Mwongozo wa Hatua za Vitendo: Ufugaji wa Kuku wa Mayai
Makala hii inasaidia kusoma na kuelewa Ufugaji wa Kuku wa Mayai. Jifunze vipengele vya utekelezaji na maswali ya kupanga kazi vinavyoibuliwa na mwongozo huu. Maelezo yamepangwa kwa kurejea maandishi yaliyochukuliwa kutoka kwenye PDF halisi. Kwa mifano, jedwali na michoro kamili, tumia kitabu kilichopachikwa chini.
Namna ya kutumia taarifa za kitabu katika kazi
KULEA VIFARANGA KEEPING CHICKS
Katika sehemu hii, mwongozo unagusia mambo yafuatayo:
Kabla ya kuwaleta vifaranga nyumbani kwako hakikisha unafanya maandalizi yafuatayo; Hakikisha umeandaa sehemu maalumu ya kuwalea vifaranga (Brooder) Hakikisha una taa za kandili au balbu zinazotumia umeme au jiko la mkaa kwa ajili ya kuwapatia joto vifaranga. Hakikisha umeandaa matandazo ya kuweka kwenye sakafu kama maranda ya mbao,mapumba ya mpunga n.k. kwa ajili ya kuwapa joto Eneo la mita mraba 1 (1m2) hutosha vifaranga 20 hadi kufikia umri wa wiki 4 Dhibiti joto bandani au sehemu maalum ya kuwalea vifaranga (Brooder) hadi kufikia nyuzijoto…
Kabla ya kutumia taarifa hizi shambani, linganisha na hali ya banda, kuku, rasilimali na ushauri wa afisa mifugo.
CHANJO NA UMUHIMU WAKE
Katika sehemu hii, mwongozo unagusia mambo yafuatayo:
Utaratibu wa Chanjo kwa vifaranga ni Lazima, ili kuwafanya vifaranga wasikumbwe na magonjwa ya aina zote. Faida kubwa za chanjo kwa Kuku ni kama ifuatavyo; Kuchanja kuku kwa wakati husaidia mwili wa kuku kuwa na uwezo mkubwa wa kuzuia magonjwa. Kama ugonjwa umeingia, Idadi ya kuku watakaoathirika huwa ndogo sana Kuku watakao kufa kwa ajili ya ugonjwa huwa ni ndogo. Kuna Chanjo za aina nyingi zinazotumiwa na kuku wa mayai kama Marex, Ranikheth, Gumboro, Bruchaities, Bosonto, Salmonela n.k.
Kabla ya kutumia taarifa hizi shambani, linganisha na hali ya banda, kuku, rasilimali na ushauri wa afisa mifugo.
ANGALIZO KABLA YA KUTOA CHANJO
Katika sehemu hii, mwongozo unagusia mambo yafuatayo:
Utoaji wa chanjo una taratibu zake, Inakupasa kuzifwata kwa uangalifu taratibu hizo. Taratibu hizo ni kama ifuatavyo; Wakati wa kutoa chanjo washike kuku wako vizuri Wachanje kuku wako pasipo kutumia nguvu nyingi, washike taratibu. Usiwape chanjo kuku waliougua, wapatie kuku wenye afya tu. Fanya chanjo wakati wa hali ya hewa ya baridi (Cold weather condition) Baada ya kumaliza kufanya chanjo, osha vifaa vyako vyote na Maji ya moto au dawa za kutibu vifaa kutokana na vimelea vya magonjwa (germicide medicine/antiseptic)
Kabla ya kutumia taarifa hizi shambani, linganisha na hali ya banda, kuku, rasilimali na ushauri wa afisa mifugo.
