Skip to main content

Ufugaji Bora na Rahisi wa Kuku wa Kienyeji – Muundo 01: Misingi na Dhana Muhimu

MAKTABA YA UFUGAJI WA KUKU • DEVINE VISION TECH

Misingi na Dhana Muhimu: Ufugaji Bora na Rahisi wa Kuku wa Kienyeji – Muundo 01

Makala hii inasaidia kusoma na kuelewa Ufugaji Bora na Rahisi wa Kuku wa Kienyeji – Muundo 01. Fahamu dhana na maneno muhimu yanayoelezwa ndani ya kitabu hiki cha ufugaji wa kuku. Maelezo yamepangwa kwa kurejea maandishi yaliyochukuliwa kutoka kwenye PDF halisi. Kwa mifano, jedwali na michoro kamili, tumia kitabu kilichopachikwa chini.

Chanzo: Ufugaji Bora na Rahisi wa Kuku wa Kienyeji – Muundo 01 · PDF · 28 kurasa

Ufugaji Bora na Rahisi wa Kuku wa Kienyeji - Muundo 01 – jalada la PDF
Picha ya jalada inaweza kuhitaji ruhusa ya kutazama faili katika Google Drive.

Dhana muhimu na maelezo yake kwenye chanzo

UFUGAJI BORA NA RAHISI WA KUKU WA KIENYEJI 4

Katika sehemu hii, mwongozo unagusia mambo yafuatayo:

Watunze vizuri kwa kuwapatia chakula kilicho na mchanganyiko kamili wa viini lishe vinavyotakiwa katika mwili wa kuku, yaani; wanga, protini, calcium, chumvichumvi, madini joto nk (kama nilivyoeleza hapa chini). Wawekee na Jogoo mmoja mzuri wa kienyeji/kizungu/chotara (kama nilivyoeleza hapa chini juu ya uchaguzi wa majogoo). Wanapoanza kutaga watayarishie mahali pazuri/Kiota kizuri cha kutagia na kuatamia kwa kuwajengea viota ndani ya banda. Hakikisha mahali hapo hapavuji wala hapapati unyevunyevu wala joto kali sana. Hakikisha mahali hapo…

Chunguza maana ya maneno yanayotumika na jinsi yanavyohusiana na vipengele vingine vya mwongozo.

KKUKU/VIFARANGA VIFARANGA CHUMBA/BANDA 2

Katika sehemu hii, mwongozo unagusia mambo yafuatayo:

Inashauriwa kuwa siyo salama kufuga aina nyingine ya ndege kama vile njiwa, bata, bata mzinga nk kwa kuwachanganya na kuku maana kila aina ya ndege wanamagonjwa yao. Hivyo kuwachanganya kutakufanya ushindwe namna ya kuwatibu wanapopatwa na ugonjwa. Pia chawa wa njiwa huleta ugonjwa wa Ndui hasa kuku wanapoangua vifaranga wao. Hapa ugonjwa unaweza kufyeka vifaranga wako wote 60/100 kama utafuata ushauri wangu! Baada ya wiki 2 hadi 3 baada ya kuwanyang’anya vifaranga kuku wako wataanza tena kutaga mayai. Wakiatamia wote 5 Kama utaimarisha huduma…

Chunguza maana ya maneno yanayotumika na jinsi yanavyohusiana na vipengele vingine vya mwongozo.

KKUKU/VIFARANGA VIFARANGA CHUMBA/BANDA 6

Katika sehemu hii, mwongozo unagusia mambo yafuatayo:

Banda liwe na vichanja maana kuku hupenda kulala juu ya vichanja maana nao ni ndege. 2. Vyombo safi na vizuri kwaajili ya chakula na maji. 3. Walazie majani makavu/maranda ya mbao/makapi ya mazao sakafuni kwa banda zima. UCHAGUZI NA UHIFADHI WA MAYAI. Mayai huharibika kwa urahisi sana yasipo tayarishwa na kutunzwa vizuri kwa uangalifu. Matayarisho huanzia bandani hadi ndani kwa kufanya yafuatayo; o Hakikisha viota vyote ni safi wakati wote. o Chakula kiwe ni cha kuimarisha gamba la yai na vyakula vingine. o Vyombo vya kukusanyia mayai viewe…

Chunguza maana ya maneno yanayotumika na jinsi yanavyohusiana na vipengele vingine vya mwongozo.

KKUKU/VIFARANGA VIFARANGA CHUMBA/BANDA 7

Katika sehemu hii, mwongozo unagusia mambo yafuatayo:

Lakini unashauriwa kusugua kwa mkono bila maji ili kusafisha maana maji hupunguza ubora wa yai na maranyingi yai huharibika haraka. o Weka katika vyombo visafi kwa kuelekeza sehemu ya yai iliyo pana iwe juu na sehemu nyembamba iwe chini, beba kwa uangalifu. o Hifadhi mayai katika sehemu ya baridi nyuzijoto10 hadi 16 za sentigredi. o Mayai yapangwe kwa daraja kwa kufuata ukubwa na rangi ili kuvutia wateja na kuongeza bei. Pia unaweza kuweka kwa kufuata muda unapoyaokota kutoka bandani. Weka lebo yenye tarehe ili usichanganye wakati wa…

Chunguza maana ya maneno yanayotumika na jinsi yanavyohusiana na vipengele vingine vya mwongozo.

