Skip to main content

Kiswahili Form Two Notes – Matumizi ya Lugha katika Miktadha Mbalimbali

Maelezo haya ya Kiswahili Form Two yanahusu Matumizi ya Lugha katika Miktadha Mbalimbali. Yamepangwa katika sehemu zilizo wazi ili kurahisisha kusoma, kuelewa na kufanya marudio.

—

Matumizi ya lugha ni namna ambavyo wazungumzaji wa lugha hutumia lugha kwa kuzingatia

mila, desturi na kaida mbalimbali za jamii inayohusika.

Rejesta

Kwa ujumla tunaweza kufasili rejesta kama mtindo wa lugha kutegemeana na kazi fulani, muktadha wa matumizi, lengo na uhusiano wa wanaowasiliana. Katika muktadha rasmi rejesta hurejelea upande mmoja kama vile, msamiati wa kiufundi, adabu maalum na matumizi ya lugha fasaha, mfano katika elimu, mahakamani na kadhalika.

Kuwasiliana kwa kutumia Rejesta

Rejesta za Mitaani

Haya ni mazungumzo yanayozungumzwa magengeni nayo hueleweka na wazungumzaji wenyewe. Ni lugha ambayo huchipuka kutokana na kikundi cha watu ambacho ni kidogo. Mfano wa maneno yanayotumika sana mitaani ni kama vile “Mshikaji” (rafiki) Demu” (mwanamke) nk. Kwa ujumla lugha ya mitaani ni lugha isiyo sanifu, ni lugha iliyojaa maneno ya mitaani

ambayo yanaeleweka kwa wazungumzaji wenyewe.

Mazungumzo ya Kwenye Shughuli Maalum (Rejesta za Mahali) Mazungumzo ya kwenye shughuli maalumu hayafanywi kiholela, bali yanafuata taratibu na kanuni maalum zinazojitokeza katika mazingira haya. Kutokana na kutumiwa kwake kwa muda mrefu kwenye mazingira yale yale.

Mazungumzo ya kwenye shughuli maalumu ni kama vile mazungumzo ya: Maofisini au mahali popote pa kazi

Mahakamani

Hotelini

Hospitalini

Msikitini

Kanisani n.k

Mazungumzo ya mahotelini yana utaratibu wake ambao katika hali ya kawaida inaweza

isieleweke.

— eee

Nani wali kuku?

B: Mimi

Chai moja wapi?

B: Hapa

| Katika mazungumzo haya A anapouliza “Nani wali kuku”, ana maana kuwa nani anahitaji kula

wali na nyama ya kuku”. Hapa hana maana ya kumwainisha mtu aitwaaye “wali kuku”.

| Kwa upande wa lugha ya mahakamani ni tofauti na lugha ya hotelini. Lugha ya mahakamani inasisitiza usahihi ili kuondoa migongano miongoni mwa wanaohusika. Mfano 1 Mfano:

Wakili wa Utetezi: Nakuuliza jaribio la kutaka kupindua serikali litakuwa kosa la namna gani katika sheria za Tanzania?

| Kamishna Msaidizi: (Baada ya kupewa kitabu cha sheria za Tanzania na kukisoma) Ni kosa la uhaini.

Wakili wa Utetezi: Ulichukua muda mrefu kufikia jibu hili. Washitakiwa wawili hawahusiani na | makosa haya?

| Kamishna Msaidizi: Sijui.

Kimsingi hii ni hali ya kawaida kabisa katika mahojiano ya mahakamani. Mara nyingi mahojiano katika mahakama hayaendi haraka sana. Kila mtu anaychusika — hakimu, mwendesha mashtaka,

wakili, mdaiwa, shahidi, n-k. hujieleza kwa wazi wazi bila kujali urefu wa maelezo.

Rejesta Zinazohusu Watu Rejesta zinazohusu watu ni yale mawasiliano yasiyo rasmi, ni yale maongezi ya kawaida ya kila

siku au mazungumzo rasmi; kwa mfano mazungumzo kati ya: © Vijana wenye rika moja, + Wazee wenyewe,

» Wanawake wenyewe,

+ Wanaume wenyewe,

+ Mwalimu na mwanafunzi, | – Meneja na wafanyakazi wake, | © Mtuna mpenzi wake, nk.

Mazungumzo miongoni mwa marafiki wa rika moja huzungumza lugha ambayo wao wenyewe

wanaielewa na sio rahisi kwa mtu wa rika lingine kuiclewa lugha hiyo.

| Mfano 2

Mfano:

‘Basi, Master jana wikiendi ilikuwa kibaridi sana. Basi nilizamia infoo kwenye zinga la mnuso huko saiti za upanga. Nilifika getini nikakuta baunsa kanyuti chedro likisubiri kumtoa noma kila mzamiaji. Alikuwa mnoko kishenzi. Akatema mkwara mbuzi, nikajibu kwa mkwaradume….akabloo mimi ndani’.

Maana ya Maneno

Wikiendi — Mwisho wa wiki

Kibaridi -tulivu

Kuzamia infoo — Kuingia mahali bila kualikwa

Zinga la Mnuso ~sherehe kubwa

Saiti -sehemu

Baunsa limenyuti chedro — Ni mlinzi wa mlangoni ametulia pembeni Noma — Hatari

Mnoko kishenzi — kinaa sana

Mkwara mbuzi — Vitisho dhaifu (Sani, Toleo Na 49).

Mtu asomapo maelezo hayo, mara moja unaona jinsi vijana hawa wa rika moja waishio mjini

wanavyozungumza Kiswahili. Si rahisi kwa mzungumzaji wa Kiswahili sanifu kuielewa kirahi lugha hiyo.

Dhima za Rejesta

Katika kipengele cha utambulisho wa kijamii tunaangalia namna aina ya lugha ya mazungumzo inavyoweza kujidhihirisha miongoni. mwa watumiaji. wake au kuwatambulisha na kuwatofautisha wanajamii husika. Pia katika utambaulisho wa kijamii tunaangalia vile ambavyo mtu hutambulika katika jamii kulingana na namna anavyoongea kulingana na hadhi, tabaka, na jinsi' ambavyo mtu huyo anavyoweza kusababisha mshikamano au mwachano_ katika mazungumzo. Kwa mfano jamii itamtambua mwanajamii kuwa ni msomi kulingana na mtindo wa lugha ya mazungumzo anaoutumia, au ni mtu wa mtaani kulingana na lugha anayotumia. Rejesta, ina nafasi kubwa sana katika maendeleo ya kiuchumi kwa mtu binafsi na taifa kwa ujumla. Hii ni kutokana na kwamba, madhumuni makuu ya mawasiliano katika biashara ni kuwavutia wateja na kuwafanya kuamini kuwa bidhaa ama huduma wanazouziwa ni za kiwango cha juu na ni thamani bora kwa pesa zao. Hivyo lugha ya biashara (rejesta), kwa kawaida ni

lugha ya kutangaza uzuri wa bidhaa au huduma, huwa na sentensi au vifungu vifupi, mfano

in wea gh wm Mahe wom

“Okoa mapesa chungu mbovu” pia huwa na lugha ya kupumbaza na kuaminisha, mfano “Kunywa XYZ kufumba na kufumbua afya yako itakurudia”.

Pia rejesta inasaidia sana kurahisisha mawasiliano miongoni mwa wazungumzaji katika masuala mbalimbali ya kibiashara na hata katika huduma mbalimbali za kijamii. Mfano hospitalini “mbili mara tatu”, hotelini “kuku wali tafadhali”, sokoni “kata nusu” na maeneo mengine.

Baadhi ya rejesta hutumika kupunguza idadi ya maneno hivyo kufanya mazungumzo yawe mafupi na yanayoeleweka kwa urahisi mfano rejesta za hotelini kama vile:- Muuzaji: wapi ng’ombe? Mteja: hapa Muuzaji: wapi chai chapati? Mteja: hapa.

