Kiswahili Kidato cha Nne – Uundaji wa Maneno

Kiswahili Kidato cha Nne – Uundaji wa Maneno

Maelezo haya ya Kiswahili Kidato cha Nne yanahusu Uundaji wa Maneno. Yamepangwa kwa vipengele vinavyosomeka kwa urahisi kwenye simu, huku maudhui ya msingi, mifano, maelezo na mazoezi yaliyotambulika kutoka kwenye nyaraka yakihifadhiwa.

Lugha hukua na kubadilika kila wakati kulingana na maendeleo ya jamii. Kigezo kimojawapo | cha kukua na kubadilika kwa lugha ni kuongezeka kwa msamiati. Ili msamiati uongezeke katika lugha sharti maneno mapya yaundwe.

| Njia za Uundaji Maneno Uundaji wa Msamiati hutokea kwa njia mbalimbali zifuatazo:

1. Kubadili mpangilio wa herufi.

Kuambatanisha maneno.

3. Kutohoa maneno ya lugha nyingine. 4. Uambishaji wa maneno, | 5. Kufanikisha sauti, umbo, mlio na sura.

Kuunda msamiati kwa kubadili mpangilio wa herufi Neno hujengwa kwa vitamkwa au herufi. Neno jipya lenye maana tofauti huweza kuundwa kwa kubadili mpangilio wa neno lingine Mfano * Neno lima, lina herufi |, i, m, a, herufi hizi huweza kujenga maneno kama mali, kumi,imla, mila. « Neno tua lina herufi t, u, a, herufi hizi zina weza kujenga maneno kama:- tatu, tua, viatu, tatua. Njia ya kuambatanisha maneno Kuna njia tatu za kuambatanisha meneno Nijia ya kurudufisha au kukariri neno Mfano; barabara, sawasawa, polepole, katikati, vilevile.

Njia ya uundaji wa Msamiati kwa kuunganisha maneno mawili tofauti Nomino na Nomino

+ Punda + mlia unapata Pundamilia + Bibi + Shamba unapata Bibishamba | + Afisa + Elimu unapata A fisaelimu + Mwana + Siasa unapata Mwanasiasa « Bata + maji unapata Batamaji | Kuunganisha kitenzi na Nomino/Jina « Changa + moto changamoto | + Chemsha + bongo chemshabongo ] > Piga + mbizi pigambizi

+ Zima + moto zimamoto

Kuunganisha maneno mawili na kudondosha baadhi ya herufi Mfano

Baraza la Kiswahili Tanzania BAKITA Mzaliwa wa mahali Fulani MZAWA Chama cha Mapinduzi CCM Nyamamfu NY AMAFU

Kutohoa maneno kutoka lugha nyingine

Kila lugha na tabia ya kuchukua maneno lugha nyingine ili kukidhi mahitaji ya Msamiati. Maneno kutoka lugha nyingine yanapoteuliwa hubadilishwa kimatamshiili ya fuate kanuniza Kiswahili.

Maneno yanayotoholewa kutoka lugha nyingine husanifishwa na asasi za lugha ya Kiswahili ndipo ya ruhusiwe kutumiwa rasmi.

Mfano

Neno la Kiswahili Lugha ya Mwanzo Neno Lililotoholewa

Kijerumani Schule Salama Kiarabu Salaam Duka Kihindi Dukan Karoti Kiingereza Carrot Shati Kiingereza Shirt Picha Kiingereza Picture Papai Kihispania Papaya Meza Kireno Mezi Shukrani Kiarabu Shukran Negeli Kihaya Engeli Ikulu Kinyamwezi Tkulu Nevatuka Kizanaki Ngvatuka Ndafu Kichaga Ndafu

Namba

Kuunda maneno kwa njia ya uambishaji wa maneno

Hii ni njia ya kubandika viambishi awali na tamati kwe nyekiini. Ujenzi wa maneno hutokana na mzizi mmoja kuonesha maana tofauti ingawa maana zina husiana.

Mfano mzizi: -lim-.Tukipachika viambishi awali na tamati tunapata maneno kama lima, analima, walilima, kilimo, limiana,halitalimwa na ukulima.

Kufananisha sauti, sura au tabia

Example 4

Mfano

Kengele – utokana na sauti ya kengele inapo pigwa

Pikipiki – hutokana na muungurumo wa pikipiki

Ndizi mkono wa tembo — Ndizi inayo fananishwa na mkono wa mnyama tembo

Chubwi – Jiwe au chura atumbukiapo katika kina cha maji.

Mazingira yanayoelezea Kuhitaji Maneno Mapya

————-

Mabadiliko mengi yanatokea kila siku katika nyanja mbalimbali za kimaisha-mabadiliko ya kiuchumi, kisiasa, kisayansi na kiteknolojia. Katika mazingira kama haya, watu watahitaji kuwasiliana, lugha itahitaji kuunda maneno ili kuwasilisha dhana mpya zilizoibuka. Kwa mfano, maneno kama vile nywila, kisakuzi, udukuzi, puku, talakirishi n.k yameundwa ili kuwasilisha | dhana za kiteknoljia kwa Kiswahili.

Undaji wa Maneno katika Miktadha mbalimbali

Mabadiliko ya kimaendeleo yanafanya lugha ihitaji maneno ya kuyafikisha na kutumiwa na | jamii. Ili kukidhi mahitaji hayo, maneno mapya yanazuka. Maneno hayo yanaweza kuwa katika fani mbalimbali, kama vile sayansi na teknolojia, siasa, utamaduni na uchumi kulingana na mkondo wa maendeleo. Mfano wa msamiati ni kama vile fedha, ushuru, kumpyuta, ukoloni, hospitali, suruali n.k

Get Well-Formatted PDF Notes

For a cleaner PDF copy for offline study, revision and printing, request the notes through WhatsApp.

GET WELL-FORMATTED PDF NOTES

banner
Scroll to Top