Maelezo haya ya Kiswahili Form Two yanahusu Uundaji wa Maneno. Yamepangwa katika sehemu zilizo wazi ili kurahisisha kusoma, kuelewa na kufanya marudio.
Uundaji wa maneno ni ujenzi au uzalishaji au utengenezaji wa maneno mapya. Uundaji wa maneno mapya husaidia kuongeza msamiati katika lugha ili kukidhi mahitaji ya mawasiliano. Uundaji wa maneno mapya husababishwa na mabadiliko ya kiuchumi, kisiasa na kiutamaduni na maendeleo ya kisayansi yanayotokea katika jamii. Kwa mfano tunayo maneno mapya, kama vile
ufisadi, uwekezaji, ukeketaji, ujasiriamali na mengine mengi kutokana na mabadiliko ya kijamii.
Kutumia Uambishaji
Kubainisha Mofimu katika Maneno
Uambishaji wa maneno ni kitendo cha kupata maneno kwa kubandika Mofimu kwenye kiini cha neno, uambishaji kutokea kabla ya kiini cha neno au mzizi wa neno. Mfano kiini pig- unaweza kuunda maneno kama inapiga, anayepiga, mpigaji, amepigika nk.
Mofimu zinazobadilika kwenye kiini cha neno huitwa Viambishi.
Katika lugha ya Kiswahili viambishi hutokea kabla na baada ya kiini cha neno.
Mfano
Wanapendana = Wa-na-pendan-a kiini cha neno ni-pend-.
Mofimu zilizobadilisha baada ya kiini —an-na-a viambishi vinavyotokea kabla ya kiini cha neno huitwa viambisha awali au tangulizi. Viambisha vinavyotokea baada ya kiini cha neno huitwa viambishi tamati au fuatishi.
Example 1
Angalia mifano ifuatayo:
- Unapendelea -penda el-e-a
- Waliongozana wa-li- -ongoz- an-a
- Analima a-na- -lim- “a
- anayeiimbisha a-na-ye -imb- -ish-a
Dhima za Mofimu
Bainisha dhima za mofimu Baadhi ya dhima za uambishaji ni kama ifuatavyo: 1. Kuonyesha upatanisho wa usanifu maana ya maneno yanayozalishwa kutofautiana katika msingi wa kusanifu tu, lakini uhusiano wa maneno hayo hutokana na kiini au mzizi wake
uleule.Mfano;Fundisha kiini chake ni fund. Unaweza kuzalisha maneno mengine kwa
| kutumia = mzizi/ki
5.
6.
Vitenzi vikiambishwa huweza kujenga/kuunda/kuzalisha vitenzi vingine au nomino.
- fundishwa, fundishana.
- Uambishaji huonyesha nafsi
- Uambashaji huonyesha njeo (muda)
- Uambishaji huonyesha urejeshi
- Uambishaji huonyesha ukanushi
Uambishaji huonyesha hali mbalimbali za kitenzi
Example 2
Mfano
kilichopo kama vile fundishana,
mafundisho,
mfundishaji,
-chez- Mchezaji, mchezo wanacheza/atamchezea
Piga
-pig- Mpigaji, Mpiganaji_ —_watanipiga, aliyempiga/wanaompiga
Uambishaji hutumika kuzalisha viwakilishi na vielezi.
Huyu, Huyo Hu Humu, humo Wangu, wako,wake wa Hii, hizo, hiki hi
Viambishi awali vina dhima ya kudokeza nafsi, njia, idadi urejeshi na ukanushi.Mfano:
Hawakulima
Ha-, kiambishi cha ukanushi
Ku-, kiambishi njeo/wakati
Viambishi tamati vina dhima mbalimbali hudokeza hali ya utendekaji, ukamilishaji au kimalizio
cha neno na kauli za matendo kama vile kutendwa, kutendewa,kutendeka nk.
Dhima:Ukanusho, kutendeana, agizo na mtendwa, ukamilisho, usababishi.
