Tenzi za Rohoni 33 – Dhambi Ikikulemea
Tenzi Na. 33
Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 33, “Dhambi Ikikulemea”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza.
Maneno ya Wimbo
Dhambi ikikulemea,
Kwa Bwana rehema;
Hivi sasa tegemea
Neno la salama.
Tegemea, tegemea,
akwita sasa.
Ni Mwokozi, ni
Mwokozi; amini sasa.
Yesu amemwaga damu
Ya nyingi baraka;
Nawe sasa oga mumu
Zioshwamo taka.
Ni njia yeye hakika
Hwongoza rahani;
Usikawe kumshika,
Uwe barakani.
Karibu nawe wingie
Mwetu safarini,
Twende tukamwamkie,
Milele Mbinguni.