Skip to main content

Author name: contact@devinevisiontech.com

Tenzi za Rohoni

Tenzi za Rohoni 5 – Jina lake Yesu tamu

Tenzi za Rohoni 5 – Jina lake Yesu tamu Tenzi Na. 5 Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 5, “Jina lake Yesu tamu”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza. Maneno ya Wimbo Jina lake Yesu tamu; Tukilisikia Hutupoza, tena hamu Hutuondolea. Roho iliyoumia Kwalo hutibika, Chakula, njaani pia; Raha, tukichoka. Jina hili ni msingi, Ngao, ngome, mwamba, Kwa hili napata wingi, Kwangu ni akiba. Yesu, Mchunga, Rafiki Mwalimu, Kuhani, Mwanzo, Mwisho, Njia, Haki, Uzima kifoni. Moyo wangu hauwezi, Kukusifu kweli, Ila sifa zangu hizi, Bwana zikubali. Na utakaponiita, Kuja kwako Bwana, Huko kwako sitaacha Kukusifu sana. ← Tenzi 4 | Tenzi Zote | Tenzi 6 → Tazama Tenzi za Rohoni 1–164 Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

Tenzi za Rohoni

Tenzi za Rohoni 4 – Jina La Yesu Salamu!

Tenzi za Rohoni 4 – Jina La Yesu Salamu! Tenzi Na. 4 Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 4, “Jina La Yesu Salamu!”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza. Maneno ya Wimbo Jina la Yesu, Salamu! Lisujudieni, Ninyi Mbinguni, hukumu Na enzi mpeni. Enzi na apewe kwetu, Watetea dini; Mkuzeni Bwana wenu, Na enzi mpeni. Enyi mbegu ya rehema, Nanyi msifuni; Mmeponywa kwa neema, Na enzi mpeni. Wenye dhambi kumbukeni Ya msalabani, Kwa furaha msifuni, Na enzi mpeni. Kila mtu duniani Msujudieni, Kote-kote msifuni, Na enzi mpeni. Sisi na wao pamoja Tu mumo sifani, Milele sifa ni moja, Ni “Enzi mpeni.” ← Tenzi 3 | Tenzi Zote | Tenzi 5 → Tazama Tenzi za Rohoni 1–164 Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

Tenzi za Rohoni

Tenzi za Rohoni 3 – Hata Ndimi Elfu

Tenzi za Rohoni 3 – Hata Ndimi Elfu Tenzi Na. 3 Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 3, “Hata Ndimi Elfu”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza. Maneno ya Wimbo Hata ndimi elfu elfu, Hazitoshi kweli Bwana Yesu kumsifu, Kwa zake fadhili. Yesu, jina liwezalo Kufukuza hofu; Lanifurahisha hilo, Lanipa wokovu. Jina hilo ni uzima; Ni afya amani; Laleta habari njema; Twalipiwa deni. Yesu huvunja mapingu Ya dhambi moyoni; Msamaha, tena nguvu, Twapata rohoni. Kwa sauti yake vile Wafu hufufuka Wakafurahi milele, Pasipo mashaka. Ewe Yesu wangu Bwana, Uwezo nipewe, Kuhubiri kote sana, Wote wakujue. ← Tenzi 2 | Tenzi Zote | Tenzi 4 → Tazama Tenzi za Rohoni 1–164 Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

Tenzi za Rohoni

Tenzi za Rohoni 2 – Twamsifu Mungu

Tenzi za Rohoni 2 – Twamsifu Mungu Tenzi Na. 2 Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 2, “Twamsifu Mungu”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza. Maneno ya Wimbo Twamsifu Mungu kwa Mwana wa Pendo, Aliyetufia na kupaa juu. Aleluya! Usifiwe; Aleluya! Amin. Aleluya! Usifiwe, utubariki. Twamsifu Mungu kwa Roho Mtukufu, Ametufunulia Mwokozi wetu. Twamsifu Mwana, aliyetufia, Aliyetwaa dhambi akazifuta. Twamsifu Mungu wa neema yote, Ametukomboa akatuongoza. Tuamshe tena, tujazena pendo, Na moyoni uwashe moto wa Roho. ← Tenzi 1 | Tenzi Zote | Tenzi 3 → Tazama Tenzi za Rohoni 1–164 Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

Tenzi za Rohoni

Tenzi za Rohoni 1 – Mwokozi Umeokoa

Tenzi za Rohoni 1 – Mwokozi Umeokoa Tenzi Na. 1 Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 1, “Mwokozi Umeokoa”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza. Maneno ya Wimbo Mwokozi umeokoa, Nimekuwa wako wewe. Damu imenisafisha; Sifa kwa mwana Kondoo. Utukufu, Aleluya! Sifa kwa Mwana Kondoo! Damu imenisafisha, Utukufu kwa Yesu! Nilijitahidi sana Ila sikupata raha; Bali kwa kumtegemea Nilipata Baraka. Daima namwegemea Damu ikifanya kazi, Nikioga kwa chemichemi Itokayo Mwokozi. Sasa nimewekwa wakfu; Nitaishi kwako wewe: Fahari nashuhudia Ya wokovu wa bure. Nasimama kwake Yesu, Ameponya roho yangu; Ameniondoa dhambi, Anifanye mzima. Nilikuwa kifungoni, Niliteswa na dhambi, Nilifungwa minyororo Yesu akanifungua. Sifa, ameninunua! Sifa, nguvu za wokovu! Sifa, Bwana huhifadhi! Sifa zake milele. Tenzi Zote | Tenzi 2 → Tazama Tenzi za Rohoni 1–164 Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

banner
Scroll to Top