Skip to main content

Author name: contact@devinevisiontech.com

Tenzi za Rohoni

Tenzi za Rohoni 15 – Chakutumaini Sina

Tenzi za Rohoni 15 – Chakutumaini Sina Tenzi Na. 15 Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 15, “Chakutumaini Sina”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza. Maneno ya Wimbo Ila damu yake Bwana, Sina wema wa kutosha Dhambi zangu kuziosha; Kwake Yesu nasimma, Ndiye mwamba: ni salama Ndiye mwamba: ni salama. Njia yangu iwe ndefu Yeye hunipa wokovu; Mawimbi yakinipiga Nguvu zake ndiyo nanga. Damu yake na sadaka Nategemea daima, Yote chini yakiisha Mwokozi atanitosha. Nikiitwa hukumuni, Rohoni nina amani Nikivikwa haki yake Sina hofu mbele zake. ← Tenzi 14 | Tenzi Zote | Tenzi 16 → Tazama Tenzi za Rohoni 1–164 Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

Tenzi za Rohoni

Tenzi za Rohoni 14 – Yesu kwa imani

Tenzi za Rohoni 14 – Yesu kwa imani Tenzi Na. 14 Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 14, “Yesu kwa imani”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza. Maneno ya Wimbo Yesu kwa imani, Nakutumaini, Peke yako; Nisikie sasa, Na kunitakasa, Ni wako kabisa Tangu leo. Nipe nguvu pia Za kusaidia Moyo wangu; Ulikufa wewe, Wokovu nipewe Nakupenda wewe, Bwana wangu. Hapa nazunguka Katika mashaka, Na matata; Palipo na giza Utaniongoza Hivi nitaweza Kufuata. Takuwa mzima Nivushe salama Mautini; Sina hofu kamwe Ukiwapo name Nami nikwandame Siku zote. ← Tenzi 13 | Tenzi Zote | Tenzi 15 → Tazama Tenzi za Rohoni 1–164 Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

Tenzi za Rohoni

Tenzi za Rohoni 13 – Tafuta daima utakatifu

Tenzi za Rohoni 13 – Tafuta daima utakatifu Tenzi Na. 13 Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 13, “Tafuta daima utakatifu”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza. Maneno ya Wimbo Tafuta daima utakatifu; Fanya urafiki na Wakristo tu; Nena siku zotena Bwana wako, Baraka uombe kwa kila jambo. Tafuta daima utakatifu; Uwe peke yako ukimwabudu; Ukimwangalia mwokozi wako, Utabadilishwa kama alivyo. Tafuta daima utakatifu; Kiongozi wako aew Yesu tu; Katika furaha au huzuni Dumu kumfuata Yesu Mwokozi. Tafuta daima utakatifu; Umtawaze Roho moyoni mwako; Akikuongoza katika haki, Hufanywa tayari kwa kazi yake. ← Tenzi 12 | Tenzi Zote | Tenzi 14 → Tazama Tenzi za Rohoni 1–164 Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

Tenzi za Rohoni

Tenzi za Rohoni 12 – Ewe Roho wa Mbinguni

Tenzi za Rohoni 12 – Ewe Roho wa Mbinguni Tenzi Na. 12 Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 12, “Ewe Roho wa Mbinguni”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza. Maneno ya Wimbo Ewe Roho wa Mbinguni Uje kwetu sasa. Ufanye makazi yako Ndani ya Kanisa. Ndiwe mwanga, umulike Tupate jikana; Mengi kwetu yapunguka, Tujalize, Bwana. Ndiwe Moto, teketeza Taka zetu zote: Moyo na iwe sadaka Ya Mwokozi, yote. Ndiwe Umande, na kwako Tutaburudika, Nchi kavu itakuwa Ni yenye Baraka. Roho wa Mbinguni uwe Nasi hapa chini, Mwili uufananishe Na kichwa Mbinguni. ← Tenzi 11 | Tenzi Zote | Tenzi 13 → Tazama Tenzi za Rohoni 1–164 Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

Tenzi za Rohoni

Tenzi za Rohoni 11 – Nina haja nawe

Tenzi za Rohoni 11 – Nina haja nawe Tenzi Na. 11 Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 11, “Nina haja nawe”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza. Maneno ya Wimbo Nina haja nawe Kila saa; Hawezi mwingine Kunifaa. Yesu, nakuhitaji Vivyo kila saa! Niwezeshe, Mwokozi, Nakujia. Nina haja nawe; Kaa nami, Na maonjo haya, Hayaumi. Nina haja nawe; Kila hali, Maisha ni bure, Uli mbali. Nina haja nawe, Nifundishe Na ahadi zako Zifikishe. Nina haja nawe, Mweza yote, Ni wako kabisa Siku zote. ← Tenzi 10 | Tenzi Zote | Tenzi 12 → Tazama Tenzi za Rohoni 1–164 Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

Tenzi za Rohoni

Tenzi za Rohoni 10 – Usinipite!