Pia katika kutolea elimu ya dini kanisani na msikitini rejesta ina nafasi kubwa katika kujenga maadili.

Vilevile rejesta ina nafasi ya kupamba mazungumzo, wazungumzaji wengi wanapozungumza hapa na pale hupenda kutumia maneno tofautitofauti ili kufanya mazungumzo yawe ya kuvutia. Mfano mazungumzo miongoni mwa vijana:

Kijana 1: Niaje? Nakuona umechili

Kijana 2: mzuka jembe. Kama kawa… kama dawa!

Misimu

Kuwasiliana kwa Kutumia Misimu

Misimu ni semi za muda na mahali maalum ambazo huzuka na kutoweka kutegemea mazingira maalum. misimu inayodumu huweza kuingia katika methali, nahau au misemo ya lugha ya jamii hiyo.

Chanzo cha misimu

Misimu huzuka kulingana na mabadiliko ya kihistoria yanayoikumba jamii husika katika nyakati

mbalimbali.

Misimu huzuka kutokana na haja ya watu kuelezea hisia zoa juu ya matukio mbalimbali

yaliyotokea katika vipindi fulani kwa mfano, njaa, mafuriko, vita n.k. Aina za misimu

  1. Misimu ya pekee. Hii ni misimu ambayo huelezea mahusiano ya kikundi kimoja kutoka katika utamaduni mmoja, na hujulikana miongoni mwao pekee.
  2. Misimu ya kitarafa, Misimu hii hujulikana na watu wengi katikia eneo kubwa, yaweza

kuwa ni kata, wilaya au tarafa.

| 3. Misimu zagao. Ni misimu iliyocnea nchi nzima au pengine kuvuka mipaka ya nchi,

misimu hii husikika redioni, magazetini na hata kwenye vitabu. Msimu uliokita mizizi

sana huweza kusanifishwa na kuwa msamiati rasmi.

Sifa za misimu

| + Huzuka na kutoweka kufuatana na mabadiliko ya jamii

* Nilugha isiyo sanifu

e Inachuki

* Nilugha ya mafumbo

+ Ina maana nyingi Dhima ya misimu

* Hutumika kupamba lugha

* Hutumika kukuza lugha

+ Hutumika kutunza historia ya jamii fulani

| © Hutumika kuibua hisia mbalimbali za wazungumzaji

  • | ¢ Hufurahisha na kuchekesha
  • Lugha ya Kimazungumzo na ya Kimaandishi
  • Sifa ya Lugha ya Kimazungumzo
  • Lugha ya mazugumzo ni maongezi ya watu wawili au zaidi bila kutumia maandishi. Lugha ya
  • mazungumzo ambayo ndiyo lugha kongwe zaidi ya lugha ya maandishi ina dhima kubwa ya
  • kufanikisha mawasiliano miongoni mwa watu au kikundi fulani. Lugha hii ya mazungumzo
  • ilianza punde tu binadamu alipoanza kukabiliana na mazingira yake, hivyo kimsingi lugha ya
  • mazungumzo ndiyo nguzo kuu ya kufanikisha shughuli zote za kibinadamu kutokana na nafasi
  • yake kimatumizi.
  • Faida ya lugha ya mazungumzo

¢ Mzungumzaji anaweza kukaa ana kwa ana na msikilizaji, hivyo hukuza uhusiano.

| + Mzungumzaji anaweza kutumia ishara za mwili katika kusisitiza maelezo yake.

+ Mzungumzaji anaweza kupata nafasi ya kuuliza au kuulizwa maswali.

}) ©) Mzungumzaji anaweza kuonesha hisia zake kwa kulia, kupaza sauti, kupunguza sauti, kuonyesha

| furaha huzuni au hasira.

+ Mzungumzaji anaweza kuuliza maswali, kuona hisia za mzungumzaji kwa kusikiliza lugha

zinazotolewa na kuangalia ishara za mwili zinazotumika.

{ . atempennenene

Mzungumzaji anaweza kupata nafasi ya kufuta usemi wake, kuongezea jambo au kutoa maclezo

ya ziada.

Mzungumzaji anaweza kubadilisha lugha yake kulingana na mazingira aliyomo. Mzungumzaji anao uhuru wa kutumia lugha ya mitaani, misimu kulingana na muktadha. Matatizo ya lugha ya mazungumzo

Maelezo lazima yahifadhiwe kichwani, hivyo kama mtu hana kumbukumbu, taarifa zilizotolewa

hupotea na kusahaulika.

Mtumiaji wa lugha ya mazungumzo anaweza kurudiarudia vipengele fulani na hivyo kuichosha

hadhira. Ujumbe unaweza usieleweka kama unatolewa kwenye kelele nyingi

Lugha ya maandishi Hii ni lugha inayowasilishwa kwa njia ya maandishi. Lugha ya maandishi huzihusiha pande mbili, mwandishi na msomaji. Lugha ya maandishi sharti iwe fasaha ili msomaji anaposoma maandishi hayo, apate kuelewa kila kitu, yaani asibaki akijiuliza maswali.

Lugha ya maandishi huambatana na alama za uakifishaaji, hii husaidia maandishi kusomeka

vizuri na kueleweka kwa urahisi

Ubora wa lugha ya maandishi Lugha ya maandishi huwawezesha watu walio mbali kuwasiliana.

Lugha ya maandishi hustawisha sarufi ya lugha na misingi yake, kwa sababu mwandishi

anahakikisha kwamba anazingatia vizuri kanuni za kisarufi ili msomaji wake aweze kumwelewa.

Ili kuhakikisha maelezo yake yanaeleweka mwandishi analazimika kuandika kwa uwazi na kwa

kuzingatia kanuni na miko yote ya uandishi. Usdhaifu wa lugha ya maandishi

Lugha hii hutumiwa na wale tu wanaojua kusoma na kuandika. Lugha ya maandishi haina msisimko uletwao na lafudhi na matamshi.

Msomaji hukosa vidokezo vingi ambavyo katika lugha ya mazungumzo huchangia katika

mawasiliano.

Lugha ya maandshi inamnyima mwandishi nafasi ya kupima welewa wa msomaji kwa kuwa

hamwoni.

Dhima ya lugha ya mazungumzo na lugha ya maandishi

— ee eee eee

Lugha ya mazungumzo na lugha ya maandshi zote zina umuhimu wa pekee katika maisha ya kila siku kwa sababu ndizo zinzaowezesha watu kuwasiliana kwa namna mbalimbali.

Umuhimu wa lugha ya maandshi pia hutokana na dhima yake kwa watu. Maandishi yanaweza

kuhifadhiwa na kusambazwa kwa watu wengi hata walio mbali. Maandishi yanahifadhi

ine wanaweza kusoma na

| kumbukumbu na kwa muda mrefu. Kwa hali hii, watu wa vizazi vi kujua mambo yaliyofanyika kame nyingi zilizopita.

| Tofauti kati ya lugha ya mazungumzo na lugha ya maandishi

1. Lugha ya mazungumzo huwezesha mawasiliano ya ana kwa ana lakini lugha ya

maandishi haiwezeshi mawasiliano ya ana kwa ana.

Lugha ya mazungumzo haihitaji maandalizi wakati ugha ya maandishi huhitaji maandalizi. Mwandishi atalazimika kupata muda wa kuandika pamoja na kuandaa vifaa kama vile kalamu, karatasi n.k

| 3. Lugha ya mazungumzo hailazimiki kuzingatia kanuni za kisarufi, lakini lugha ya maandshi hutakiwa kuzingatia kanuni za kisarufi.

| Tofauti nyingine kati ya lugha ya maandishi na lugha ya mazungumzo huweza kuonyeshwa

katika jedwali lifuatalo.