1 Ufugaji Huria

Katika sehemu hii, mwongozo unagusia mambo yafuatayo:

Aina hii ya ufugaji, kuku huachiwa huru wajitafutie chakula na maji wao wenyewe. Utaratibu huu hutumika zaidi kufugia kuku wa kienyeji ambapo mfugaji hupata hasara na pengine hupata faida kidogo maana kuku hukosa uangalizi na hawapewi chakula cha ziada. Faida. o Haina gharama kubwa za ufugaji. o Kuku hupata mazoezi ya kutosha. Hasara. o Huharibu mazingira maana hula nafaka, mazao nk. o Ni rahisi kuambukizwa na kusambaza magonjwa. o Ni rahisi kuathiriwa na hali mbaya ya hewa, watu na wanyama wakali kama paka, vicheche, mwewe, kipanga, nyoka nk.…

Chunguza maana ya maneno yanayotumika na jinsi yanavyohusiana na vipengele vingine vya mwongozo.

1 Ufugaji Huria 5

Katika sehemu hii, mwongozo unagusia mambo yafuatayo:

Namna ya kuandaa chakula cha kuku. Vyakula vya kuku vinapaswa kuwa na aina/viini lishe muhimu kama vile Protini, Wanga, madini na Vitamini. Vyakula hivyo vimegawanyika kama ifuatavyo; o Vyakula vya kujenga mwili ni; Jamii ya kunde,samaki, dagaa,mashudu ya ufuta/alizeti/pamba, o Vyakula vya kulinda mwili ili usipatwe na maradhi ni; Mafuta ya samaki na majani mabichi kama vile; kabichi, mchicha,majani ya mpapai na nyasi mbichi. o Vyakula vinavyojenga mwili/mifupa ni kama vile; Aina za madini, chokaa, chumvi na mifupa iliyosagwa. o Vyakula…

Chunguza maana ya maneno yanayotumika na jinsi yanavyohusiana na vipengele vingine vya mwongozo.

1 Ufugaji Huria 6

Katika sehemu hii, mwongozo unagusia mambo yafuatayo:

Na kama huwezi unaweza kujitengenezea wewe mwenyewe kwa kukusanya mahitaji muhimu ya viinilishe kama ifuatavyo hapa chini; Aina ya chakula Kiwango cha uchanganyaji (%) Vyakula Vifaranga Kuku wa Nyama Kuku wa Mayai (Kgs) (Kgs) (Kgs) Mahindi 70 70 70 Ulezi 20 40 40 Mtama 20 30 30 Mpunga 40 70 70 Ngano 5 40 40 Pumba za Mahindi 10 20 20 Pumba za Mpunga 10 20 20 Pumba za Matama 10 20 20 Pumba za Ngano 5 15 15 Mashudu ya Nazi 10 30 40 Mashudu ya Pamba 5 10 10 Mashudu ya Alizeti 10 20 20 Mashudu ya Ufuta 10 10 5 Damu iliyokaushwa 5 5 5 Mifupa…

Chunguza maana ya maneno yanayotumika na jinsi yanavyohusiana na vipengele vingine vya mwongozo.

1 Pilipili kichaa 6

Katika sehemu hii, mwongozo unagusia mambo yafuatayo:

Namna ya kuzuia. o Kuku wapewe chakula chenye mchanganyiko wa viinilishe vyote muhimu kama vile Vitamini, madini na Chokaa kufuatana na umri/aina na mahitaji yake. o Wapewe majani mabichi kama mchicha, kabichi na majani ya mapapai. o Wapewe mchanganyiko wa vitamin na madini kama chokaa na chumvi kwa kiwango maalum maana ikizidi pia yaweza kuathiri kuku. 3. MUHIMU. Ili liziua magonjwa ya kuku na kupata faida kubwa kwa kufuga kuku, ni muhimu sana mtu anayehudumia kuku bandani aweze kutambua haraka dalili za magonjwa ya kuku kama nilivyoeleza…

Chunguza maana ya maneno yanayotumika na jinsi yanavyohusiana na vipengele vingine vya mwongozo.

1 FORMULA 100Kgs za Chakula cha Kuku

Katika sehemu hii, mwongozo unagusia mambo yafuatayo:

1. Mahindi yaliyoparazwa 25Kgs. 2. Pumba za Mahindi 25Kgs. 3. Dagaa/Uduvi 10Kgs. 4. Unga wa Mifupa/Bionemeal 5Kgs. 5. Chokaa/Limestone 5Kgs. 6. Mashudu ya Alizeti 5kgs. 7. Mashudu ya Pamba 10kgs. 8. Ngando ndogondogo 5kgs. 9. Machicha ya ngano/Wheat Brand 10kgs. milioni-1-a.html

Chunguza maana ya maneno yanayotumika na jinsi yanavyohusiana na vipengele vingine vya mwongozo.

Soma PDF ya Kitabu Kamili

Muonekano wa PDF unategemea ruhusa za faili katika Google Drive. Kama haisomeki, tumia kiungo cha kufungua chanzo.

Rudi kwenye Maktaba ya Vitabu

Makala ni mwongozo wa kusoma chanzo. Hakiki jedwali, gharama na maelezo ya kiufundi kwenye PDF ya asili kabla ya kufanya maamuzi. Kwa masuala ya afya ya kuku, shirikisha mtaalamu wa mifugo. Ruhusa za kuchapisha na upatikanaji wa PDF kwa umma bado zinahitaji kuthibitishwa.

Scroll to Top
Changia Notes / Document