Mfano
Neno
Anapiga
wT =
‘anapigana -an Asipigwe -w
Amempigisha ~ish-
Viambishi tamati vina dhima ya kutambulishwa mapema/nomino zilizoundwa kutokana na vitenzi.
SS Ee ES eee Piga pig- -o
Mchezo chez- 0
Mtembezi tembe- Zi
Mfiwa -fi- -us-a
Kutumia Mnyumbuliko
Mazingira yanayosababisha Mahitaji ya Maneno Mapya
Elezea mazingira yanayosababisha mahitaji ya maneno mapya
Mnyumbulisho ni neno linalotokana na neno nyumbua. Kunyumbua kitu ni kuvuta, kuongeza urefu wa kitu hicho.
Kunyumbua katika lugha ya Kiswahili ni kuongeza vinyumbulishi katika katika kiini ili kupata msamiati mpya. Hivyo basi, mnyumbulisho ni njia mojawapo na inasaidia kuunda maneno kwa njia ya kunyumbulisha.
Viambishi vinapochukuliwa katika kiini cha neno, basi neno hilo huwa limenyumbulishwa. Kwa mfano neno lima kiini chake lim- huweza kunyumbulishwa na kupata maneno mengine mpya, kama lim-ishwa, lim-ia, lim-w-a.
Pia maneno ya mnyumbulisho yanaweza kuundwa kwa kuongeza viambishi kwenye shina, kwa
mfano: eleka Elekeana, elekea, elekwa, elekesha Shikishana shik shikisha Shikishana, shikisha, shikishaneni
Kwa ujumla tunawaza kusema kuwa maneno ya kawaida hunyumbulika. Hivyo kiini/mzizi au shina moja huweza kuzalisha maneno mengine mengi ambayo yanatokana na msingi moja wa maana.
Dhima ya Uambishaji na Mayambulikoa wa Maneno
— eee
Dhima ya uambishaji ni kuleta upatanisho wa kisarufi, kuonesha idadi na umoja na wingi katika
ngeli za majina, kuonesha njeo na kuonesha urejeshi pamoja na hali mbalimbali kwa uambikaji wa viambishi kabla ya mzizi wa neno. Aidha dhima ya mnyambuliko ni kuonesha matokeo ya tendo na kuzalisha kauli mbalimbali kwa kupachika viambishi baada ya mzizi wa neno.
Kuunda Maneno mbalimbali kwa kutumia Mnyambuliko
Unda maneno mbalimbali kwa kutumia mnyambuliko
Uundaji wa maneno mbalimbali kwa kutumia mnyambuliko hufanyika kwa kupachika viambishi baada ya mzizi wa neno na hivyo kulifanya neno husika liweze kuonesha matokeo mbalimbali ya
matendo pamoja na kuzalisha kauli mbalimbali za matendo.
Zoezi 1
Unda maneno mbalimbali kwa kutumia mnyambuliko
Kutumia Maneno ya Mayambuliko katika Miktadha mablimbali
Tumia maneno ya mnyambuliko katika miktadha mablimbali
Maneno ya mnyambuliko hutumika katika miktadha mbalimbali ambapo miktadha hiyo hujitokeza katika kauli mbalimbali za vitenzi. Kauli hizo ni kauli ya kutenda, kauli ya kutendwa, kauli ya kutendewa, kauli ya kutendea, kauli ya kutendeka, kauli ya kutendesha, kauli ya
kutendana, na kauli ya kutendama.
Zoezi 2
Tumia maneno ya mnyambuliko katika miktadha mablimbal
Maelezo Ya Ziada
UUNDAJI WA MANENO
Uundaji wa maneno ni shughuli ya kuunganisha viambajengo (vipashio) mbalimbali ili kupata maneno tofauti yenye maana mbalimbali ambazo ni kamili.
Kwa kuwa maendeleo ya jamii hubadilika, hukua na kuongezeka hivyohivyo lugha nayo hukua na kubadilika kwa lengo la kukidhi haja ya mawasiliano.
