Tenzi za Rohoni 19 – Ndiyo dhamana, Yesu wangu

Tenzi za Rohoni 19 – Ndiyo dhamana, Yesu wangu

Tenzi Na. 19

Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 19, “Ndiyo dhamana, Yesu wangu”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza.


Maneno ya Wimbo

Ndiyo dhamana, Yesu wangu;
Hunipa furaha za Mbingu;
Mrithi wa wokovu wake
Nimezawa kwa Roho yake.

Habari njema, raha yangu
Yesu ndiye Mwokozi wangu,
Habari njema, raha yangu
Yesu ndiye mwokozi wangu.

Kumsalimu moyo wangu,
Mara namwona raha yangu;
Aniletea malaika,
Wananilinda, taokoka.

Sina Kinyume, nashukuru,
Mchana kutwa huja kwangu;
Usiku kucha kuna nuru;
Mwokozi wangu; ndimi huru.

Hali na mali anitwaa!
Mara namwona anifaa,
Nami nangoja kwa subira;
Akiniita, nije mara.


Tazama Tenzi za Rohoni 1–164


Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

banner
Scroll to Top