Skip to main content

Tenzi za Rohoni

Tenzi za Rohoni

Tenzi za Rohoni 25 – Nimekombolewa na Yesu

Tenzi za Rohoni 25 – Nimekombolewa na Yesu Tenzi Na. 25 Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 25, “Nimekombolewa na Yesu”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza. Maneno ya Wimbo Nimekombolewa na Yesu Aliyenirehemia; Kwa bei ya mauti yake Nimekuwa mtoto wake. Kombolewa! Nakombolewa na damu; Kombolewa! Mimi mwana wake kweli. Kukombolewa nafurahi, Kupita lugha kutamka; Kulionyesha pendo lake, Nimekuwa mtoto wake. Nitamwona uzuri wake, Mfalme wangu wa ajabu; Na sasa najifurahisha, Katika neema yake. Najua taji imewekwa Mbinguni tayari kwangu; Muda kitambo atakuja, Ili alipo, niwepo. ← Tenzi 24 | Tenzi Zote | Tenzi 26 → Tazama Tenzi za Rohoni 1–164 Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

Tenzi za Rohoni

Tenzi za Rohoni 24 – Mwokozi Moyoni Mwangu

Tenzi za Rohoni 24 – Mwokozi Moyoni Mwangu Tenzi Na. 24 Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 24, “Mwokozi Moyoni Mwangu”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza. Maneno ya Wimbo Tangu siku hiyo aliponijia, Akae moyoni mwangu, Sina giza tena, ila mwanga pia Kwa Yesu mwokozi wangu. Amani moyoni mwangu, kwa Yesu, Mwokozi wangu; Sina shaka kamwe, Kwa sababu yeye, Yu nami moyoni mwangu. Sina haja tena, ya kutanga-tanga, Ndiye kiongozi wangu. Dhambi zangu zote zimeondolewa, Na Yesu, Mwanawe Mungu. Matumaini yangu ni ya hakika, Katika Mwokozi wangu. Hofu zangu na hamu zimeondoka, kwa kuwa ninaye Yesu. Siogopi tena, nikiitwa kufa, Yu nami daima, Yesu. Mlango wa Mbinguni ni yeye pia, “Tapita humo kwa damu.” Nitaketi na yeye huko milele, Nisifu Mwokozi wangu. Nina raha moyoni majira yote, Kwa Yesu, Mwanawe Mungu. ← Tenzi 23 | Tenzi Zote | Tenzi 25 → Tazama Tenzi za Rohoni 1–164 Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

Tenzi za Rohoni

Tenzi za Rohoni 23 – Ni Salama Rohoni Mwangu

Tenzi za Rohoni 23 – Ni Salama Rohoni Mwangu Tenzi Na. 23 Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 23, “Ni Salama Rohoni Mwangu”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza. Maneno ya Wimbo Nionapo amani kama shwari, Ama nionapo shida; Kwa mambo yote umenijulisha, Ni salama rohoni mwangu. Salama rohoni, Ni salama rohoni mwangu. Ingawa shetani atanitesa, Nitajipa moyo kwani Kristo ameona unyonge wangu, Amekufa kwa roho yangu. Dhambi zangu zote, wala si nusu, Zimewekwa msalabani; Wala sichukui laana yake, Ni salama rohoni mwangu. Ee Bwana himiza siku ya kuja, Panda itakapolia; Utakaposhuka sitaogopa Ni salama rohoni mwangu. ← Tenzi 22 | Tenzi Zote | Tenzi 24 → Tazama Tenzi za Rohoni 1–164 Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