Ili msamiati uongezeke lazima maneno yaundwe kwa lengo la kuboresha mawasiliano kulingana na wakati uliopo.
Umuhimu Wa Uundaji Wa Maneno
1. Kupata msamiati wa kutosha katika lugha husika ili kukidhi mabadiliko yanayojitokeza.
2. Kukabiliana na suala la maendeleo ya sayansi na teknolojia katika ongezeko la maneno mapya.
3. Ubunifu wa maneno mbalimbali hutokana na njia mbalimbali kama vile uambishaji wa maneno, kubadili mpangilio wa herufi kutohoa maneno ya lugha nyingine, kuambatanisha maneno, kufananisha sauti, umbo, mlio.
Uundaji Wa Maneno Kwa Kutumia Mofimu=
(a) MOFIMU
1. Maana
• Mofimu ni kipashio kidogo chenye maana ya kisanifu na kileskia, kipashio hicho kinaweza kuwa sehemu ya neno au neno zima.
- Mofimu yenye maana ya kileskia aghalabu huwa na mofimu ambazo haziambatanishwi na kipashio kingine chochote.
- Mofimu – Ni kipashio kidogo kabisaa cha kiisimu ambacho kina maana kisarufi au kileksika.
Mfano; Baba, Mungu, Fikiri, bora
• Mofimu zenye maana ya kisarufi ni mofimu zinazoambatanishwa na mofimu nyingine katika uundaji wa maneno. Mofimu hizo huwa ni sehemu tu ya maneno yanayoambatanishwa katika mzizi wa neno mfano:
– M – toto
– Tu – ta- pi – ka
– U – som – i
Katika Kiswahili, mofimu inaangaliwa katika daraja la vipashio vya lugha. kipashio hiki hakiwezi kuvunjwavunjwa zaidi bila kupoteza maana.
1. Mtoto (Watoto)
– Hapa kuna mofimu mbili katika neno hili mofimu ya kwanza ni m – ambayo ni mofimu ya kisarufi inayoonesha idadi (umoja) na ''wa'' katika wingi.
– Mofimu ya pili ni toto ambayo ndio shina la neno hilo, kwa kutumia shina hili unaweza kupata maneno mengine kama vile utoto, vitoto, kitoto, kijitoto.
– Mofimu shina (toto) ni mofimu ya kileskia yaani ni mofimu yenye maana kamili na ambayo yaweza kutumika kuundia maneno mengine katika lugha.
– Mofimu (m-) katika “mtoto” ni mofimu ambayo maana yake hudhihirika kutokana na kujitegemeza katika mofimu ya kileskia. Bila kujiegemeza kwenye mzizi wa neno maana yake haiwezi kubainika.
Aina Za Mofimu
Kuna aina kuu mbili za mofimu
(i) Mofimu huru (sahihi)
(ii) Mofimu tegemezi
1. Mofimu Huru/ Sahihi
Ni mofimu inayoweza kusimama peke yake na kuweza kutumiwa katika tungo bila kuwa na kiambishi chochote. Mofimu huru zina hadhi ya neno na zinaweza kuwa aina yoyote ya neno kama vile: –
– Majina (nomino): juma, simba, baba, mama, dada, kaka
– Viwakilishi: mimi, sisi, yeye, wao, ninyi
– Vivumishi: safi, chafu, kile, refu
– Vitenzi: Sali, tafiti, jibu
– Viunganishi: na, hata, hadi
– Vielezi: haraka , polepole, sana, mno
2. Mofimu Tegemezi
Ni mofimu zinazofungamana na mofimu nyingine na zinapotumika hutegemeana ili kueleza dhana iliyokusudiwa. Mofimu hizi zinapofungamana huunda neno. Mofimu zinazounda neno huweza kuwa mbili au zaidi kulingana na mchangamano wa dhana ulio katika neno linaloundwa
Mtoto – m- toto
Watacheza – wa – ta – chez – a
Anasoma – a – na – som –a
Mkulima – m – ku – lim –a
Nafsi
Nafsi katika umoja nafsi katika wingi
(i) mimi NI sisi TU
(ii) wewe U ninyi M
(iii) yeye A wao WA
Neno “analima” lina mofimu nne (4) ambazo hufungamana na kujenga neno “analima” kila moja ya mofimu hizi isimamapo peke yake haina maana yoyote isipokuwa ina maana kisarufi ambayo humuwezesha mwanaisimu kuchambua maana ya mofimu hiyo.
