Pakua Windows Matoleo Yote
Windows 11, Windows 10 64-bit, Windows 10 Pro na Windows 7 pamoja na Rufus na hatua za kutengeneza bootable USB na ku-install Windows.
Pakua Windows ISO
Windows 11 Pro
ISO kwa ajili ya clean installation au kutengeneza bootable USB.
Pakua Windows 11Windows 10
Windows 10 ISO ya 64-bit kwa reinstall au bootable USB.
Pakua Windows 10Windows 10 Pro 1511
Toleo la zamani la Windows 10 Pro kwa matumizi ya compatibility maalumu.
Pakua Windows 10 ProWindows 7 All Versions
ISO ya Windows 7 yenye matoleo mbalimbali kwa kompyuta za zamani au matumizi ya legacy.
Pakua Windows 7Pakua Rufus
Rufus 4.15
Rufus hutumika kutengeneza bootable USB kutoka kwenye Windows ISO.
Pakua Rufus DirectRufus 4.15 Portable
Toleo portable; halihitaji installation ya kawaida kabla ya kulitumia.
Pakua Rufus PortableJinsi ya Kutengeneza Bootable USB kwa Rufus
- Pakua Windows ISO unayotaka kutumia.
- Pakua na fungua Rufus.
- Weka flash disk ya angalau 8 GB. Data iliyopo kwenye USB itafutwa.
- Device: chagua flash disk sahihi.
- Boot selection: chagua Disk or ISO image, bonyeza SELECT, kisha chagua ISO.
- Partition scheme: kwa computer nyingi za kisasa zenye UEFI tumia GPT. Kwa baadhi ya computer za zamani za Legacy BIOS tumia MBR.
- Bonyeza START na subiri mpaka Rufus ionyeshe READY.
Jinsi ya Ku-install Windows
- Fanya backup ya mafaili yako muhimu.
- Weka bootable USB kwenye computer unayotaka ku-install.
- Washa computer na fungua Boot Menu. Mara nyingi key huwa F12, F9, F11, Esc au nyingine kulingana na brand.
- Chagua USB drive kutoka boot menu.
- Chagua Language, Time na Keyboard, kisha bonyeza Install now.
- Weka genuine product key ukiwa nayo. Kama computer tayari ina digital license inayolingana na edition unayosakinisha, unaweza kuchagua I don’t have a product key na ku-activate baada ya ku-connect internet.
- Chagua edition inayolingana na leseni yako.
- Kwa clean install chagua Custom: Install Windows only. Hakikisha partition unayochagua ni sahihi kabla ya kuifuta au kuformat.
- Endelea na installation. Computer itarestart mara kadhaa.
- Baada ya installation, connect internet, fungua Windows Update na install drivers za computer yako.
GPT au MBR: Nichague Ipi?
| Aina ya Computer | Partition Scheme | Target System |
|---|---|---|
| Computer nyingi za kisasa | GPT | UEFI |
| Computer za zamani | MBR | BIOS / Legacy |
Kuhusu Windows Activation
Kwa usalama na uhalali wa leseni, tumia genuine product key au digital license. Kwa Windows 11 nenda Settings > System > Activation. Kwa Windows 10 nenda Settings > Update & Security > Activation. Activators zinazobypass leseni hazijawekwa kwenye post hii.
Official Windows Downloads na Miongozo
Kama unataka ISO ya sasa kutoka Microsoft, tumia kurasa rasmi:
Windows 11 OfficialWindows 10 OfficialMicrosoft Installation Media GuideRufus Official WebsiteMaswali Yanayoulizwa Mara kwa Mara
USB ya Windows iwe na ukubwa gani?
Kwa Windows 11 na Windows 10, USB ya angalau 8 GB inapendekezwa.
Je, lazima niwe na product key wakati wa installation?
Si kila mara. Kama computer ina digital license inayolingana na edition unayosakinisha, activation inaweza kufanyika baada ya ku-connect internet. Vinginevyo tumia genuine product key.
Kwa nini Windows 11 haikubali ku-install?
Sababu inaweza kuwa hardware kutokidhi mahitaji, UEFI/Secure Boot/TPM settings, partition scheme isiyolingana, au installation media yenye tatizo.
Naweza ku-install bila kufuta mafaili?
Kwa baadhi ya upgrade au reinstall options unaweza kuhifadhi files na apps. Clean install inaweza kufuta kila kitu, hivyo backup ni muhimu.