  • Kipengele Mazungumzo Maandishi 1, Wahusika huonana 1, Wahusika hawaonani
  • Viungo vya mwili hutumika 2. Viungo vya mwili havitumiki
  • Maandalizi na matumizi hufanyika 3. Maandalizi_hufanyika kabla ] Maktadha wakati mmoja ya matumizi Mada Hazina uzito mkubwa Huelekea kuwa na uzito mkubwa. Mpangilio wa mada Hautabiriki. Unaclekea kutokuwa na Hutabirika. Huelekea kuwa na na mawazo mtiririko. mtiririko.

Hauelekei kuwa na kina. Hazichujwi kwa Mjadala wa mada _uaangalifu. Unaelekea kuwa na kina. Huchujwa.

Dhima ya matumizi ya lugha

| Dhima kuu ya lugha ni kupashana habari, ujuzi na maarifa mbalimbali. Vilevile lugha husaidia | kujenga uhusiano mwema baina ya watu. Uhusiano huo unaweza kuwa wa kijamii, kielimu, | kibiashara, kihuduma, kisiasa, kiuchumi n.k. Kwa hiyo, kujua jinsi ya kuitumia lugha kama

inavyotakiwa, kunasaidia kufikisha vizuri ujumbe unaotakiwa bila kuupotosha. Vilevile

kunasaidia kuepuka migongano, hasa ya kijamii kwa kuwa utakuwa umetumia lugha kwa mujibu

wa mila na desturi za jamii inayohusika.

Mambo ya kuzingatia katika matumizi ya lugha

| 1. Mada inayozungumziwa: Mada za mazungumzo zipo nyingi. Kuna mada za kijamii, kwa mafano ndoa, unyago, mapenzi, kif, matanga, burudani, muziki n.k. Kuna mada za | kibiashara kwa mfano bidhaa, kodi, vibali, fedha, hasara, faida n.k. Kwa hiyo, ili

mazungumzo yaweze kwenda vizuri, wazungumzaji wanatakiwa kuzingatia mada husika.

v

Muktadha wa mazungumzo: Mazungumzo yanaweza kuathiriwa na miktadha tofauti. Kwa mfano kuna miktadha ya kidini, kiganga, huzuni, sherehe, kisiasa, kielimu, kibiashara n.k. Mazungumzo yanaweza kufanyika mjini, kijijini, ugenini, shuleni, dukani, hotelini n.k

| 3. Malengo ya mazungumzo hayo: Malengo ya mazungumzo nayo yanaathiri matumizi ya lugha. Kwa mfano, lengo linaweza kutoa taarifa, kuhoji, kukejeli, kutia moyo n.k. Sasa | jinsi lugha itakavyotumika katika kutoa taarifa ni tofauti na itakavyotumika katika kutia

moyo au kukejeli.

| 4. Uhusiano uliopo baina ya wazungumzaji: Matumizi ya lugha huweza kuathiriwa pia na mahusiano ya wazungumzaji. Kuna mazungumzo baina ya watoto, wanafunzi, wazee, viongozi, marafiki n.k. Upo uhusiano wa daktari na mgonjwa, mwalimu na mwanafunzi, mnunuzi na muuzaji. Kwa hiyo mazingira baina ya pande hizi mbili yatategemea uhusiano wao, kwa hiyo kaida za uhusiano huu utapaswa kuzingatiwa. Kwa hiyo, kwa kuzingatia mambo haya manne, itawafanya wazungumzaji wawe makini katika uteuzi wa

maneno, miundo, mifano na kina cha ufafanuzi wa maelezo au habari inayozungumzwa.

Dhima ya Lugha ya Kimazungumzo na ya Kimaandishi

Lugha ya kimazungumzo na ya kimaandishi zina dhima kuu ya kupasha habari, ujuzi, na maarifa | mbalimbali, husaidia kujenga uhusiano mwema baina ya watu, kufikisha ujumbe unaotakiwa vizuri bila kupotosha, kufundishia ujuzi, kuchochea maendeleo, kuhifadhi historia ya jamii na | kueleza mawazo au hisia za watu. Lugha ya Kimazungumzo na ya Kimaandishi katika Miktadha Sahihi

| Tumia lugha ya kimazungumzo na ya kimaandishi katika miktadha sahihi

| Matumizi ya lugha ya kimazungumzo na ya kimaandishi katika muktadha sahihi huongozwa na mambo yafuatayo, ambayo ni mada inayozungumzwa, muktadha au mahali mazungumzo hayo

yanapofanyika, malengo ya mazungumzo hayo na uhusiano uliopo kati ya wazungumzaji.

Zoezi I. Tumia lugha ya kimazungumzo na ya kimaandishi katika miktadha sahihi.

Matamshi na Lafudhi ya Kiswahili

Matamshi ni namna ambavyo mtu anatamka neno au jinsi mtu anavyozungumza lugha. Unaposema fulani ana matamshi mazuri ya Kiswahili utakuwa unamaanisha anazungumza Kiswahili fasaha.

Neno moja linaweza kuzungumzwa/kutamkwa kwa namna tofauti na watu mbalimbali kutokana na sababu mbali mbali, sababu hizo ni pamoja na enco la kijiografia anakotoka huyo mtu, kabila lake, kundi lake la kijamii mfano msanii au mwanasiasa, na elimu aliyonayo. Hizi zote zinaweza

zikawa ni sababu za kufanya watu watofautiane katika matamshi.

Lafudhi Mbalimbali za Kiswahili Dhana ya matamshi huhusisha

  • Sauti za lugha husika
  • Mkazo
  • Kiimbo
  • Sauti za lugha ya Kiswahili

Sauti za ugha ya Kiswahili hujumuisha irabu na konsonanti, ambazo kwa ujumla huunda sauti 24, irabu tano na konsonanti 19 (konsonanti x na q hazipo katika matamshi ya kiswahili). Sauti za Kiswahili hutamkwa kama zilivyoandikwa, kwa mfano maneno “data” au “dengue” wewe unayatamkaje? Wengi huyatamka kama yalivyo hata kama wakiwa wanazungumza kiingereza, hii ni kwa sababu maneno ya Kiswahili hutamkwa kama yalivyoandikwa.

Kwa hiyo unapotamka maneno ya Kiswahili ni sharti uzingatie sauti asilia za lugha ya Kiswahili. Kuna watu huwa wanaandika hivi “xaxa”, hii huwa unaitamkaje? Au “ucjal” huwa unaitamkaje? Kwa kufuata matamshi asilia ya Kiswahili “ucjal” itatamkwa “uchijal” sijui itakuwa ina maana gani sasa. Na pengine umekuwa ukitumia maandishi ya namna hii hata kwenye insha zako ukidhani upo sahihi au ni kwa mazoea tu, sasa kwa kuwa umejua matamshi sahihi ya Kiswahili ni yapi, utajifunza kuyatumia kwa usahihi katika maandishi rasmi na yasiyo rasmi.

Mkazo

Katika lugha ya Kiswahili kuna namna ya kutamka maneno ili kuleta maana mbali mbali, kwa mfano neno “barabara” litaleta maana husika kulingana na jinsi lilivyotamkwa. Hivyo, mkazo ni

pale silabi inapotamkwa kwa kukazwa. Maneno ya Kiswahili huwa na silabi moja ambayo

hutamkwa kwa nguvu zaidi kuliko silabi nyingine. Unapotamka silabi iliyotiwa mkazo, sauti hupandishwa juu kiasi.

Maneno mengi ya Kiswahili, hasa yale yenye asili ya Kibantu hutia mkazo katika silabi ya pili kutoka mwisho.

Kwa mfano:ba ‘bu, maya ‘i, rama ’ni (mimi nilikuwa nikitamka ra’mani), baraba'ra (njia).

Baadhi ya maneno yenye asili ya kigeni, huwa na mkazo katika silabi nyingine. Kwa

mfano: bara’bara (sawa sawa), Alha'misi

Kiimbo Ni utaratibu maalum wa upandaji na ushukaji wa mawimbi ya sauti unaojitokeza katika utamkaji wa lugha fulani.

