Tenzi za Rohoni 71 – Mteteeni Yesu

Tenzi za Rohoni 71 – Mteteeni Yesu

Tenzi Na. 71

Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 71, “Mteteeni Yesu”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza.


Maneno ya Wimbo

Mteteeni Yesu,
Mlio askari;
Inueni beramu,
Mukae tayari,
Kwenda nae vitani,
Sisi hatuchoki
Hata washindwe pia
Yeye amiliki.
Mteteeni Yesu,
Vita ni vikali;
Leo siku ya Bwana,
Atashinda kweli,
Waume twende naye,
Adui ni wengi,
Lakini kwake Bwana
Tuna nguvu nyingi.
Mteteeni Yesu,
Wenye ushujaa;
Nguvu zenu za mwili
Hazitatufaa;
Silaha ya injili
Vaeni daima,
Kesheni mkiomba,
Sirudini nyuma.
Mteteeni Yesu,
Vita ni vikali,
Wengi wamdharau,
Hawamkubali,
Ila atamiliki
Tusitie shaka,
Kuwa naye vitani
Twashinda hakika.


Tazama Tenzi za Rohoni 1–164


Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

banner
Scroll to Top