Skip to main content

Author name: contact@devinevisiontech.com

Tenzi za Rohoni

Tenzi za Rohoni 35 – Twende kwake

Tenzi za Rohoni 35 – Twende kwake Tenzi Na. 35 Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 35, “Twende kwake”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza. Maneno ya Wimbo Twende kwake, twende kwake, kwake Yesu sasa, Sasa twende kwake, kwake Yesu sasa! Akwokoe. akwokoe, Bwana Yesu sasa! Sasa akwokoe, Bwana Yesu, sasa! Msadiki, msadiki, Bwana Yesu sasa, Sasa msadiki, Bwana Yesu sasa! Anaweza, anaweza, Bwana Yesu sasa, Sasa anaweza, Bwana Yesu sasa! Anapenda, anapenda, Bwana Yesu, sasa, Sasa anapenda, Bwana Yesu sasa! Njoo hima, njoo hima, kwake Yesu sasa, Sasa njoo hima, kwake Yesu, sasa! ← Tenzi 34 | Tenzi Zote | Tenzi 36 → Tazama Tenzi za Rohoni 1–164 Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

Tenzi za Rohoni

Tenzi za Rohoni 34 – Njoni Wenye Dhambi

Tenzi za Rohoni 34 – Njoni Wenye Dhambi Tenzi Na. 34 Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 34, “Njoni Wenye Dhambi”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza. Maneno ya Wimbo Njoni! Njoni! Wenye dhambi, Njoni, msikawie; Yesu awangojea ndiye awapendaye; Ajuaye awezaye kuwaponya ni Yeye. Ewe muhitaji uje; Anakukaribisha, Imani, kweli, na toba, Neema ya kutosha, Jua sana, kwake Bwana Bure utapata. Njoni, mliolemewa Na dhambi ya Adamu; Mkingoja kujiponya Mtapotea mumu; Si wa haki, ni wakosa Waoshwao kwa damu. Ikamtokea dhiki, Mle Gethisemani; Kisha alipoangikwa Akalia mtini; ” Imekwisha”, alitosha Dhabihu ya thamani. Kristo aliye Mbinguni Hutuombea huko; Basi mtumai yeye; Kamwe mwingine hako Yesu pweke, Yesu pweke, Ndiye Mwokozi wako. Wamsifu-sifu sana Mbinguni malaika; Wachanganya nyimbo zao Na waliookoka: Aleluya wataimba Waliooshwa taka. ← Tenzi 33 | Tenzi Zote | Tenzi 35 → Tazama Tenzi za Rohoni 1–164 Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

Tenzi za Rohoni

Tenzi za Rohoni 33 – Dhambi Ikikulemea

Tenzi za Rohoni 33 – Dhambi Ikikulemea Tenzi Na. 33 Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 33, “Dhambi Ikikulemea”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza. Maneno ya Wimbo Dhambi ikikulemea, Kwa Bwana rehema; Hivi sasa tegemea Neno la salama. Tegemea, tegemea, akwita sasa. Ni Mwokozi, ni Mwokozi; amini sasa. Yesu amemwaga damu Ya nyingi baraka; Nawe sasa oga mumu Zioshwamo taka. Ni njia yeye hakika Hwongoza rahani; Usikawe kumshika, Uwe barakani. Karibu nawe wingie Mwetu safarini, Twende tukamwamkie, Milele Mbinguni. ← Tenzi 32 | Tenzi Zote | Tenzi 34 → Tazama Tenzi za Rohoni 1–164 Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

Tenzi za Rohoni

Tenzi za Rohoni 32 – Yesu Awakubali

Tenzi za Rohoni 32 – Yesu Awakubali Tenzi Na. 32 Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 32, “Yesu Awakubali”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza. Maneno ya Wimbo Wakosa Yesu awakubali, Wakosa, wahalifu, Wambieni wa mbali Habari ya wokovu. Tangazeni kwa bidii, “Akubali wakosa!” Liwe neno dhahiri, “Akubali wakosa!” Awakubali Bwana Neno lake amini Watu kila aina Waje kwake tengoni. Mimi ni safi moyo Na mbele ya sharia, Aliye safi roho Kwake ilitimia. Akubali wakosa; Nami anikubali; Alivyonitakasa Mbinguni niwasili. ← Tenzi 31 | Tenzi Zote | Tenzi 33 → Tazama Tenzi za Rohoni 1–164 Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

Tenzi za Rohoni

Tenzi za Rohoni 31 – Msingi Imara

Tenzi za Rohoni 31 – Msingi Imara Tenzi Na. 31 Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 31, “Msingi Imara”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza. Maneno ya Wimbo Msingi imara, enyi wa kweli, Umekwisha pigwa kwa neno hili; Aongeze lipi? Mnayo pia Kwa Yesu mliomkimbilia. Wambiwapo vuka maji ya giza, Mito ya mashaka taipunguza; Takupa nawe, nikuwezeshe, Ipata kufaa, isikutishe! Utakapopishwa ndani ya moto Nnguvu nitakupa, upate pato; Huteketezwi, ila taka zako, Na zitasalia dhahabu zako. Hata zije mvi, walio wangu Hawaoni kwisha mapenzi yangu; Nazo zitakapowenea, ndipo Mabegani mwangu niwatwekapo. Na mtu aliyenitegemea Kamwe kwa adui sitamtia; Nguvu za jehanam zijapotisha, Mtu wangu kamwe sitamuacha. ← Tenzi 30 | Tenzi Zote | Tenzi 32 → Tazama Tenzi za Rohoni 1–164 Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