Katika utaratibu wa utamkaji, dhana ya Kiimbo huandamana pia na dhanna ya kidatu (yaani , kiwango cha juu, cha chini au cha kati cha sauti katika usemaj), Kwa hivyo ni muhimu hapa kueleza tofauti zilizopo baina ya kiimbo na kidatu. Wakati kiimbo kina maana ya kupanda na kushuka kwa mawimbi ya sauti ya lugha, kidatu kina maana ya kiwango cha sauti isikikayo,

wakati wa utamkaji ama kuwa juu, kuwa katikati au kuwa chini.

Aina za viimbo

Kiimbo cha maelezo: Kiimbo cha maelezo ni kile ambacho kwa kawaida msemaji wa lugha akiwa kwenye kidatu chochote kile mawimbi sauti ya usemaji wake yanakuwa takriban katika mstari ulionyooka. Mfano, Mwalimu anafundisha.

Kiimbo cha maulizo: Kiimbo cha kuuliza hujitokeza kwa kutumia viwango tofauti vya kidatu

kutegemeana na aina ya swali linaloulizwa. Mfano, mwalimu anafundisha?

Kiimbo cha amri: kiimbo cha amri hakitofautiyani sana na kiimbo cha maulizo. Kiimbo cha amri, mzungumzaji hutumia kidatu cha juu zaidi kuliko ilivyo katika kiimbo cha maelezo. Mfano, njoo hapa!

Lafudhi ya Kiswahili

Lafudhi ni matamshi ya msemaji wa lugha fulani ambayo yanatokana na athari za kimazingira. Mazingira hayo yanaweza kuwa enco atokalo mtu, mahali alikosomea, kiwango chake cha elimu, tabaka lake la kijamii na kadhalika.

Lugha ya Kiswahili ni lugha ya pili kwa watumiaji wengi wa afrika mashariki, kwa hiyo hii inafanya kuwatambua wazungumzaji wa Kiswahili kulingana na makabila yao au maeneo

wanakotoka. Kwa mfano, kwa hapa Tanzania tunaweza kuwatambua watu wa mwanza kwa

| lafudhi

Musoma kwa lafudhi yao.

Mfano

Mifano

y

z

Utata

yao, watu wa mtwara kwa lafudhi yao, watu wa pemba kwa lafudhi yao au watu wa

3.

Usiniretee maswara ya ubaguzi wa kikabira hapa (Wakuria) Amemupiga mutoto ya watu juu amemuibia mfaranga makumi mawili (Wakongo) Ukikaa nchale, ukichimama nchale (Wamakonde)

Wewe unakamuaga mang’ombe tu moja kwa moja (Wasukuma)

Mbona_ unakuwa_ kinganganizi, nilishakwambia_ sikupendi lakini wewe bado

unaningangania tu! (Wahaya)

katika Mawasiliano

Utata ni hali ya neno au sentensi kuwa na maana zaidi ya moja. Kwa hiyo tungo tata ni tungo

ambayo inaweza kuwa na maana zaidi ya moja.

Sababu Utata k:

L

Mfano

Mfano:

+ Alimpigia ukorofi wake (kwa sababu ya)

za Utata

atika tungo hutokea kwa sababu zifuatazo:

Neno kuwa na maana zaidi ya moja, kwa mfano neno mbuzi, kata n.k.

Kutozingatia taratibu za uandishi, Mfano; Tulimkuta Nyammy na rafiki yake, Mazala vs Tulimkuta Nyammy na rafiki yake Mazala. Katika sentensi hizi alama (,) ndio huleta tofauti, sentensi ya kwanza inamaana kulikuwa na watu wawili Nyammy na rafiki yake aitwaye Mazala na sentensi ya pili isiyo na alama (,) inamaanisha kulikuwa na watu wawili Nyammy na mtu mwingine ambaye ni rafiki yake Mazala

Kutumia maneno bila kuzingatia muktadha wa matumizi ya maneno hayo.

Utamkaji wa maneno. Wakati mwingine utata unaweza kujitokeza katika matamshi tu, ili hali katika maandishi utata hauonekani. Kwa mfano; Mimina wewe, katika maandishi linaweza kuandikwa mimi na wewe, na hivyo kuondoa utata.

Mjengo wa maneno. Utata huu huzuka katika vitenzi kama pigia. Chanzo cha utata katika kitenzi hiki ni kiambishi -i-. Kiambishi hiki kinaweza kumaanisha: kwa ajili ya…, kwa sababu ya.., kwa kutumia chombo fulani.., au mahali fulani.

|, ie ya

Alimpigia kiatu (kifaa)

  • Alimpigia ndani (mahali) Mfano 5 Mifano ya utata katika tungo
  • Patience amemwandikia Lilian barua: Sentensi hii huweza kuwa na maana kuwa

Patience ameandika barua kwenda kwa Lilian au Patience ameandika barua kwa niaba ya

| Lilian

Umefanikiwa kununua mbuzi? Sentensi hii huweza kumaanisha ununuzi wa mbuzi

mnyama au mbuzi kifaa cha kukunia nazi.

3. Alimkuta amelala kwenye nyumba ya wageni: Sentensi hii huweza kumaanisha, nyumba ya mtu lakini inatumika kwa ajili ya wageni kwa malipo au ni nyumba

| inayomilikiwa na watu ambao ni wageni katika eneo lile.

4. Attu ametumwa na Aritamba: Sentensi hii inaweza kueleweka kumaanisha, Aritamba

amemtuma Attu au Attu na Aritamba wametumwa wote kwa pamoja

Maelezo Ya Ziada

MATUMIZI YA LUGHA KATIKA MIKTADHA

MBALIMBALI Matumizi ya lugha ni namna ya kutumia lugha, mila, desturi na taratibu za jamii. Ni ambavyo mzungumzaji anatumia lugha yake kuhusiana na msikilizaji.

Hivyo lugha hutegemea

(a) Uhusiano wa wazungumzaji

(b) Mada inayozungumzwa

(c) Mazingira

(d) Dhumuni la mazungumzo

Miktadha

Ni mazingira au hali ambamo tukio hutendeka.

Au

Miktadha ni mazingira ya neno katika tungo au sentensi yenye kuzingatia uhusiano wake na maneno mengine.

Umuhimu Wa Matumizi Ya Lugha

(i) Kumsaidia mwanafunzi na msomaji wa kawaida kutumia Kiswahili kwa ufasaha.

(ii) Kumsaidia mwanafunzi na msomaji wa kawaida kutofautisha na kutumia mitindo mbalimbali ya Kiswahili

Matumizi ya lugha hutawaliwa na mambo yafuatayo

(i) MAZINGIRA

Msomaji wa lugha yoyote ile anakuwa katika mazingira yanayomtawala kimaisha, mazingira hayo ndiyo yanayomuamulia kuhusu vitendo na hata mazungumzo yake kutokana na mazingira tunapata

– Lugha ya hotelini

– Lugha ya ofisini

– Lugha ya mtaani

– Lugha ya kanisani.

(ii) UHUSIANO BAINA YA WAHUSIKA

Uhusiano baina ya wahusika nao unaathiri uzungumzaji wa lugha hapa mazungumzo au lugha itakayotumiwa itategemea unayeongea naye. Kutokana na uhusiano wa wahusika tunapata

– Lugha ya baba na mama

– Lugha ya watu wa rika moja

– Lugha ya mwalimu na mwanafunzi wa chini yake

– Lugha kati ya mtu na mpenzi wake.

Hapo baba ataongea lugha ya kuamuru na mtoto atajibu kwa unyenyekevu na hivyohivyo kwa mwalimu na mwanafunzi wake, bosi na mfanyakazi wake.

Lugha ya watu wa rika moja wanazungumza lugha ambayo wenyewe wanaelewa na siyo rahisi mtu wa rika nyingine kuelewa lugha hiyo.

