Tenzi za Rohoni 66 – Po Pote Mashamba Yajaa
Tenzi Na. 66
Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 66, “Po Pote Mashamba Yajaa”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza.
Maneno ya Wimbo
Po pote mashamba yajaa,
Tele nafaka pevu,
Po pote yang’aa meupe
Bondeni na nyandani.
Mwenye mavuno, wasihi
Upeleke wavuni,
Wakusanye mazao,
Hata kazi iishe.
Wapeleke uchaoni,
Waende na jotoni,
Mpaka jua lishukapo
Wakusanye ko kote.
Watenda kazi wa Bwana,
Mlete sasa mazao,
Na jioni ingieni
Kwake na furaha kuu.