Tenzi za Rohoni

Tenzi za Rohoni 22 – Kale nilitembea

Tenzi za Rohoni 22 – Kale nilitembea Tenzi Na. 22 Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 22, “Kale nilitembea”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza. Maneno ya Wimbo Kale nilitembea Nikilemewa dhambi Nilikosa msaada, kuniponya mateso. Usifiwe Msalaba! Lisifiwe kaburi! Linalozidi yote, Asifiwe Mwokozi! Hata nilipofika, Mahali pa Msalaba, Palinifaa sana, Sitasahau kamwe. Hicho ndicho chanzo, Cha kufurahi kwangu. Hapo ndipo mzigo, Uliponituliwa. Panapo msalaba, Kinatolewa cheti, Cha kuingia Mbinguni, Kisicho cha kanisa. Yule Bwana mjinga, Likwenda bila cheti, Kitumai kwingia, Kama walio nacho. Lipofika langoni, Akaulizwa cheti, Cha kumwonyesha Bwana, Akakutwa hanacho. Lituhuzunishalo, Ni ninyi msio nacho, Kuwa kama mjinga, Kwa siku ya arusi! Ubavuni mwa Yesu, Mlitokea damu, Chemchemi ya uzima, Itakasayo roho. Jitahidi wingie, Damuni mwa Mwokozi, Utafutiwa dhambi, Toka rohoni mwako ← Tenzi 21 | Tenzi Zote | Tenzi 23 → Tazama Tenzi za Rohoni 1–164 Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

Tenzi za Rohoni

Tenzi za Rohoni 21 – Roho Yangu Hima

Tenzi za Rohoni 21 – Roho Yangu Hima Tenzi Na. 21 Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 21, “Roho Yangu Hima”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza. Maneno ya Wimbo Roho yangu hima, na taa yako Kaiwashe vyema, hapa si pako; Nguvu zote pia za duniani Hazitakudhuru ukiamini. Yesu yuko mbele, Yesu yu nyuma, Yesu vivyo kando, walindwa vyema. Adui shetani, na nguvu zake, Bwana ameshinda, kwa kifo chake; Wewe nguvu huna, huna kabisa, Ndiwe mpungufu, mnyonge hasa. Toka na mapema, mbele ya wote, Omba, bisha sana, maisha yote; Vita vikaliko, macho ukae, Jivike silaha, nawe sishindwe. Bwana Yesu ndiye kwako mchunga, Neno lake Bwana ndilo upanga; Mbingu zitakwisha, na nchi pia, Neno lake Bwana laendelea. ← Tenzi 20 | Tenzi Zote | Tenzi 22 → Tazama Tenzi za Rohoni 1–164 Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

Tenzi za Rohoni

Tenzi za Rohoni 20 – Ninaye Rafiki naye

Tenzi za Rohoni 20 – Ninaye Rafiki naye Tenzi Na. 20 Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 20, “Ninaye Rafiki naye”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza. Maneno ya Wimbo Ninaye Rafiki naye Alinipenda mbele; Kwa kamba za pendo zake Nimefungwa milele; Aukaza moyo wangu, Uache mageule, Mimi wake, yeye wangu; Ndimi naye milele. Ninaye rafiki ndiye Aliyenifilia; Alimwaga damu yake Kwa watu wote pia; Sina kitu mimi tena, Nikiwa navyo tele; Pia vyote ni amana Ndimi wake milele. Ninaye rafiki naye Uwezo amepewa; Atanilinda mwenyewe, Juu tachukuliwa; Nikitazama Mbinguni, Hupata nguvu tele; Sasa natumika chini, Kisha juu milele. Ninaye rafiki naye, Anao moyo mwema; Ni mwalimu, kiongozi, Mlinzi wa daima; Ni nani wa kunitenga Na mapenzi ya mbele? Kwake nimetia nanga, Ndimi wake milele. ← Tenzi 19 | Tenzi Zote | Tenzi 21 → Tazama Tenzi za Rohoni 1–164 Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

Tenzi za Rohoni

Tenzi za Rohoni 19 – Ndiyo dhamana, Yesu wangu

Tenzi za Rohoni 19 – Ndiyo dhamana, Yesu wangu Tenzi Na. 19 Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 19, “Ndiyo dhamana, Yesu wangu”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza. Maneno ya Wimbo Ndiyo dhamana, Yesu wangu; Hunipa furaha za Mbingu; Mrithi wa wokovu wake Nimezawa kwa Roho yake. Habari njema, raha yangu Yesu ndiye Mwokozi wangu, Habari njema, raha yangu Yesu ndiye mwokozi wangu. Kumsalimu moyo wangu, Mara namwona raha yangu; Aniletea malaika, Wananilinda, taokoka. Sina Kinyume, nashukuru, Mchana kutwa huja kwangu; Usiku kucha kuna nuru; Mwokozi wangu; ndimi huru. Hali na mali anitwaa! Mara namwona anifaa, Nami nangoja kwa subira; Akiniita, nije mara. ← Tenzi 18 | Tenzi Zote | Tenzi 20 → Tazama Tenzi za Rohoni 1–164 Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

