate.pdf”).
Mpangilio wa Mafaili
Hifadhi mafaili yote (PDFs na picha) kwenye folder moja ili kurahisisha kazi ya kupandisha (uploading) kwenye mfumo.
Usajili wa ‘Recruitment Portal’
Ingia portal.ajira.go.tz. Jisajili kama mwanachama mpya na uanze kuingiza taarifa zako binafsi na taaluma.
Kamilisha Profile kwa 90%
Hakikisha umeingiza kila cheti sehemu husika. Profile yako lazima ionyeshe angalau 90% ili uweze kuomba kazi.
Barua ya Maombi
Andika barua ya maombi kulingana na nafasi husika, i-scan na uipakie (upload) kwenye tangazo husika.
Nyaraka Muhimu Unapokuja Kwenye Usaili
- Cheti halisi cha kuzaliwa.
- Kitambulisho cha Taifa (NIDA), Mpiga kura, au Hati ya kusafiria.
- Vyeti halisi vya kitaaluma (Academic Certificates).
- Hati ya kiapo endapo majina yanatofautiana kwenye nyaraka.
- Vyeti vya waliosoma nje lazima vihakikiwe na TCU, NACTE au NECTA.
Maandalizi ya CV Safi Inayoaminika
Wasifu binafsi (CV) ni kioo chako kwa mwajiri. Ili CV yako ipite kwenye mchujio wa awali, zingatia yafuatayo:
- Juu Kabisa: Taja majina yako yote rasmi kwa herufi kubwa kama yalivyo kwenye vyeti.
- Maelezo Mafupi (Profile): Taja matarajio yako na nini taasisi itegemee kutoka kwako.
- Historia ya Elimu: Anza na kiwango cha juu cha elimu ulichonacho kuelekea cha chini (mfano: Masters -> Degree -> Diploma -> A-level -> O-level).
- Uzoefu wa Kazi: Anza na kazi ya sasa kuelekea ulikoanzia. Taja mwajiri, muda, na majukumu yako.
- Wadhamini (Referees): Taja angalau wadhamini watatu wa kuaminika wenye anwani kamili, simu, na barua pepe.
- Kiapo na Saini: Thibitisha kuwa taarifa ulizotoa ni za kweli kwa kuweka saini na tarehe.
Uandishi wa Barua ya Maombi ya Kazi
| Kipengele | Maelezo ya Kuzingatia |
|---|---|
| Anuani ya Mwombaji | Sanduku la posta, mkoa, tarehe, simu na barua pepe. |
| Anuani ya Mwajiri | Elekeza barua kwa Katibu wa Sekretarieti ya Ajira au Mwajiri husika (K.k). |
| Kichwa cha Habari | Taja wazi nafasi unayoomba na jina la taasisi iliyotangaza. |
| Madhumuni | Elezea elimu yako, umri, uzoefu wako kwa ufupi na kwanini unaitaka hiyo kazi. |
| Hitimisho | Saini yako na jina lako kamili ni lazima. |
Masharti ya Jumla ya PSRS (UTUMISHI)
- Uraia: Mwombaji lazima awe Raia wa Tanzania.
- Umri: Kikomo cha umri wa kuajiriwa kwa masharti ya kudumu ni miaka 45.
- Vyeti vya Kughushi: Ni marufuku kuwasilisha taarifa za uongo. Hatua kali za kisheria zitachukuliwa.
- Uwasilishaji: Barua hazipokelewi kwa mkono (hard copy). Maombi yote ni kwa njia ya mtandao kupitia Ajira Portal.
Jiunge na Group Letu la WhatsApp!
Je, unakwama kwenye mfumo wa Ajira Portal? Unahitaji msaada wa kuandaa CV au barua ya maombi? Bonyeza kifungo hapa chini kujiunga na group letu la kusaidiana kujiandaa na usaili na kupata taarifa za kazi kila siku.
Tuna namba za msaada: 0735-398259 (Kiufundi) na 0736-005511 (Malalamiko).