Analima – a – na- lim – a
A – kiambishi awali kipatanishi cha nafsi ya III umoja
Na – kiambishi awali cha wakati uliopo
Lim – mzizi wa neno
A – kiambishi tamati
Dhima kuu ya mofimu ni kuongeza msamiati. Msamiati huo unaweza kuongezeka kwa kuunda
neno zima. Pia msamiati unaweza kuundwa kwa shina moja kwa kuweza kuunda na kutoa maneno yenye maana mbalimbali.
Neno “cheza” linaweza kuwa : mchezaji, mchezo, wanachezea, tulicheza, uchezeshaji, alimchezesha n.k.
Vilevile mofimu tegemezi zina dhima mbalimbali tofauti na uundaji wa msamiati. Baadhi ya dhima hizi ni kama vile,
- kudokeza nafsi
- kuonesha njeo (wakati)
- kuonesha/ kudokeza urejeshi
- kudokeza ukanushi
- kudokeza kauli mbalimbali
(b) UUNDAJI WA MANENO KWA KUTUMIA UAMBISHAJI
(i) Maana
– Uambishaji ni kitendo cha kupachika kiambajengo (mofimu) cha neno kwenye mzizi wa neno ili kukamilisha muundo wa neno
Viambishi
– Viambishi vinavyowekwa kwenye mzizi wa neno na kukamilisha muundo wa neno hilo. Viambishi vinaweza kuambilishwa kabla au baada ya mzizi wa neno (kiambishi kinaweza kupachikwa mwanzoni na mwishoni mwa mzizi wa neno ).
AU
– Viambishi ni mofimu muhimu sana katika uundaji wa maneno mapya kutokana na mzizi wa neno moja.
AU – Viambishi ni mofimu zinazowekwa kwenye mzizi wa neno na kukamilisha muundo wa neno.
Kwa mfano neno: ANAYEJIPIKIA
Viambishi awali (mwanzoni) vyake ni A – NA- YE – JI
Viambishi tamati ni –I – A – na mzizi wa neno hilo ni – PIK-
Aina Za Viambishi
(a) Viambishi awali
– Hivi ni viambishi vinavyowekwa kabla ya mzizi wa neno navyo ni vitano
(ii) Viambishi ngeli
M – tu = wa – tu
M – ti = mi – ti
M – zuri = wa – zuri
M – safi = wa – safi
(iii) Kipatanishi (kiambishi awali cha nafsi)
Hivi hujitokeza katika vitenzi na wakati fulani huitwa viambishi awali vya nafsi
Mfano: – Umoja Wingi
Ni – nalima tu – nalima (nafsi 1)
U – nalima m – nalima (nafsi 2)
A – nalima wa – nalima ( nafsi 3)
(iv) viambishi awali vya wakati (njeo)
Hivi huonesha wakati tendo limefanyika katika kitenzi
Mfano: analima
A – na- lima (wakati uliopo)
A – li – lima (wakati uliopita)
A – ta – lima (wakati ujao)
(v) Viambishi awali vya hali
Hivi huonesha hali mbalimbali katika kitenzi
Hu – lima (hali ya mazoea)
A – me – lima (hali timilifu)
A- nge – lima ( hali ya masharti)
(vi) viambishi awali vya rejeshi vya mtendaji wa jambo au tendo (kiima)
Hivi hutaja mtenda wa jambo
Ni – na- ji – kata
A – na – ye – sema
U – li – o – enea
(vii) Viambishi awali rejeshi vya mtendwa
Hivi hutaja mtendwa wa jambo
Tuli – u – panda
Nina – i – soma
Ana – m – piga
Wana – ni – soma
(viii) Viambishi awali vikanushi na yakinifu
Hivi huwekwa katika kitenzi ili kukamilisha hali ya kukanusha, viambishi vya kukanusha katika lugha ya Kiswahili ni ha – hu – na – si
U – naimba hu – imbi
Ni – nacheza si – chezi
A – naimba ha- imbi
(b) Viambishi kati
Ni viambishi vinavyopachikwa ndani ya mzizi wa neno na hivyo kuukuta katika sehemu mbili. Viambishi kati havitokei katika Kiswahili lakini vipo katika sehemu nyingine, mfano kiebrania.