“Big tunasikia unamic skonga siku hizi”

”Ah si Yule ticha mnoko…. eti kanipakazia ni mchapa daftari wa shule”

“Maticha wetu wanapanga wanipe kibano lakini nikawatoka mie nduki”

“Chekini washkaji, dingi angeniona si ingekuwa so!”

“ngoja niwape siri, nina mishemishe baby ya kuwapa kichapo wale maticha zenu mi nasepa”

“poa mwana”

(iii) MADA YA MAZUNGUMZO

Kimsingi mada ya mazungumzo hutawala usemaji na jinsi ya uzungumzaji kwa ujumla. Kutokana na mada ya mazungumzo tunapata lugha ya

  • Biashara
  • Kitaaluma
  • Mahubiri
  • Kisiasa

• Kisheria n.k

Juma : Nakusikiliza jaribio la kutaka kupindua serikali litakuwa la namna gani katika sheria za Kenya?

Ali : Ni kosa la uhariri

(iv) MADHUMUNI YA MAZUNGUMZO

Hapo mzungumzaji hutoa ufafanuzi wa yale anayotaka kusema

Hivyo ufafanuzi huo utategemea

  • Mazingira
  • Uhusiano baina ya wahusika
  • Mada ya mazungumzo

Mhadhara/ mazungumzo ya kiuchumi nchini Tanzania yanatofautiana na mhadhara/ mahubiri kanisani.

(v) JINSI YA MAZUNGUMZO

Namna mawasiliano yanavyofanywa kwa maandishi au mazungumzo utaathiri jinsi au mtindo wa uzungumzaji

Kama mfanyabiashara lazima atapamba uzungumzaji wake kwa kuwavutia wateja

“Mpambe mwanao kwa mia mbili, na mpambe mkeo kwa mia tano”

(A)Rejesta

Ni mtindo wa lugha inayotumika mahali penye shughuli Fulani ambayo ni tofauti na lugha ya kawaida

Aina Za Rejesta

(i) Lugha ya mitaani/ kijiweni

Haya ni mazungumzo yanayozungumzwa magengeni au katika makundi ya vijana wa rika fulani nayo hueleweka na wazungumzaji wenyewe. Ni lugha ambayo huchipuka kutokana na kikundi cha watu ambacho ni kidogo. Lugha hii hudumu kwa muda mfupi tu halafu hujifia.

Mfano wa maneno yanayosikika mitaani ni kama vile:

– Mshkaji / mtu wangu, mwana wangu besti, (rafiki)

– Demu (msichana)

– Nipe mkwanja( nipe pesa)

– Mzuka (safi, poa)

– Nasepa (naondoka)

– Kitaa (mtaa)

– Skonga (shule)

Kwa ujumla lugha hii siyo sanifu, ni lugha iliyojaa maneno ya mtaani ambayo yanazushwa tu na kundi fulani la wazungumzaji.

(ii) Rejesta ya mahali kwenye shughuli maalumu

Rejesta za namna hii hazifanywi kiholela, bali hufuata taratibu, sheria na kanuni maalum zinazojitokeza katika mazingira haya, mazungumzo ya kwenye shughuli maalumu ni kama vile ya

– Maofisini na mahali popote pa kazi

• Mazungumzo ya hotelini yana utaratibu wake ambao katika mfano

A : Nani wali kuku?

A: Supu mkia wapi

Katika mazungumzo hayo “A” anapouliza “nani wali kuku” ana maana kuwa nani anahitaji kula wali na nyama ya kuku. Na wala hakuna maana kuwa mtu anayeitwa.”walikuku “ au “supu mkia”)

(iii) Rejesta zinazohusu watu

Haya mawasiliano yasiyo rasmi huwa ni yale maongezi ya kawaida ya kila siku au mazungumzo rasmi.

Mfano: mazungumzo kati ya

– Vijana wa rika moja

– Mwalimu na mwanafunzi wake

– Wazee wenyewe

– Bosi/ meneja na mfanyakazi wake

(iv) Lugha ya kitarafa

Hiki ni Kiswahili cha tarafa ukikisema katika tarafa nyingine huwa ni vigumu watu wa sehemu hiyo kuelewa anasema nini kwa ujumla ni Kiswahili ambacho kimeathiriwa na vilugha /lugha mama

Kiswahili cha kiyao- John amenitona (John amenifanya)

Kiswahili cha kiha – Nitakusina (nitakupiga)

Kiswahili cha Kimakonde-Achante chana (asante sana)

Kiswahili cha kihehe – huwaga (huwa)

(v) Kiswahili rasmi/ sanifu

Ni mawasiliano kutokana na vilugha vya lugha ya Kiswahili.

Kiswahili hiki hukubaliwa na wengi katika nchi na ndicho kinachotumika katika shughuli mbalimbali za nchi na vyombo vya habari.

Dhima (Matumizi) Ya Rejesta

1. Rejesta hutumika kama kitambulisho yaani hutofautisha mtindo wa lugha miongoni mwa wazungumzaji kuwa wao ni kundi fulani.

Rejesta ya watunzi inawatambulisha wao kuwa ni tofauti na ya wavuvi ambao pia wao wana rejesta yao.

Rejesta ya kanisani /msikitini ni tofauti na rejesta ya jeshini n.k

2. Rejesta hupunguza ukali wa maneno. Rejesta inapotumiwa na kundi la watu huficha jambo hilo linalozungumzwa lisieleweke kwa wengi. Hivyo hadhira inapuuzwa kwa sababu sio watu wengi wanaoelewa.

  1. Rejesta hutumika ili kurahisisha mawasiliano au kupunguza au kuokoa muda wa kuwashughulikia watu au wateja wengi, kwa mfano anayegawa dawa hospitalini anaposema “mbili asubuhi, mchana na jioni) au “kutwa mara tatu” akiwa na maana kwamba mgonjwa anywe vidonge viwili asubuhi, viwili mchana na viwili jioni. Hapa amefupisha ili aweze kuwahudumia kwa muda mfupi wagonjwa wengine wanaosubiri kupewa dawa.
  2. Rejesta hupamba lugha miongoni mwa wazungumzaji kwa mfano rejesta ya hotelini

Mhudumu – nani supu mkia

Mteja – mimi hapa

Mhudumu – wapi wali ng’ombe

Mteja – hapa

Mazungumzo haya kati ya mhudumu na mteja licha ya kuokoa au kurahisisha mawasiliano, vilevile yanapamba mazungumzo haya.

5. Rejesta huweza kuwa kiungo cha ukuzaji lugha pale lugha inapohusika inapoweza kuunda msamiati wake.

Mambo Yanayosababisha Kutokea Kwa Rejesta

1. Ubinafsi

Yaani tabia aliyonayo mtu ya muda wa kudumu kila mtu ana namna ya kuzungumza ambapo humtofautisha na watu wengine hali hii huleta ubinafsi katika sauti yake (matamshi) na mwisho huleta mtindo wa pekee ambao ni tofauti na wengine.

2. Mwingiliano

Makundi ya watu mbalimbali yanapochangamana husababisha mwingiliano miongoni mwao na ili kuweza kutofautisha kundi moja na kundi jingine kuna mambo fulani ambayo hutofautiana miongoni mwa makundi hayo na mambo hayo katika lugha huhusisha matamshi ya maneno, mpangilio wa maneno (sarufi) tofauti hizi husababisha mitindo miwili tofauti miongoni mwa makundi hayo hivyo husababisha kuzuka kwa rejesta.

3. Kupita Kwa Wakati

Kila kipindi kwa mitindo yake katika kila mahali. Na hii ni kutokana na mabadiliko ya kihistoria yanayoikumba jamii fulani kila kipindi cha mpito wa kihistoria huweza kuwa na maneno yake ambayo huwa ni tofauti na kipindi kingine cha kihistoria. Vilevile mitindo ya lugha kutoka kipindi kimoja hadi kingine huweza kuwa tofauti. Hivyo rejesta huweza kutoka kati ya kipindi kimoja na kingine.

