Tenzi za Rohoni 18 – Akifa Yesu nikafa naye

Tenzi za Rohoni 18 – Akifa Yesu nikafa naye

Tenzi Na. 18

Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 18, “Akifa Yesu nikafa naye”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza.


Maneno ya Wimbo

Akifa Yesu nikafa naye
Uzima upya huishi naye;
Humtazama mpaka nje:
Nyakati zote ni wake yeye.

Nyakati zote nimo pendoni,
Nyakati zote ni uzimani,
Humtazama hata atokee,
Nyakati zote mimi ni wake.

Vita sipigi visivyo haki,
Na Bwana wangu hapiganiki;
Beramu yake haitwaliki,
Napo po pote hila sitaki.

Sina mashaka, akawa mbali;
Mizigo yote aihimili;
Ananituliza Imanweli,
Nyakati zote mimi husali.

Sina huzuni na mimi sidhii;
Simwagi chozi, wala siguni;
Sikuti afa, ila kitini
Daima hunifikiri mimi.

Kila unyonge huusikia;
Kila ugonjwa kwake hupoa;
Yesu ni mwenye kuniokoa
Nyakati zote hunijalia.


Tazama Tenzi za Rohoni 1–164


Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

banner
Scroll to Top