Tenzi za Rohoni 84 – Niwonapo Mti Bora

Tenzi za Rohoni 84 – Niwonapo Mti Bora

Tenzi Na. 84

Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 84, “Niwonapo Mti Bora”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza.


Maneno ya Wimbo

Niwonapo mti bora
Kristo aliponifia
Kwangu pato ni hasara
Kiburi nakichukia.
Na nisijivune, Bwana
Ila kwa mauti yako;
Upuzi sitaki tena,
Ni chini ya damu yako.
Tangu kichwa hata nyayo,
Zamwagwa pendo na hamu,
Ndako pweke hamu hiyo,
Pendo zako zimetimia.
Vitu vyote vya dunia,
Si sadaka ya kutosha;
Pendo zako zinawia
Nafsi, mali, na maisha.


Tazama Tenzi za Rohoni 1–164


Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

banner
Scroll to Top