(c) Viambishi tamati
Hivi ni viambishi vinavyoambishwa baada ya mzizi wa neno navyo ni vya aina mbili.
(i) Viambishi tamati maana
Hivi hutokea baada ya mzizi wa kitenzi bila kubadilisha umbo la mzizi wenyewe. Viambishi tamati maana hutaja maana au dhana.
Lim –a
Lim – wa
Chez – a
Chez – wa
(ii) Viambishi tamati vijenzi
Hivi ni viambishi vinavyoandikwa baada ya mzizi wa kitenzi viambishi tamati vijenzi navyo hutokea mara baada ya mzizi wa kitenzi na vina kazi kuu nne.
(a) Kuleta maana ya ziada ya kule kwenye maana ya asili iliyobebwa na mzizi wa kitenzi.
Lima – limia- limika – limisha – limiwa
Tendo – tendea – tendeka – tendesha – tendewa
(b) Kujenga mzizi mpya wa kitenzi ambao utabebeshwa maana ya asili ya kitenzi na maana ya ziada. Mzizi huu mpya huitwa “mzizi wa mnyambuliko”
Kitenzi Mzizi asilia Mnyambuliko Mzizi wa mnyambuliko
Piga Pig – Pigana Pigan
Cheza Chez – Chezeka Chezek
Imba Imb – Imbisha Imbish
Ruka Ruk – Rukiana Rukian
Lima Lim – Limika limik
(d) Huweza kubadili neno toka aina moja na kuingia aina nyingine
Omba – ombeana – ombaji – ombeka – ombi – ombeaji
T T N T N T
(e) Kuweza kuzalisha kauli mbalimbali za tendo kama ifuatavyo;-
Kauli ya kutenda;- Chez – a Chek – a
Imb – a
Kauli ya kutendwa;- Chez – wa
Chek – wa
Imb – wa
Kauli ya kutendeka;- Chez – ek – a
Chek – ek – a
Imb – ik – a
Kauli ya kutendewa;- Chez – ew –a
Chek – ew – a
Imb – iw – a
Kauli ya kutendea Chez –e –a
Chek – e – a
Imb –i –a
Kauli ya kutendeana Cheze – an – a
Cheke – an – a
Imbi – an – a
Kauli ya kutendesha Cheze – sh – a
Cheke – sh – a
Imbi – sh – a
(a) MZIZI KIINI CHA KITENZI
Mzizi au kiini ni ile sehemu ya neno inayobakia baada ya kuondolewa aina zote za viambishi yaani viambishi awali na tamati (mzizi ni sehemu isiyobadilika).
Kuna aina mbili za mzizi
(i) Mzizi asilia
Huu ni mzizi unaobakia baada ya kuondolewa viambishi tamati vijenzi. Mzizi huu mpya hubeba maana ya ziada ya hivyo viambishi maana kama vile:
Neno Mzizi Asilia
Lima lim-
Lewa lew-
Cheza chez-
Ona on-
(ii) Mzizi mnyambuliko
Huu ni aina ya mzizi ambao hujengwa na mzizi asilia pamoja na viambishi tamati vijenzi. Mzizi huu mpya hubeba maana ya ziada ya hivyo viambishi.