Tenzi za Rohoni

Tenzi za Rohoni 18 – Akifa Yesu nikafa naye

Tenzi za Rohoni 18 – Akifa Yesu nikafa naye Tenzi Na. 18 Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 18, “Akifa Yesu nikafa naye”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza. Maneno ya Wimbo Akifa Yesu nikafa naye Uzima upya huishi naye; Humtazama mpaka nje: Nyakati zote ni wake yeye. Nyakati zote nimo pendoni, Nyakati zote ni uzimani, Humtazama hata atokee, Nyakati zote mimi ni wake. Vita sipigi visivyo haki, Na Bwana wangu hapiganiki; Beramu yake haitwaliki, Napo po pote hila sitaki. Sina mashaka, akawa mbali; Mizigo yote aihimili; Ananituliza Imanweli, Nyakati zote mimi husali. Sina huzuni na mimi sidhii; Simwagi chozi, wala siguni; Sikuti afa, ila kitini Daima hunifikiri mimi. Kila unyonge huusikia; Kila ugonjwa kwake hupoa; Yesu ni mwenye kuniokoa Nyakati zote hunijalia. ← Tenzi 17 | Tenzi Zote | Tenzi 19 → Tazama Tenzi za Rohoni 1–164 Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

Tenzi za Rohoni

Tenzi za Rohoni 17 – Namwadama Bwana

Tenzi za Rohoni 17 – Namwadama Bwana Tenzi Na. 17 Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 17, “Namwadama Bwana”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza. Maneno ya Wimbo Namwadama Bwana kwa alilonena Njia yangu huning’azia; Nikimridhisha atanidumisha Taamini nitii pia. Amini utii, njia pweke ni hii Ya furaha kwa Yesu: amini ukatii. Giza sina kwangu wala hata wingu Yeye mara huviondoa Woga, wasiwasi, sononeko, basi; Huamini nitii pia. Masumbuko yote, sikitiko lote; Kwa mapenzi hunilipia; Baa, dhara, dhiki, vivyo hubariki Taamini nitii pia. Mimi sitajua raha sawasawa Ila yote Yesu kumpa; Napata fadhili na radhi kamili, Taamini nitii pia. Nitamfurahia na kumtumaini, Majumbani na njia-njia; Agizo natenda, nikitumwa hwenda, Huamini nitii pia. ← Tenzi 16 | Tenzi Zote | Tenzi 18 → Tazama Tenzi za Rohoni 1–164 Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

Tenzi za Rohoni

Tenzi za Rohoni 16 – Kumtegemea Mwokozi

Tenzi za Rohoni 16 – Kumtegemea Mwokozi Tenzi Na. 16 Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 16, “Kumtegemea Mwokozi”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza. Maneno ya Wimbo Kumtegemea Mwokozi, Kwangu tamu kabisa; Kukubali neno lake Nina raha moyoni. Yesu,Yesu namwamini, Nimemwona thabiti; Yesu,Yesu,yu thamani, Ahadi zake kweli. Kumtegemea Mwokozi, Kwangu tamu kabisa, Kuamini damu yake Nimeoshwa kamili. Kumtegemea Mwokozi, Kwangu tamu kabisa, Kwake daima napata Uzima na amani. Nafurahi kwa sababu Nimekutegemea; Yesu,Mpendwa na Rafiki Uwe nami dawamu. ← Tenzi 15 | Tenzi Zote | Tenzi 17 → Tazama Tenzi za Rohoni 1–164 Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

banner
Scroll to Top