Tenzi za Rohoni 86 – Damu Imebubujika

Tenzi za Rohoni 86 – Damu Imebubujika

Tenzi Na. 86

Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 86, “Damu Imebubujika”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza.


Maneno ya Wimbo

Damu Imebubujika,
Ni ya Imanweli,
Wakioga wenye taka,
Husafiwa kweli.
Ilimpa kushukuru
Mwivi mautini;
Nami nisiye udhuru,
Yanisafi ndani.
Kondoo wa kuuawa,
Damu ina nguvu,
Wako wote kuokoa,
Kwa utimilivu.
Bwana tangu damu yako
Kunisafi kale,
Nimeimba sifa zako;
Taimba milele.
Nikifa tazidi kwimba
Sifa za wokovu
Ulimi ujaponyamaa
Vumbini mwa ufu.
Bwana, umenikirimu
Nisiyestahili
Kwa damu yako, sehemu
Ya mali ya kweli.
Nikubali kukwimbia,
Mbinguni milele,
Mungu nitakusifia
Jina lako pweke.


Tazama Tenzi za Rohoni 1–164


Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

banner
Scroll to Top