Mwongozo Kamili wa Kufuzu Ajira Portal kwa Watu Wote
Soma mwongozo wa kina zaidi nchini Tanzania unaoelezea hatua kwa hatua jinsi ya kujiandikisha, kujaza taarifa zako, na mbinu za ushindi kwenye usaili wa serikali.
Mfumo wa ‘Recruitment Portal’ ndio njia pekee ya ushindani wa haki katika Utumishi wa Umma.
UTANGULIZI: Kwa Nini Usajili Sahihi ni Muhimu?
Serikali ya awamu ya tano sasa imeanza kutangaza nafasi za ajira kwenye vitengo mbalimbali baada ya kipindi kirefu cha mpito kilichosababishwa na uhakiki wa watumishi hewa na wenye vyeti vya kughushi. Ongezeko kubwa la wahitumu limesababisha soko la ajira kuwa gumu, lakini changamoto kubwa ni kwamba wahitimu wengi hawajui hatua zinazopaswa kufuata wakati wa kujisajili kwenye mfumo wa Recruitment Portal.
Makala hii itakuelekeza jinsi ya kujenga ‘Profile’ yako hatua kwa hatua kulingana na muundo wa mfumo wa Ajira Portal ili uhakikishe unakidhi vigezo vya kuitwa kwenye usaili.
NAMNA YA KUJISAJILI AJIRA PORTAL (HATUA KWA HATUA)
Ili kuanza mchakato wako, tembelea tovuti ya portal.ajira.go.tz na ufuate hatua hizi:
Kufungua Akaunti (Registration)
Bonyeza neno ‘Register’. Utatakiwa kuweka Baruapepe (Email) yako inayofanya kazi. Ni muhimu kutumia email yako binafsi. Baada ya hapo, nenda kwenye email yako ili kuthibitisha (Verify) akaunti yako kupitia link utakayotumiwa.
Kujaza Taarifa Binafsi (Personal Details)
Hapa ndipo unapoingiza jina lako kamili, tarehe ya kuzaliwa, na namba yako ya NIDA. Mfumo huu umeunganishwa na NIDA, hivyo hakikisha majina yako yanashabihiana na yale yaliyopo kwenye vitambulisho vyako.
Muonekano wa Menu ya Ajira Portal Dashboard
Academic Qualifications (Elimu)
Hapa utaingiza vyeti vyako vya Kidato cha Nne, Sita, na Chuo. ZINGATIA: Kila cheti kinapaswa ku-scaniwa katika mfumo wa PDF na kugongwa muhuri wa Mwanasheria (Certified True Copy). Transcripts hazikubaliki kama mbadala wa cheti halisi.
Professional Qualifications & Experience
Kama una leseni kutoka bodi za kitaalamu (mfano: NBAA, ERB, Bodi ya Walimu n.k), ziingize hapa. Pia, weka historia yako ya kazi (Working Experience) kwa kuanza na kazi ya sasa kuelekea ulikoanzia.
MAMBO 10 YA KUZINGATIA WAKATI WA KUFANYA MAOMBI
- 1. Vyeti Halisi (Original Only): Usi-upload result slip au transcript. Mfumo unahitaji Academic Certificate pekee.
- 2. Email na Password: Fungua email yako mwenyewe na uhifadhi password vizuri. Usitumie email ya Stationary.
- 3. Uhakiki wa Mwanasheria: Vyeti vyote lazima vihakikiwe na kugongwa muhuri na Wakili au Mahakama.
- 4. Picha (Passport Size): Piga picha rasmi na uhifadhi ‘soft copy’ yenye jina lako.
- 5. Scanning Ubora: Hakikisha vyeti vinaonekana vizuri baada ya kuscan. Tumia mfumo wa PDF.
- 6. Majina ya Mafaili: Ipe mafaili majina yanayoeleweka (mfano: “Form Four.pdf”).
- 7. Profile Completion (90%+): Hakikisha profile yako imekamilika kwa zaidi ya 90% ndipo uombe kazi.
- 8. Barua ya Maombi: Andika barua mahususi kwa kila nafasi unayoomba na i-upload kulingana na tangazo.
- 9. NIDA Number: Hakikisha una namba ya NIDA iliyo sahihi kwani inatumika kuvuta taarifa zako binafsi.
- 10. Muda wa Maombi: Usisubiri siku ya mwisho. Mfumo huwa na msongamano mkubwa saa za lala salama.
NYARAKA MUHIMU UNAPOKUJA KWENYE USAILI
Ikiwa utafanikiwa kuitwa kwenye usaili (Interview), unapaswa kuwa na nyaraka hizi halisi (Originals):
- Cheti halisi cha kuzaliwa: Ni lazima kwa ajili ya kuthibitisha umri na uraia.
- Utambulisho: NIDA, Pasipoti, Leseni, au Barua ya Serikali ya Mtaa.
- Vyeti halisi vya kitaaluma: Kidato cha nne, sita na chuo.
- Hati ya Kiapo: Ikiwa una tofauti yoyote ya majina kwenye nyaraka zako.
- Waliosoma Nje: Vyeti vihakikiwe na TCU, NACTE au NECTA.
VITU VYA MSINGI VYA KUZINGATIA KWENYE MFUMO
Watafuta kazi wengi hukataliwa (disqualified) kwa sababu ya kukiuka masharti ya jumla:
- Umri: Kisheria mwombaji anapaswa kuwa na umri usiozidi miaka 45 kwa ajira za kudumu.
- Njia ya Maombi: Barua kwa mkono hazikubaliki kabisa. Maombi yote ni kwa njia ya mtandao.
- Kazi ya Sasa: Kama tayari ni mtumishi wa umma, ni lazima barua yako ipite kwa mwajiri wako na igongwe mhuri.
- Uraia: Waombaji lazima wawe Raia wa Tanzania.
Kamilisha Maombi Yako Kwa Usahihi!
Kufaulu Ajira Portal kunahitaji umakini na kufuata kanuni. Ikiwa unahitaji kusaidiwa kuandaa **CV ya kitaalamu** au barua ya maombi, au unahitaji ushauri wa kina kuhusu mchakato wa usaili, bonyeza kifungo hapa chini.
KWA USHAURI ZAIDI
Ikiwa bado unayo maswali au unahitaji muongozo zaidi kuhusu usaili na maandalizi ya kazi serikalini, tunakushauri yafuatayo:
- Pitia tovuti ya Sekretarieti ya Ajira (www.ajira.go.tz) mara kwa mara kwa taarifa za hivi karibuni.
- Jiunge na majukwaa ya kijamii yanayotoa mafunzo ya usaili (Interviews prep).
- Hakikisha unabadilisha namba zako za simu na email kwenye mfumo ikiwa utapoteza zile za mwanzo.
- Muhimu: Usikubali kutuma pesa kwa mtu yeyote anayeahidi kukupa ajira serikalini. Ajira ni za ushindani na bure!