Kitenzi Mzizi asilia Mnyambuliko Mzizi mnyambuliko
Tema tem Temana Teman
Pata Pat Patisha Patish
Lia Li Lilika Lilik
Kula Kul Liwa Liw
Soma Som Somana Soman
(b) SHINA LA KITENZI
Shina la kitenzi ni mzizi wowote (yaani mzizi asilia au mzizi wa mnyambuliko) uliofunguliwa irabu -a- isiyo na maana maalum ya sarufi.
Mzizi shina
Lim + a lima
Chez + a cheza
Fik +a fika
Liw +a liwa
Vitenzi vyenye asili ya kigeni ambao huishia na irabu e, i, u katika mzizi asilia yao.
– “arifu”
– “tafiti”
– “samehe”
– “Sali”
– “jibu”
Vitenzi hivyo, mzizi asilia na shina huwa kitu kimoja
Mzizi = shina + a
Shina = mzizi + a
Kubainisha Mofimu Au Viambishi
Kubainisha mofimu (viambishi) ni kitendo cha kutenga neno katika mofimu au viambishi vinavyolijenga.
Hatua Muhimu Katika Kubainisha Mofimu
Hatua zifuatazo ni muhimu katika kubainisha mofimu nazo ni: –
(a) Kutambua aina ya neno ( neno huru au changamano) huundwa na mofimu tegemezi. Neno huru halivunjwivunjwi lakini neno changamano linavunjwavunjwa na kubainisha mofimu zake. Mfano wa neno huru = dada, kaka, mama.
Mfano wa neno changamano = a – na – on – a
= anaona
(b) Kutenga (kuvunjavunja) mofimu au viambishi vinavyounda neno hilo yaani tambua viambishi awali, mzizi, kiini na viambishi tamati. Viambishi na mzizi hupatikana katika neno changamano
Bainisha mofimu katika maneno yafuatayo na eleza kazi za kila mofimu.
(i) Anasoma – a – na- som – a
1 2 3 4
- Kiambishi awali kipatanishi nafsi III umoja
- Kiambishi awali cha wakati uliopo
- Mzizi wa kitenzi
- Kiambishi tamati
(ii) Dunia – hili ni neno huru ambalo huundwa na mofimu hizi hazivunjwivunjwi
(iii) Waliompiga – wa – li- o – m – pig – a
1 2 3 4 5 6
- Kiambishi awali kipatanishi nafsi ya tatu wingi
- Kiambishi awali cha wakati uliopita
- Kiambishi awali rejeshi cha watenda
- Kiambishi awali rejeshi cha watendwa
- Mzizi wa kitenzi
- Kiambishi tamati
Dhima Ya Mofimu/ Viambishi
1. Kuonesha nafsi katika kitenzi
Ni – nasoma= Tu – nasoma – I
U – nasoma = m – nasoma – II
A – nasoma = wa – nasoma- III
2. Kuonesha njeo katika vitenzi
A – na – cheza – wakati uliopo
A – li – cheza – wakati uliopita
A – ta – cheza – wakati ujao
3. Kuonesha umoja na wingi katika nomino na viambishi
M – toto = wa – toto
Ki – su = vi -su
4. Kuonesha hali mbalimbali za kitenzi
Mfano: – hali ya masharti
A – ki – ja
A – nge – ku – ja
– Hali ya kuendelea kwa tendo = a – na – li – ma
– Hali timilifu= a – me – sem – a
– Hali ya mazoea= hu – soma
5. Kuonesha uyakinishi na ukanushi katika vitenzi
Mfano: – ni – nalima – si – limi
A – nacheza – ha – chezi
U – naimba – hu – imbi
6. Kuonesha urejeshi wa mtenda au mtendwa katika kitenzi
Mfano: – A – na – ye – lima – Mtenda
A – na – u – penda – mtendwa
7. Kuonesha kauli mbalimbali za vitenzi
Kauli ya kutenda – a – na – pik – a
Kauli ya kutendea – a – na -pik -i – a
Kauli ya kutendewa- a – na – pik – iw – a
Kauli ya kutendeana – wa – na – pik – ian – a
Kauli ya kutendesha – a – na – pik – ish – a