Mfano: enzi za ukoloni, uhuru, azimio la Arusha, hali ngumu ya maisha n.k

4. Shughuli Iliyopo

Hapo hutegemeana na mazingira gani ambayo shughuli hiyo inafanyika mfano; msikitini, kanisani, darasani, mahakamani, hotelini, hospitalini, shughuli fulani katika mazingira fulani hutupatia rejesta za mahali.

5. TOFAUTI ZA HADHI ZA WAHUSIKA (Uhusiano wa wahusika)

Mfano; wasomi au wasiosoma, mwajiri/ mwajiriwa, tajiri/ maskini, hali hii kwa ufupi

husababishwa na matabaka yaliyopo katika jamii. Tabaka moja na tabaka jingine hutumia lugha

ambayo huwa ni tofauti miongoni mwao hivyo husababisha rejesta kuzuka miongoni mwa matabaka hayo.

6. Matumizi Ya Uficho Tafsida

Hali hii pia husababisha kuzuka kwa rejesta kwani husababisha mitindo mbalimbali miongoni mwa wazungumzaji mfano: mwanaume mwenye mambo ya kike huitwa shoga, punga, bwabwa n.k.

(B)Misimu / Simo

Misimu/ simo ni maneno yanayosanifu yanayozuka/ zushwa na kikundi cha watu wachache wenye tamaduni moja ili kuelezana mahusiano yao kama kikundi au kuhusu jamii kubwa ambamo vikundi hivyo vinaishi katika kipindi fulani cha muda na hatimaye maneno hayo hupotea na yanayodumu husanifiwa na kuwa msamiati rasmi wa lugha inayohusika.

1. Msimu huzuka kutokana na mabadiliko ya kihistoria yanayoikumba jamii katika nyakati mbalimbali

2. Misimu mingine huzuka hali ya utani miongoni mwa watu mbalimbali. Mara nyingi misimu ya aina hii hubeba kebehi, dhihaka, bezo, dharau au kusifu kuliko kawaida.

Sababu Za Kutumia Misimu

1. Kutaka mazungumzo yawe siri ili yasieleweke kwa watu wengine

Mfano: nafunga ofisi, nasepa

  1. Kudhania ndio ujuzi wa lugha. Hasa kwa vijana walio wengi wakionesha ujana wao. Mfano wanaposema nimewaka au nimechalala ile mbaya au nimefulia.
  2. Kufanya mambo mazito na ya maana kuwa mepesi na ya kawaida mfano mtu anaposema , “kutoa chai” “kula mlungula” – kutoa rushwa/ kula rushwa.

Njia Zitumikazo Kuunda Misimu

(i) Njia ya kufupisha maneno

Neno linaweza kufupishwa makusudi na matokeo yake kuwa ni msimu mfano kwa wanafunzi wa shule za upili katika kidato cha 5 na 6 wana vifupisho vya michepuo yao ya masomo.

Mfano: HKL (Hatusomi Kufaulu Lazima) n.k na chuo kikuu kuna neno DISCO – Mwanafunzi

kutoendelea na masomo

(ii) Lugha za kutohoa lugha za kigeni

Kwa kutumia utohozi tunapata misimu kama

Feg – kiingereza “fag” maana sigara

Demu – kiingereza “Dame” maana msichana

(iii) Njia ya kutumia sitiari

Sitiari ni mlinganisho wa ufanano wa umbo, rangi, kimo, dhima/kazi n.k

Baina ya vitu, misimu mingi huundwa kwa njia hii mfano……

(iv) Njia ya kutumia tunakali

Njia hii inatumika pia katika uundaji wa misimu

Maneno kama vile

– Mataputapu – Pombe ya kienyeji

– Malapa (ndala) – Inatokana na sauti inayosikika wakati mtu atembeapo akiwa amevaa kandambili “lap lap”

(v) Njia ya kubadili maana ya msingi

Njia hii nayo imetumika katika uundaji wa misimu mfano mtu kutumia maneno kama vile kumfia, kumzimikia ina maana kumpenda sana.

  1. Misimu huzuka na kutoweka. Hii ni kutokana na mabadiliko ya kihistoria
  2. Misimu ni lugha isiyo sanifu

Huzushwa na watu kutokana na hisia

  1. Misimu ni lugha ya mafumbo hufahamika na kikundi kidogo cha watu
  2. Misimu ina chumvi/ chuku
  3. Misimu ina maana nyingi
  4. Misimu hupendwa sana na wengi sababu ina mvuto
  5. Misimu huhifadhi historia ya jamii.

Aina Za Misimu

1. Misimu ya pekee

Aina hii ya misimu huelezea mahusiano ya kikundi kimoja kutoka kwenye utamaduni mmoja. Misimu hii hupatikana sehemu moja ya kazi au mahali waishipo watu wa aina moja. Kutokana na jambo hili eneo la matumizi ya misimu ya aina hii huwa ndugu, na kimsingi huibua hisia za aina zote kwa binadamu. Misimu hii huitwa ya kipekee kwa sababu haijulikani nje ya eneo la kuzuka kwake, isipokuwa wale tu ambao wamo katika kikundi hicho, mifano ya watu watumiao misimu ya pekee ni wanafunzi wa shule moja, wafanyakazi wa ofisi ya aina moja, wanamichezo n.k.

2. Misimu ya kitarafa

Aina hii ya misimu huchukua eneo kubwa au pana kidogo kimatumizi inaweza kupatikana kwenye hata tarafa, wilaya, mkoa n.k watu walioko katika kundi hili wana mchanganyiko wa tamaduni, si rahisi kutambua mipaka ya maeneo haya ya kitarafa, lakini kimsingi yanaweza kuwa ya kijiografia, kihistoria au hata kilugha. Kuenea kwa misimu hii inategemea hali au tabia ya kuingiliana kwa watu katika shughuli za maisha ya siku hadi siku, kama vile biashara, michezo n.k, mara nyingi misimu ya kitarafa hutokana na: –

– Vitu vilivyo katika eneo hili

– Lugha itumikayo katika eneo hili

– Uzoefu wa mazingira na uwezo wa lugha ya msanii.

3. Misimu zagao

Aina hii ya misimu huenea nchi nzima au hata kuvuka mipaka ya nchi. Misimu zagao hutumika katika mikoa yote na vilevile hutumika katika magazeti, vitabu na vipindi vya redio na television, misimu inayoshika mizizi bila kufutika.

Katika lugha husanifiwa na kuwa msamiati wa lugha

Mfano: – kabwela, wafurukutwa, wakereketwa, buzi, ukapa, wapambe, ngangari, ng’atuka n.k

Matumizi (Dhima) Za Misimu

(i) Kukuza lugha

(ii) Kupamba lugha

(iii) Kufanya mawasiliano yawe mafupi na yenye kueleweka kwa haraka.

(iv) Kuwa na siri/ hupunguza ukali wa maneno wakati wa mazungumzo ya kawaida

(v) Kuhifadhi historia ya jamii

(vi) Kuibua hisia mbalimbali za wazungumzaji

(vii) Kufurahisha na kuchekesha

(viii) Kukosoa na kuihasa jamii

(ix) Kuunganisha watu na makundi mbalimbali.

Lugha Ya Mazungumzo Na Lugha Ya Maandishi

Maana ya lugha

Lugha ni mfumo wa sauti za nasibu za binadamu zenye mpangilio maalumu wenye kuleta maana zilizokubalika na jamii husika kwa ajili ya mawasiliano.

Mambo ya msingi yanayojenga maana ya lugha

– Lugha ni sauti za nasibu – kwa sababu mwanadamu hazaliwi na lugha bali huikuta katika jamii.