Tenzi za Rohoni 10 – Usinipite! Tenzi Na. 10 Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 10, “Usinipite!”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza. Maneno ya Wimbo Usinipite Mwokozi, Unisikie; Unapozuru wengine, Usinipite. Yesu,Yesu, Unisikie; Unapozuru wengine, Usinipite. Kiti chako cha rehema, Nakitazama; Magoti napiga pale, Nisamehewe. Sina ya kutegemea, Ila Wewe tu; Uso wako uwe kwangu; Nakuabudu. U Mfariji peke yako; Sina Mbinguni, Wala duniani pote, Bwana mwingine. ← Tenzi 9 | Tenzi Zote | Tenzi 11 → Tazama Tenzi za Rohoni 1–164 Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

Tenzi za Rohoni

Tenzi za Rohoni 9 – Yesu kwetu ni rafiki

Tenzi za Rohoni 9 – Yesu kwetu ni rafiki Tenzi Na. 9 Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 9, “Yesu kwetu ni rafiki”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza. Maneno ya Wimbo Yesu kwetu ni rafiki, Hwamiwa haja pia; Tukiomba kwa Babaye Maombi asikia; Lakini twajikosesha, Twajitweka vibaya; Kwamba tulimwomba Mungu Dua angesikia. Una dhiki na maonjo? Una mashaka pia. Haifai kufa moyo, Dua atasikia Hakuna mwingine mwema Wa kutuhurumia; Atujua tu dhaifu; Maombi asikia. Je, hunayo hata nguvu, Huwezi kuendelea, Ujapodharauliwa Ujaporushwa pia, Watu wange kudharau, Wapendao dunia, Hukwambata mikononi, Dua atasikia. ← Tenzi 8 | Tenzi Zote | Tenzi 10 → Tazama Tenzi za Rohoni 1–164 Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

Tenzi za Rohoni

Tenzi za Rohoni 8 – Taji mvikeni

Tenzi za Rohoni 8 – Taji mvikeni Tenzi Na. 8 Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 8, “Taji mvikeni”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza. Maneno ya Wimbo Taji mvikeni, Taji nyingi tena, Kondoo mwake kitini, Bwana wa mabwana; Name tamsifu Alikufa kwangu, Ni mfalme mtukufu, Mkuu wa Mbingu. Taji mvikeni Mwana wa bikira; Anazovaa kichwani Aliteka nyara; Shiloh wa wanabii, Mchunga wa watu, Shina na tanzu vya Yese, Wa Bethirehemu. Taji mvikeni Bwana wa mapenzi; Jeraha zake ni shani Ni vito vya enzi, Mbinguni hakuna Hata malaika Awezaye kuziona Pasipo kushangaa. ← Tenzi 7 | Tenzi Zote | Tenzi 9 → Tazama Tenzi za Rohoni 1–164 Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

Tenzi za Rohoni

Tenzi za Rohoni 7 – Ni Tabibu Wa Karibu

Tenzi za Rohoni 7 – Ni Tabibu Wa Karibu Tenzi Na. 7 Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 7, “Ni Tabibu Wa Karibu”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza. Maneno ya Wimbo Ni tabibu wa karibu; Tabibu wa ajabu; Na rehema za daima; Ni dawa yake njema. Imbeni, malaika, Sifa za Yesu Bwana; Pweke limetukuka Jina lake Yesu. Hatufai kuwa hai, Wala hatutumai, Ila kweli yeye ndiye Atupumzishaye. Dhambi pia na hatia Ametuchukulia; Twendeni na amani Hata kwake Mbinguni. Huliona tamu jina La Yesu Kristo Bwana, Yuna sifa mwenye kufa Asishindwe na kufa. Kila mume asimame, Sifa zake zivume; Wanawake na washike Kusifu jina lake. Na vijana wote tena, Wapendao sana Waje kwake wawe wake Kwa utumishi wake. ← Tenzi 6 | Tenzi Zote | Tenzi 8 → Tazama Tenzi za Rohoni 1–164 Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

Tenzi za Rohoni

Tenzi za Rohoni 6 – Baba, Mwana, Roho

Tenzi za Rohoni 6 – Baba, Mwana, Roho Tenzi Na. 6 Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 6, “Baba, Mwana, Roho”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza. Maneno ya Wimbo Baba, Mwana, Roho, Mungu mwenye enzi, Kila tukiamka tunakuabudu Baba, Mwana, Roho, Mungu wa mapenzi, Ewe Utatu, tunakusifu. Baba, Mwana, Roho, wakuaminio Wanakutolea shukrani zao Wanakusujudia malaika nao: Wewe u mwanzo, nawe u mwisho. Baba, Mwana, Roho, sisi tu gizani, Utukufu wako hatuoni kosa; U Mtakatifu, nawe u mapenzi, U peke yako, mwenzio huna. Baba, Mwana, Roho, Mungu mwenye enzi, Ulivyoviumba vyote vyakusifu: Baba, Mwana, Roho, Mungu wa mapenzi Ewe Utatu, tunakusifu. ← Tenzi 5 | Tenzi Zote | Tenzi 7 → Tazama Tenzi za Rohoni 1–164 Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

banner
Scroll to Top