Tenzi za Rohoni 3 – Hata Ndimi Elfu

Tenzi za Rohoni 3 – Hata Ndimi Elfu

Tenzi Na. 3

Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 3, “Hata Ndimi Elfu”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza.


Maneno ya Wimbo

Hata ndimi elfu elfu,
Hazitoshi kweli
Bwana Yesu kumsifu,
Kwa zake fadhili.

Yesu, jina liwezalo
Kufukuza hofu;
Lanifurahisha hilo,
Lanipa wokovu.

Jina hilo ni uzima;
Ni afya amani;
Laleta habari njema;
Twalipiwa deni.

Yesu huvunja mapingu
Ya dhambi moyoni;
Msamaha, tena nguvu,
Twapata rohoni.

Kwa sauti yake vile
Wafu hufufuka
Wakafurahi milele,
Pasipo mashaka.

Ewe Yesu wangu Bwana,
Uwezo nipewe,
Kuhubiri kote sana,
Wote wakujue.


Tazama Tenzi za Rohoni 1–164


Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

banner
Scroll to Top