Tenzi za Rohoni

Tenzi za Rohoni 30 – Nilikuwa kondoo aliyepotea

Tenzi za Rohoni 30 – Nilikuwa kondoo aliyepotea Tenzi Na. 30 Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 30, “Nilikuwa kondoo aliyepotea”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza. Maneno ya Wimbo Nilikuwa kondoo aliyepotea, Sikupenda zizi kamwe, ila kutembea Nilikuwa mwana asiyesikia, Sikupenda baba yangu wala kutulia. Na mchunga mwema alinitafuta, Baba kwa mapenzi ndiye aliyenivuta; Karibu ya kufa, kwa kiu na kwa njaa, Waliniona mnyonge, waliniokoa. Yesu ni mchunga, mwenziwe hapana, Aliosha taka zangu, dhambi nyingi sana; Kwa vidonda vyangu alitia dawa. Ndiye aliyenipata, na kwake nalindwa. Nilikuwa kondoo aliyepotea Sasa nampenda Baba, na mchunga pia; Kwanza nilitanga na kukosa sana, Hivi nyumbani mwa Baba sipotei tena. ← Tenzi 29 | Tenzi Zote | Tenzi 31 → Tazama Tenzi za Rohoni 1–164 Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

Tenzi za Rohoni

Tenzi za Rohoni 29 – Baba yetu aliye Mbinguni

Tenzi za Rohoni 29 – Baba yetu aliye Mbinguni Tenzi Na. 29 Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 29, “Baba yetu aliye Mbinguni”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza. Maneno ya Wimbo Baba yetu aliye Mbinguni Amenifurahisha yakini Kuniambia mwake chuoni Ya kuwa nami Yesu pendoni. Anipenda Mwokozi Yesu, Anipenda, anipenda; Anipenda Mwokozi Yesu, Anipenda mimi. Nimuachapo kutanga mbali, Yeye yu vivyo, hupenda kweli, Hunirejeza kwake moyoni; Kweli yu nami Yesu pendoni. Anipenda! Nami nampenda; Kwa wokovu alionitenda; Akanifia Msalabani Kwa kuwa nami Yesu pendoni. Haya kujua yanipa raha; Kumuamini kuna furaha; Humfukuza mara shetani, Kwona yu nami Yesu Pendoni. Sifa ni nyingi asifiwazo, Moja ni sana katika hizo, Wala siachi, hata Mbinguni, Kwimba, “Yu nami Yesu pendoni”. ← Tenzi 28 | Tenzi Zote | Tenzi 30 → Tazama Tenzi za Rohoni 1–164 Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

Tenzi za Rohoni

Tenzi za Rohoni 28 – Anipenda ni kweli

Tenzi za Rohoni 28 – Anipenda ni kweli Tenzi Na. 28 Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 28, “Anipenda ni kweli”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza. Maneno ya Wimbo Anipenda ni kweli; Mungu anena hili; Sisi wake watoto; kutulinda si zito. Yesu anipenda, Yesu anipenda, Kweli anipenda, Mungu amesema. Kwa kupenda akafa Niokoke na kufa; Atazidi taka, Sana ataniweka. Anipenda kabisa; Niuguapo sasa Anitunza Mbinguni Nniliyelala chini. Kunipenda haachi, Tu sote hapa chini Baada ya mashaka Kwake tanipeleka. ← Tenzi 27 | Tenzi Zote | Tenzi 29 → Tazama Tenzi za Rohoni 1–164 Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

Tenzi za Rohoni

Tenzi za Rohoni 27 – Mungu Ni Pendo

Tenzi za Rohoni 27 – Mungu Ni Pendo Tenzi Na. 27 Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 27, “Mungu Ni Pendo”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza. Maneno ya Wimbo Mungu ni pendo, apenda watu; Mungu ni pendo, anipenda Sikilizeni furaha yangu, Mungu ni pendo, anipenda. Nilipotea katika dhambi, Nikawa mtumwa wa shetani. Akaja Yesu kuniokoa, Yeye kanipa kuwa huru Sababu hii namtumikia, Namsifu yeye siku zote. ← Tenzi 26 | Tenzi Zote | Tenzi 28 → Tazama Tenzi za Rohoni 1–164 Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

Tenzi za Rohoni

Tenzi za Rohoni 26 – Yesu Unipendae

Tenzi za Rohoni 26 – Yesu Unipendae Tenzi Na. 26 Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 26, “Yesu Unipendae”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza. Maneno ya Wimbo Yesu unipendaye Kwako nakimbilia, Ni wewe utoshaye, Mwovu akinijia; Yafiche ubavuni, Mwako maisha yangu; Nifiikishe mbinguni Wokoe moyo wangu. Ngome nyingine sina; Nategemea kwako. Usinitupe Bwana , Nipe neema yako, Ninakuamania Mwenye kuniwezesha; Shari wanikingia, Vitani wanitosha. Nakutaka Mpaji Vyote napata kwako; Niwapo muhitaji, Utanijazi vyako; Nao waangukao Wanyonge wape nguvu; Poza wauguao, Uongoze vipofu. Bwana umeniosha Moyo kwa damu yako; Neema ya kutosha Yapatikana kwako; Kwako Bwana naona Kisima cha uzima; Mwangu moyoni Bwana, Bubujika daima. ← Tenzi 25 | Tenzi Zote | Tenzi 27 → Tazama Tenzi za Rohoni 1–164 Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

banner
Scroll to Top