KUKATA MIDOMO YA KUKU NA UMUHIMU WAKE
Katika sehemu hii, mwongozo unagusia mambo yafuatayo:
Kukata au kupunguza midomo ya kuku wa mayai ni muhimu sana. Zifuatazo ni faida muhimu za kuwakata kuku midomo; Ukataji wa midomo husaidia kupunguza hali ya kuku kudonoana. Husaidia kuzuia upotevu wa chakula. Vilevile husaidia kupunguza tabia ya kudonoa mayai. Namna ya kuwakata kuku midomo Wakate vifaranga wako midomo wakifikia umri wa siku 8 hadi 10. Wakate tena midomo wakishakua wakifikia umri wa wiki 8 hadi 12. Kwa vifaranga wakate sm 0.2 kutoka kwenye pua. Kwa kuku wanaokua wakate sm 0.45 kutoka kwenye pua. Wakate midomo yote wa juu na wa…
Kabla ya kutumia taarifa hizi shambani, linganisha na hali ya banda, kuku, rasilimali na ushauri wa afisa mifugo.
KUWAPA CHAKULA
Katika sehemu hii, mwongozo unagusia mambo yafuatayo:
Kuna makampuni mengi ya kutengeneza chakula cha kuku wa mayai ulimwengu mzima. Kwa hiyo unaweza ukanunua chakula kwa hao watengenezaji au ukatengeneza mwenyewe nyumbani kwako. Kama utanunua au utatengeneza mwenyewe lazima uhakikishe kwamba unapata chakula chenye ubora na chenye virutubisho vyote muhimu. Kirutubisho cha Protini na Madini ni muhimu sana kwa kuku wa mayai. Wapatie madini ya Calcium 2% kwa wiki mbili baada ya kuzaliwa. Kama utaona hawaongezeki uzito kama inavyotakiwa, wapatie Chakula cha kuanzia (Starter feed) kwa wiki 8, wape…
Kabla ya kutumia taarifa hizi shambani, linganisha na hali ya banda, kuku, rasilimali na ushauri wa afisa mifugo.
NAMNA YA KUTENGENEZA CHAKULA CHA KUKU WA MAYAI
Katika sehemu hii, mwongozo unagusia mambo yafuatayo:
Kutengeneza chakula cha kuku wa mayai, si jambo la mzaha mzaha, kwamba unachanganya changanya tu hovyo hovyo, inakupasa uwe makini sana kuhakikisha unaweka virutubisho vyote vinavyofaa kwa kuku wa umri husika. Kama utaona huwezi kukidhi vigezo vya kutengeneza vyakula hivi, basi unaweza ukanunua kwenye makampuni mbalimbali yanayotengeneza vyakula hivi kwa kuzingatia ubora na yanayopatikana
Kabla ya kutumia taarifa hizi shambani, linganisha na hali ya banda, kuku, rasilimali na ushauri wa afisa mifugo.
KUWAPATIA MAJI YA KUNYWA
Katika sehemu hii, mwongozo unagusia mambo yafuatayo:
Afya bora ya kuku hutegemea sana jinsi unavyowapa maji safi na salama. Inatakiwa uwapatie kuku wako maji ya kutosha kulingana na uhitaji. Pia yatibu maji ya kunywa ya kuku ili kuua bacteria wa kwenye maji kwa kutumia dawa ya Klolini (Chlorine) au Bliching powder. Chagua sehemu nzuri ya kuweka chombo cha maji ya kunywa ndani ya banda la kuku. Wapatie maji ya baridi wakati wa joto kali na wapatie maji ya vuguvugu wakati wa baridi kali. Ukifwata maelekezo yote ya hapo juu kwa uangalifu, utaiona faida kubwa ya kufuga kuku wa mayai.
Kabla ya kutumia taarifa hizi shambani, linganisha na hali ya banda, kuku, rasilimali na ushauri wa afisa mifugo.
Soma PDF ya Kitabu Kamili
Muonekano wa PDF unategemea ruhusa za faili katika Google Drive. Kama haisomeki, tumia kiungo cha kufungua chanzo.
Makala ni mwongozo wa kusoma chanzo. Hakiki jedwali, gharama na maelezo ya kiufundi kwenye PDF ya asili kabla ya kufanya maamuzi. Kwa masuala ya afya ya kuku, shirikisha mtaalamu wa mifugo. Ruhusa za kuchapisha na upatikanaji wa PDF kwa umma bado zinahitaji kuthibitishwa.