– Lugha ni sauti zenye maana ambazo mtu huzitoa kupitia ala za sauti kama meno, ulimi,mdomo, kaa kaa n.k

– Lugha ni sauti zenye utaratibu maalumu ambazo hufuata utaratibu fulani uliokubaliwa na jamii ya watu fulani.

– Lugha inatawaliwa na maneno ya utamaduni wa watu fulani kwa kuzingatia mila na desturi za maisha ya watu hao.

– Lugha ni sauti za kusemwa kwa sababu lugha ya asili ya mwanadamu ni lugha ya mazungumzo.

– Lugha ni hali ya binadamu tu, wanyama, ndege na wadudu hawana lugha bali wana milio.

– Lugha ni sauti za kueleza wazi ambazo humwezesha mwanadamu kupashana habari au kujuliana hali na mwenzake.

– Lugha ina maana fulani kwa sababu sauti zinapowekwa kwenye mfumo maalumu ndipo zinapokuwa na maana katika lugha hiyo.

Kuna Aina Kuu Mbili Za Lugha

(i) Lugha ya mazungumzo na

(ii) Lugha ya maandishi

• Lugha ya mazungumzo

Hii ni lugha inayotolewa kwa njia ya mazungumzo ya mdomo.

– Lugha hii hukutanisha pande mbili, mzungumzaji na msikilizaji.

– Lugha hii huonesha hali ya mzungumzaji kama ana hasira, huzuni, furaha.

– Mzungumzaji inabidi aitumie hii lugha fasaha na sarufi na mpango mzuri wa mawazo, uwazi na ukweli katika maelezo yake ili aweze kueleweka kwa msikilizaji wake.

– Msikilizaji nae anatakiwa awe mtulivu na msikivu ili kufahamu yanayozungumzwa aweze kufasiri kupima yale aliyoyasikia kwa uzoefu wake wa siku zote.

Sifa Za Lugha Ya Mazungumzo

(i) Ina msemaji na msikilizaji. Hii ikiwa na maana kuwa msemaji ndiye chanzo cha mazungumzo na msikilizaji ndiye kikomo.

(ii) Huwakutanisha ana kwa ana msemaji na msikilizaji.

(iii) Hubadilika badilika kutegemeana na mazingira ambayo mtu anaongea pamoja na watu. Hii huibua mitindo mbalimbali ya utumizi wa lugha.

(iv) Huonesha hali ya mzungumzaji mfano, hasira, chuki n.k

(v) Huwasilishwa kuzungumzwa kwa sauti.

(vi) Mzungumzaji hutakiwa azingatie ufasaha na usanifu wa lugha, mpangilio mzuri wa mawazo, uwazi na ukweli katika maelezo yake ili aeleweke.

• Lugha ya maandishi

Ni lugha ambayo huwasilishwa kwa njia ya maandishi

– Ni kiwakilishi cha lugha ya mazungumzo

– Lugha hii ni uwezo wa mtu binafsi kutoa mawazo yake na kuyaweka katika maandishi.

– Lugha ya maandishi humlazimu mwandishi atumie muda mrefu kwa sababu huitaji kufikiri kabla ya kuandika pia mwandishi azingatie kanuni na taratibu za uandishi ili kutoa maneno na sentensi sahihi.

Sifa Za Lugha Ya Maandishi

(i) Mwandishi na msomaji, mwandishi chanzo na msomaji kikomo.;

(ii) Nyenzo kubwa ya uwasilishwaji wake ni maandishi.

(iii) Haibadiliki badiliki – ikishaandikwa hubaki vilevile hata kama ni makosa

(iv) Huitaji kufikiri kwa makini kabla ya kutoa. Hivyo ina maadili ambayo mwandishi hufanya ili afanikiwe zoezi lake.

(v) Hudumu kwa muda mrefu kama kumbukumbu baada ya kuandikiwa.

TOFAUTI BAINA YA LUGHA YA KIMAZUNGUMZO NA LUGHA YA

KIMAANDISHI

• Uwasilishaji

Lugha ya kimazungumzo huwasilishwa kwa njia ya mazungumzo au masimulizi, lakini lugha ya kimaandishi huwailishwa kwa maandishi

• Mabadiliko

Mara nyingi sana lugha ya mazungumzo hubadilika kutokana na mazingira, wahusika, mada, wakati na madhumuni yake. Lugha ya kimaandishi haibadiliki pindi tu ikishaandikwa hata kama ilikuwa na makosa.

• Uhusiano na hadhira

Lugha ya mazungumzo huwakutanisha ana kwa ana, mzungumzaji na msikilizaji, lakini lugha ya kimaandishi haiwakutanishi ana kwa ana mwandishi na msomaji.

• Maandalizi

Lugha ya mazungumzo haihitaji maandalizi makubwa ya mada, lakini lugha ya maandishi ili kutafakari mambo yatakayoandikwa na huandaa vifaa kama vile peni, rula, karatasi n.k

• Uhifadhi

Lugha ya kimazungumzo huhifadhiwa kwa kichwa hivyo si rahisi kukumbukwa kwa muda mrefu, lakini lugha ya kimaandishi huhifadhiwa kwenye vitabu na majarida ambapo hudumu kwa muda mrefu.

• Gharama

Lugha ya kimazungumzo haihitaji gharama nje ya ala za sauti ili kuwezesha kutamka maneno vizuri.

Lugha ya kimaandishi ina gharama kubwa kwa sababu huhitaji vifaa vya kuandikia kama karatasi, kalamu na vifaa vingine ili iandikwe kwa ukamilifu na muda.

• Wahusika

Lugha ya mazungumzo ina utajiri wa wahusika. Ni lugha ya kila mtu ajifunzayo toka utotoni, hivyo wazungumzaji ni wengi.

Lugha ya kimaandishi wahusika ni wachache kwani ni wale tu wawezao kusoma na kuandika.

• Uhai

Lugha ya kimazunguzo ina uhai kwani kuonesha ujumbe pamoja nakuelezea hali ya mzungumzaji kama ana hasira, chuki, furaha n.k

Lugha ya kimaandishi ni vigumu kuonesha na kuelewa wazi hali ya mwandishi.

(Dhima Ya Lugha Kiujumla)

– Lugha ni chombo cha lazima na muhimu katika mawasiliano ya binadamu yaani hutumika katika kupashana habari.

– Lugha ni chombo muhumu katika kufundishia elimu kuanzia ngazi za chini hadi ya juu.

– Lugha ni chombo muhimu katika kuleta maendeleo kwa sababu hutumika katika kuhimiza shughuli za maendeleo ya jamii.

– Lugha ni alama ya utambulisho ambayo hutumika kutambulisha jamii juu ya taarifa fulani, watu fulani au kabila fulani.

– Lugha ni chombo muhimu katika kuleta maelewano na upatanisho miongoni mwa wanajamii.

– Lugha ni chombo muhimu katika kutunza kumbukumbu za jamii husika.

Makosa Ya Kisarufi Na Kimantiki

Lugha inapotumika vibaya hupoteza lengo na madhumuni ya mzungumzaji kwa msikilizaji wake. Upotoshaji huu unaweza kujitosheleza katika sarufi au mantiki.

1. Makosa ya kisarufi

Makosa ya kisarufi hujumuisha makosa ya kimsamiati, kimuundo, kimaana na kimatamshi. Vipengele hivi vikitumiwa vibaya basi makosa hayo ni msamiati.

Miundo ya sentensi, upatanisho wa kisarufi na matamshi

(a) Kosa la msamiati

Baadhi ya watu huchanganya msamiati wakati wa kuzungumza. Hali hii husababisha kosa la kimsamiati mfano mtu huchanganya neno mazingira na mazingara kwa kudhani maneno yote yana maana sawa.

(b) Kosa la miundo ya sentensi

Vilevile makosa ya miundo ya sentensi hujitokeza kwa sababu ya kukiuka miundo ya sentensi ya Kiswahili.

