Skip to main content

Tenzi za Rohoni 155 – Hapana Rafiki Kama Yesu

Tenzi za Rohoni 155 – Hapana Rafiki Kama Yesu

Tenzi Na. 155

Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 155, “Hapana Rafiki Kama Yesu”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza.


Maneno ya Wimbo

KIITIKIO:
Yesu ajua shida zetu,
aweza kutuongoza.
Hapana rafiki kama Yesu,
yu pekee, yu pekee.

1. Hapana rafiki kama Yesu,
yu pekee, yu pekee.
Hapana mpozi kama Yesu,
yu pekee, yu pekee.

2. Yeye anaye sifa, ni Yesu,
yu pekee, yu pekee.
Ndiye aliye mnyenyekevu,
yu pekee, yu pekee.

3. Yesu pamoja nasi daima,
yu pekee, yu pekee.
Kwa usiku aleta salama,
yu pekee, yu pekee.

4. Kulinda Yesu yu mwaminifu,
yu pekee, yu pekee.
Atawakubali wahalifu,
yu pekee, yu pekee.

5. Alipelekwa awe Mwokozi,
yu pekee, yu pekee.
Anatutayarishia enzi,
yu pekee, yu pekee.


Tazama Tenzi za Rohoni 1–164


Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

Scroll to Top