Kauli ya kutendwa – a – na – pik – w – a
Tofauti Ya Mofimu Na Silabi
Na Mofimu Silabi
Mofimu ni kipashio cha kiima Ni sehemu ya neno ambayo huweza 1 chenye maana kisarufi na kileksia kutamkwa mara moja na kwa pamoja kamusi kama fungu la sauti
Kila mofimu ina kazi maalum kisarufi
(mfano) analima Si kila silabi ina kazi maalumu mfano silabi ''bali" ikisimama peke yake A – na – lim – a haiwakilishi maana yoyote kisarufi
Katika silabi hakuna viambishi hivyo Katika mofimu kuna viambishi awali na tamati
Katika mofimu kuna mizizi, shina la Katika silabi hakuna mzizi wala shina. neno
- Silabi huvunjavunja hata mofimu huru
- Mofimu huru hazivunjwivunjwi,
- mfano;
- hubaki zilivyo mfano; neno baba
- lina mofimu huru moja
- baba – ba + ba = silabi mbili
- Silabi huvunjavunja mzizi wa neno
- Mofimu hazivunjivunji mzizi wa mfano; “analima” lina silabi nne
- neno mfano;
- A – na – li – ma
- Lima mzizi lim
- 1 2 3 4
- Mara nyingi katika neno kuna idadi
- Mara nyingi katika neno kuna idadi nyingi za silabi. Mfano;
- ndogo ya mofimu. Mfano; “mama”
- lina mofimu moja, anacheza lina Mama – lina silabi mbili
- mofimu nne
- Anacheza – lina silabi nne
(c) UUNDAJI WA MANENO KWA KUTUMIA MNYAMBULIKO
Unyambulishaji unatokana na neno “nyambua” ikiwa na maana refusha au vuta kitu.
Mnyambuliko ni kitendo cha uvutaji au urefushaji kipashio / vipashio katika mzizi wa neno. Aidha mnyambuliko unahusu upachikaji wa mofimu zinazofuata mzizi wa neno. Mofimu hizi huitwa mofimu fuatishi (viambishi tamati)
Soma – Som – e – a
Som – ek –a
Som – esh – a
Som – w – a
Som – ean – a
Som – o
Vitenzi
Vitenzi vyote vya Kiswahili isipokuwa kitenzi kishirikishi “ni” vinaweza kunyambulika.
Piga – pigia, pigana, pigisha, pigwa, pigiana, cheza, chezea, chezeana, chezeshwa, chezwa.
Baadhi ya majina ya ujumla hupokea viambishi tamati na mengine hupokea viambishi tamati vijenzi.
Nyumba – nyumbani
Bustani – bustanini
Hewa – hewani
Maji – majini
Viwakilishi
Hivi huchukua viambishi tamati maana
(a) Viwakilishi vya nafsi kama vile
Mimi – miye
Wewe – weye
Sisi – siye
Ninyi – niye
(b) Viwakilishi virejeshi vya amba.
- Ambalo
- Ambacho
- Ambavyo
Vivumishi
Hivi huchukua viambishi tamati vijenzi
Safi – safisha, safishwa, safishia, safishika
Fupi – fupika, fupisha, fupishika, fupishwa
Refu – refusha, refushwa, refushika
Viunganishi
Hesabu ndogo ya viunganishi huchukua viambishi tamati vitenzi.
Mfano : – Labda, labdatisha, labdilika, labdishwa.
Dhima Ya Mnyambuliko
(i) Mnyambuliko wa maneno hukuza msamiati wa lugha husika.
(ii) Mnyambuliko wa maneno hupanua maana ya maneno.
(iii) Mnyambuliko wa maneno huzalisha kauli mbalimbali za vitenzi kutenda, kutendwa, kutendea, kutendeka, kutendana, kutendeana kutendesha, kutendeshwa.
Continue Studying Form Two
Get the Complete PDF Notes
Would you like these notes in a well-formatted PDF for easier reading and offline study? Click below to ask for the complete PDF notes.