Mtu akisema Simba aliuwawa na mwindaji, hapa msikilizaji anaweza akapata maana mbili.

(i) Msikilizaji anaweza kuelewa mwindaji alimwua simba au simba pamoja na mwindaji walikufa wote.

(ii) Nilimpikia uji bibi.

Maana – Alifanya tendo la kupika uji kwa ajili ya bibi

Alipika uji badala ya bibi

(c) Kosa la upatanisho wa kisarufi

Makosa ya upatanisho wa kisarufi pia huathiri sana lugha kati ya mzungumzaji na msikilizaji, kwa kawaida katika Kiswahili nomino mtenda ndiyo inayotawala upatanisho wa kisarufi kwenye kivumishi na kitenzi mfano mtu anaweza kukosea na kutamka

(i) Mtoto mdogo analia

Watoto wadogo wanalia

Mtoto wanacheza mpira

Mtoto anacheza mpira

(d) Kosa la kimatamshi

Makosa ya kimatamshi nayo ni sehemu ya makosa ya kisarufi watu wengine hushindwa kutamka baadhi ya maneno (sauti) ya lugha ya kishwahili sanifu.

(a) Kura na kurara je? – Kula na kulala je?

(b) Msichana mhodari – Msichana hodari

(c) Selasini na thaba – Thelathini na saba

(d) Achante sana – Ahsante sana

(e) Ng’ombe wako ngambo ya mto

– Ng’ombe wako ng’ambo ya mto

2. Makosa ya kimantiki

Mantiki ni mtiririko wa fikra zilizopangwa ili kujenga hoja yenye kukubalika. Kosa la kimarufuku ni hali ya kukosa utaratibu mzuri wa kufikiri hasa wakati wa kuzungumza na kuandikwa

Mara nyingi tatizo hili hutokea kwa sababu ya upotofu wa mawazo ya mzungumzaji.

(a) Nyumba imeingia nyoka

Nyoka ameingia kwenye nyumba

(b) Jicho limeingia mdudu

Mdudu ameingia jichoni

(c) Chai imeingia nzi

Nzi ameingia kwenye chai

(d) Mfupa hauna ulimi

Ulimi hauna mfupa

– Kusahihisha makosa

Makosa ya kawaida yataendelea kuwepo katika lugha yoyote ile kama vile Kiswahili kwa hiyo hatuna budi kujitahidi kuzuia makosa hayo.

Inatubidi kuhakikisha makosa ya kisarufi na kimantiki katika msamiati, matamshi, muundo na maana hayajitokezi kwenye mazungumzo, barua, shuleni na kwenye vyombo vya habari kama vile redio, televisheni na magazeti

Vilevile jitihada za marekebisho ya kisarufi na kimantiki sharti zitiliwe maanani tangu kiwango cha elimu ya msingi, sekondari na vyuoni hadi vyuo vikuu.

Mara nyingi makosa ya kimsamiati husababishwa na vyombo vya habari kwa hiyo ni muhimu somo la utumizi wa lugha ya Kiswahili lizingatiwe sana katika vyombo vya habari ili kuepusha upotoshaji wa jamii.

Kwahiyo kamusi ni kitabu muhimu sana kwa sababu huwa na orodha ya maneno tofauti yanayotumiwa na wazungumzaji na maana zake.

-Makosa ya kisarufi

Ni ukiukaji wa kanuni, sheria na taratibu za lugha kimatamshi, kimsamiati kimuundo na kimaana.

-Makosa ya kimantiki

Ni hali ya kukosa utaratibu mzuri wa kufikiri hasa wakati wa kuzungumza au kuandika

Kufanana kwa lugha ya mazungumzo na lugha ya maandishi

(a) Lugha zote hutumika katika kufanya mawasiliano na kupashana habari.

(b) Lugha zote ni mali ya mwanadamu mwenyewe

(c) Lugha zote huwa na mada inayozungumziwa au kuandikwa ili kueleweka vizuri kwa msikilizaji au msomaji inabidi kuwe na mpangilio mzuri wa mada na mtiririko mzuri wa mawazo.

(d) Lugha zote zina chanzo na kikomo, chanzo cha lugha ya maandishi ni mwandishi na lugha ya mazungumzo ni mzungumzaji na kikomo ni msomaji na msikilizaji.

(e) Vilevile lugha zote hutumika katika kuhimiza shughuli zote za maendeleo ya jamii kwa sababu huleta maendeleo, amani na mshikamano kwa jamii husika.

Lugha ya Kiswahili na mfumo wake wa matamshi. Matamshi na lafudhi ya Kiswahili imeathiriwa sana na lugha nyingine za kibantu kwa watanzania wengi, Kiswahili ni lugha ya pili, lugha ya kwanza ni ya makabila kama vile:

Kisukuma, kinyamwezi, kiluguru, kiha, kichaga, kihaya n.k

Kiswahili kina lafudhi yake ya matamshi sahihi ya kutamka , mara nyingi huathiriwa na lugha mama

– Ni matamshi ya mzungumzaji yanayotokana na lugha yake (lugha mama) ya mwanzo au lugha ya zinazozunguka.

Matamshi

– Ni kitendo cha kutoa nje ya kinywa au pua ya mwanadamu sauti ambazo hutumika katika mazungumzo au usemi wowote.

Kosa sahihi

Ch sh

Chabiki shabiki

Changa shanga

Mchenga mshenga

-g- -gh-

Garama gharama

Magaribi magharibi

Buguza bughuza

-f- -v-

Futa vuta

Fita vita

Faa vaa

-L- -r-

Lika rika

Fahali fahari

Hawala hawara

-ng- ng’

Ngombe Ng’ombe

Ngara Ng’ara

Mngao Mng’ao

Nt nd

Ntani ndani

Ntungu ndugu

Ky ch

Kyai chai

Kyama chama

K g

Kari gari

Kama gama

S z

Saa zaa

Kasa kaza

Z j

Zana jana

Zua jua

Z au s th

Zamani thamani

Selasini thelathini

Matamshi na lafudhi ya Kiswahili huweza kuathiri hata sentensi ya Kiswahili mfano sentensi hizi hazina lafudhi na matamshi sahihi ya Kiswahili.

(a) Kyai kya moto kimeletwa na mpishi

Chai ya moto imeletwa na mpishi

(b) Ngombe watarejea zizini magaribi

Ng’ombe watarejea zizini magharibi

(c) Kuathiriwa kwa lafudhi na matamshi sahihi ya Kiswahili huweza kutokana na

(a) Athari za lugha mama. Mfano mpare hutumia th badala ya s

Thatha – sasa

Thithi – sisi

Thote – sote

Mfano: Thithi thote tunywe thupu

Sisi sote tunywe supu

(b) Mzungumzaji kuwa na kithembe

Thamba – shamba

Dithemba – disemba

Thema – sema

(c) Maumbile / ukosefu wa ala fulani za sauti

– Mtu asiye na meno hushindwa kusema ala zinazotamkwa kwenye meno mfano:

Dhahabu – zahabu

Dhambi – zambi

(d) Kutumia neno bila kuzingatia mazingira au muktadha unaohusika na utumizi wa maneno hayo

Utata Katika Mawasiliano

Mawasiliano ni mchakato wa upashaji na ubadilishaji wa habari kwa njia mbalimbali.

Mara nyingi utata wa lugha ya Kiswahili huweza kujitokeza katika tungo neno au tungo sentensi.

Sababu za utata

(a) Uwezo wa neno moja kuwa na maana zaidi ya moja mfano mbuzi.

(b) Kutozingatia taratibu za uandishi

1. Tulimkuta Juma na rafiki yake, Abdi

Continue Studying Form Two

Get the Complete PDF Notes

Would you like these notes in a well-formatted PDF for easier reading and offline study? Click below to ask for the complete PDF notes.

GET WELL-FORMATTED PDF NOTES

View More Secondary School Notes

Scroll to Top
Changia Notes / Document